Mtume rehema na amani ziwe juu yake amewahimiza wenye uwezo wa tendo la ndoa na gharama ya ndoa waoe; kwani hilo Iinahifadhi macho yake kutokana na mambo yaliyokatazwa, linalinda usafi wake wa mwili, na linamzuia asiingie katika uasherati, ambaye hawezi kukidhi mahitaji ya ndoa hali ya kuwa ana uwezo wa kufanya tendo la ndoa basi ni lazima afunge, kwani hii itakata matamanio ya tupu na shari ya manii.
- Uislamu umechunga sana sababu za mtu kujizuia na machafu na kusalimika na machafu.
- Himizo la kufunga swaum kwa ambaye hatoweza gharama za ndoa; kwa sababu hudhoofisha matamanio.
- Kufunga kunafananishwa na kuhasiwa; Kwa sababu kuhasi ni kuchubua mishipa ya korodani mbili, na kwa kitendo hicho hupotea matamani ya tendo la ndoa, hivyo hivyo swaumu hudhoofisha hamu ya tendo la ndoa.
صحيح البخاري (3/ 26) (1905). صحيح مسلم (2/ 1018) (1400). الإلمام بشرح عمدة الأحكام للشيخ ،لإسماعيل الأنصاري (2/ 57). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص565). خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص281).