Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Asiswali mmoja wenu katika nguo moja ambayo hakuna chochote mabegani mwake

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لاَ يُصَلِّي أَحَدُكُمْ فِي الثَّوْبِ الوَاحِدِ لَيْسَ عَلَى عَاتِقَيْهِ شَيْءٌ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Asiswali mmoja wenu katika nguo moja ambayo hakuna chochote mabegani mwake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kuswali katika nguo moja kutoyaacha wazi mabega yake na shingo yake kiasi kwamba haweki chochote chenye kumsitiri; kwa sababu mabega mawili hata kama si uchi; ila kuyasitiri yanawezekana wakati wa kusitiri uchi, na ni jambo lililo karibu na kumheshimu na kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu wakati wa kusimama mbele yake katika swala.

Mafunzo
  1. Inafaa kuswali katika nguo moja ikiwa itasitiri sehemu za wajibu kusitiriwa.
  2. Inafaa kuswali katika nguo mbili, moja inasitiri juu ya mwili, na nyingine inasitiri chini yake.
  3. Inapendeza na ni sunna mwenye kuswali awe katika muonekano mzuri.
  4. uwajibu wa kufunika mabega mawili au moja ndani ya swala, akiweza kufanya hivyo, na imesemekana kuwa katazo ni la kujitakasa (mbele ya Mwenyezi Mungu).
  5. Uchache wa yale waliyoyamiliki Maswahaba katika mali, mpaka utakuta mmoja wao hamiliki nguo mbili.
  6. Amesema Imam Nawawi katika maana ya hadithi: Hekima yake nikuwa akijifunga chini na kukawa juu ya mabega yake hakuna kitu basi hatosalimika na kutofunuka uchi wake, tofauti na ambavyo atakaiweka sehemu ya nguo juu ya bega lake, na ni kwa sababu anaweza kuhitaji kuishika kwa mkono wake au mikono yake akashughulishwa na hilo, na ikampita sunna ya kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto chini ya kifua chake, na kuinyanyua kwake pale ambapo ni sheria kuinyanyua, na mengineyo, kwa sababu ndani yake kuna kuacha kusitiri juu ya mwili na sehemu ya pambo, na alisema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Chukueni pambo lenu katika kila msikiti" [Al-Araf: 31].
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 81) (359). صحيح مسلم (1/ 368) (516). سبل السلام، لمحمد الصنعاني (1/ 198). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (2/ 8). فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (1/ 501). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (2/ 330). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص203).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Masharti ya Swala.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com