Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Masharti ya Swala.

Hadithi 4

Alichelewesha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- swala ya ishaa, akatoka Omar, akasema: Swala Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wamelala wanawake na watoto, akatoka na kichwa chake kikitona maji akisema: Lau kama nisingehofia kuwapa tabu umma wangu basi ningewaamrisha swala hii waiswali wakati huu

عن عَبْد اللَّهِ بْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما قال: «أّعْتَمَ النَبِيُّ -صلَّى الله عليه وسلَّم- بِالعِشَاء، فَخَرَج عُمَر فقال: الصَّلاةَ يا رسول الله، رَقَد النِسَاءُ والصِّبيَان. فَخَرَجَ ورَأسُهُ يَقطُر يقول: لَولاَ أن أَشُقَّ عَلَى أُمَّتِي -أو على النَّاس- لَأَمَرتُهُم بهذه الصَّلاة هذه السَّاعَة».
Kutoka kwa Abdillahi bin Abbas -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: "Alichelewesha Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- swala ya Ishaa, akatoka Omar, akasema: Swala Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wamelala wanawake na watoto, akatoka na kichwa chake kikitona maji akisema: Lau kama nisingehofia kuwapa tabu umma wangu basi ningewaamrisha swala hii waiswali wakati huu".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alichelewa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika swala ya ishaa, mpaka usiku ukawa mkubwa,na wakalala wanawake na watoto, miongoni mwa wale wasiokuwa na uwezo wa kuvumilia kusubiri kwa muda mrefu, akaenda kwake Omar bin Khattwab -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- na akasema: Swala, hakika wamelala wanawake na watoto. Akaja-Rehema na Amani ziwe juu yake- kutoka nyumbani kwake akielekea msikitini na kichwa chake kikitona maji kwasababu ya kuoga na akazungumza kwa kulibainisha hilo kuwa kilichobora katika swala ya ishaa ni kuichelewesha, lau kama si tabu wanazozipata wale wenye kuisubiri swala: Lau kama nisingehofia tabu kwa umma wangu basi ningewaamrisha swala hii katika wakati huu wakuchelewa.

Marejeo

الإلمام بشرح عمدة الأحكام لإسماعيل الأنصاري، ط1، دار الفكر، دمشق، 1381هـ تيسير العلام شرح عمدة الأحكام للبسام، حققه وعلق عليه وخرج أحاديثه وصنع فهارسه: محمد صبحي بن حسن حلاق، ط10، مكتبة الصحابة، الإمارات - مكتبة التابعين، القاهرة، 1426 هـ تنبيه الأفهام شرح عمدة لأحكام لابن عثيمين، ط1، مكتبة الصحابة، الإمارات، 1426هـ عمدة الأحكام من كلام خير الأنام صلى الله عليه وسلم لعبد الغني المقدسي، دراسة وتحقيق: محمود الأرناؤوط، مراجعة وتقديم: عبد القادر الأرناؤوط، ط2، دار الثقافة العربية، دمشق ، بيروت، مؤسسة قرطبة، 1408 هـ صحيح البخاري، تحقيق: محمد زهير بن ناصر الناصر، ط1، دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم: محمد فؤاد عبد الباقي)، 1422هـ. صحيح مسلم، تحقيق: محمد فؤاد عبد الباقي، دار إحياء التراث العربي، بيروت، 1423 هـ.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Asiswali mmoja wenu katika nguo moja ambayo hakuna chochote mabegani mwake

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لاَ يُصَلِّي أَحَدُكُمْ فِي الثَّوْبِ الوَاحِدِ لَيْسَ عَلَى عَاتِقَيْهِ شَيْءٌ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake: "Asiswali mmoja wenu katika nguo moja ambayo hakuna chochote mabegani mwake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kuswali katika nguo moja kutoyaacha wazi mabega yake na shingo yake kiasi kwamba haweki chochote chenye kumsitiri; kwa sababu mabega mawili hata kama si uchi; ila kuyasitiri yanawezekana wakati wa kusitiri uchi, na ni jambo lililo karibu na kumheshimu na kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu wakati wa kusimama mbele yake katika swala.

Mafunzo
  1. Inafaa kuswali katika nguo moja ikiwa itasitiri sehemu za wajibu kusitiriwa.
  2. Inafaa kuswali katika nguo mbili, moja inasitiri juu ya mwili, na nyingine inasitiri chini yake.
  3. Inapendeza na ni sunna mwenye kuswali awe katika muonekano mzuri.
  4. uwajibu wa kufunika mabega mawili au moja ndani ya swala, akiweza kufanya hivyo, na imesemekana kuwa katazo ni la kujitakasa (mbele ya Mwenyezi Mungu).
  5. Uchache wa yale waliyoyamiliki Maswahaba katika mali, mpaka utakuta mmoja wao hamiliki nguo mbili.
  6. Amesema Imam Nawawi katika maana ya hadithi: Hekima yake nikuwa akijifunga chini na kukawa juu ya mabega yake hakuna kitu basi hatosalimika na kutofunuka uchi wake, tofauti na ambavyo atakaiweka sehemu ya nguo juu ya bega lake, na ni kwa sababu anaweza kuhitaji kuishika kwa mkono wake au mikono yake akashughulishwa na hilo, na ikampita sunna ya kuweka mkono wa kulia juu ya mkono wa kushoto chini ya kifua chake, na kuinyanyua kwake pale ambapo ni sheria kuinyanyua, na mengineyo, kwa sababu ndani yake kuna kuacha kusitiri juu ya mwili na sehemu ya pambo, na alisema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Chukueni pambo lenu katika kila msikiti" [Al-Araf: 31].
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 81) (359). صحيح مسلم (1/ 368) (516). سبل السلام، لمحمد الصنعاني (1/ 198). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (2/ 8). فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (1/ 501). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (2/ 330). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص203).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Msikae juu ya makaburi, na wala msisali kwa kuyaelekea

عن أبي مَرْثَدٍ الغَنَوِيّ رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «لَا تَجْلِسُوا عَلَى الْقُبُورِ، وَلَا تُصَلُّوا إِلَيْهَا».
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Marthad Al-Anawiy -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Msikae juu ya makaburi, na wala msisali kwa kuyaelekea".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Amekataza -Rehema na amani ziwe juu yake- kukaa juu ya makaburi. Kama alivyokataza kusali kwa kuyaelekea makaburi, kwa kaburi kuwa upande wa kibla cha mwenye kusali; kwa sababu hilo ni katika njia za shirki.

Mafunzo
  1. Katazo la kusali makaburini au kati kati yake au kuyaelekea, isipokuwa swala ya jeneza kama ilivyothibiti katika mafundisho ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
  2. Katazo la kusali kwa kuyaelekea makaburi ni kuziba mianya ya kuingia katika ushirikina.
  3. Uislamu umekataa kuchupa mipaka katika makaburi na kuyadhalilisha pia, hakuna kuyapuuza wala kuyatukuza.
  4. Heshima ya muislamu inabakia hata baada ya kufa kwake, kwa kauli yake -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Kuvunja mfupa wa maiti ni kama kuuvunja akiwa hai".
Marejeo

صحيح مسلم (2/ 668) (972). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (2/ 30). فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لمحمد العثيمين (1/ 522). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (4/ 285).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Imenyanyuliwa kalamu kwa watu wa aina tatu: Kwa aliyelala mpaka aamke, na kwa mtoto mdogo mpaka abalehe, na kwa mwendawazimu mpaka apate akili

عن علي رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «رُفِعَ الْقَلَمُ عن ثلاثة: عن النائم حتى يَسْتَيْقِظَ، وعن الصبي حتى يَحْتَلِمَ، وعن المجنون حتى يَعْقِلَ».
Imepokelewa kutoka kwa Othman -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Imenyanyuliwa kalamu kwa watu wa aina tatu: Kwa aliyelala mpaka aamke, na kwa mtoto mdogo mpaka abalehe, na kwa mwendawazimu mpaka apate akili".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kubeba wajibu ni lazima kwa mwanadam isipokuwa hawa watatu: Mtoto mdogo mpaka akue na abalehe. Na kwa mwendawazimu aliyepoteza akili mpaka akili irudi. Na kwa aliyelala mpaka aamke. Kubeba wajibu kumeondolewa kwao, na kutenda kwao madhambi hakuandikwi, lakini mtoto huandikiwa kheri anapofanya, isipokuwa mwendawazimu na aliyelala; kwa sababu wote hawa wako katika kundi la mtu asiyekubalika ibada yake kwa kupoteza hisia.

Mafunzo
  1. Kupoteza uwezo wa mtu hutokea ima kwa sababu ya usingizi, ambao unamzuia kuwa na uwezo wa kuwa macho ili kutekeleza wajibu wake, au kwa sababu ya umri wake mdogo na utoto, ambao unamfanya kupoteza uwezo, au kwa sababu ya wendawazimu ambao huvuruga kazi za akili yake, au kinachofananishwa na hayo kama vile ulevi, atakayepoteza uwezo sahihi wa kupambanua na kufikiri, akakosa sifa kwa sababu ya sababu hizi tatu, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa uadilifu Wake na upole wake na ukarimu Wake amemuondolea dhambi kwa yale yanayotokea kwa makusudi au uzembe katika haki za Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  2. Kutoandika dhambi zao hakufuti baadhi ya hukumu za kidunia dhidi yao; kama mwendawazimu akiua, hakuna kisasi wala kafara kwake, na mtu wake mwenye akili timamu lazima alipe fidia.
  3. Kubalehe kuna dalili tatu: Kutokwa na manii, kwa kujiotea au kwa kinginecho, au kuota nywele sehemu za siri, au kutimiza miaka kumi na tano, na linaongezeka jambo la nne kwa mwanamke: nalo ni hedhi.
  4. Amesema Al-Subki: Mtoto kijana, na wengine wakasema: Mtoto aliye tumboni mwa mama yake anaitwa kijusi, akizaliwa anaitwa mvulana, na akiachishwa kunyonya, basi ni mvulana mpaka saba, basi anakuwa kijana mpaka kumi, kisha mdogo hadi kumi na tano, na kilicho yakini ni kwamba anaitwa mvulana katika matukio yote haya, alisema Al-Suyuti.
Marejeo

سنن أبي داود (6/ 455) (4403). سنن الترمذي (3/ 93) (1423). السنن الكبرى للنسائي (6/ 487) (7303). سنن ابن ماجه (3/ 199) (2042). مسند أحمد (2/ 254) (940). فتح ذي الجلال والاكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (5/ 57). توضِيحُ الأحكَامِ مِن بُلوُغ المَرَام، للبسام (3/ 327). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (7/ 582).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com