Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba mlango mmoja miongoni mwa milango ya Pepo unaitwa: Mlango wa Rayyan, wataingia hapo wafungaji siku ya Kiyama, hatoingia yeyote zaidi yao, patanadiwa: Wako wapi wafungaji, basi watasimama na wataingia, hatoingia hapo yeyote zaidi yao, atakapomaliza kuingia wa mwisho wao utafungwa, na hatoingia tena yeyote.
- Amesema Nawawi: Katika hadithi hii kuna ubora wa swaumu na heshima kwa wafungaji.
- Mwenyezi Mungu amewatengea wafungaji mlango katika milango minane ya Pepo, watakapouingia utafungwa.
- Kumebainishwa kuwa Pepo inamilango.
- Amesema Assanadi: Kauli yake: "Wako wapi wafungaji", yaani: Wenye kukithirisha kufunga, kama mtu muadilifu na dhalimu, husemwa kwa mtu aliyezoea hilo, na si kwa mwenye kufanya hilo mara moja.
- "Rayyan" Yaani: Mwenye kukata kiu; kwa sababu wafungaji hupata kiu na hasa hasa katika siku za kiangazi zenye joto la muda mrefu; watalipwa kwa kuitwa mlango huu kwa kile kilichokuwa kinawahusu wao, mlango wa Rayyan, na imesemekana kuwa Rayyan ni wingi wa kulowesha koo kinyume cha kiu, na umeitwa hivyo; kwa sababu ndio malipo ya wafungaji kwa kiu yao na njaa yao.
صحيح البخاري (3/ 25) (1896). صحيح مسلم (2/ 808) (1152). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 360). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 868). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 270).