Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi bin Masoud -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alitajwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake mtu mmoja aliyelala usiku mpaka pakapambazuka, akasema: "Huyo ni mtu aliyekojolewa na Shetani ndani ya masikio yake, au alisema: ndani ya sikio lake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Alitajwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake mtu mmoja aliyelala mpaka pakapambazuka na Jua likachomoza na wala hakunyanyuka kwenda katika swala ya faradhi, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Huyo ni mtu ambaye Shetani kakojoa ndani ya sikio lake.
Mafunzo
Ni karaha kuacha kusimama usiku, nakuwa hilo ni kwa sababu ya Shetani.
Kutahadhari na Shetani anayemkalia mwanadam katika njia zote; ili amkinge na kuzuia kati yake na kumtii Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Amesema bin Hajari: Kauli yake: "Hakusimama kuswali" Makusudio yake ni aina ya sala, na inawezekana kuwa ni ahadi, na inakusudiwa ni swala ya usiku au swala ya faradhi.
Amesema Twaibi: Limetajwa sikio pekee, japokuwa jicho ndio linastahiki zaidi kulala ikiwa ni ishara ya uzito wa usingizi, kwa sababu masikio ndio nyenzo za umakini, na umetajwa mkojo; kwa sababu ndio mwepesi kupenya katika njia za sikio, na mwepesi kutembea katika mishipa, na kusababisha uvivu katika viungo vyote.
Marejeo
صحيح البخاري (4/ 122) (3270).
صحيح مسلم (1/ 537) (774).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (2/ 328).
نزهة المتقين، لمجموعة من الباحثين (2/ 834).
فتح الباري شرح صحيح البخاري، لأحمد العسقلاني (3/ 28).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 193).
المنهاج شرح صحيح مسلم بن الحجاج، النووي (6/ 64).
عن عمرو بن شُعيب عن أبيه عن جدِّه قال: قال رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: «مُرُوا أولادكمِ بالصلاةِ وهم أبناءُ سبعِ سِنينَ، واضرِبوهم عليها وهم أبناءُ عَشرٍ، وفرِّقوا بينهم في المَضاجِعِ».
Kutoka kwa Amri Bin Shuab kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Waamrisheni watoto wenu kuswali nao wakiwa watoto wa miaka saba, na wapigeni kwa ajili yake nao wakiwa watoto wa miaka kumi, na watenganisheni baina yao katika malazi".
Imepokelewa na Abu DaudDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa baba awaamrishe watoto wake wa kiume na wa kike kusali na umri wao ukiwa mikaa saba, na awafundishe wanayoyahitaji kwa ajili ya kuitekeleza. Na wakifikisha miaka kumi azidi kutilia mkazo, awapige wanapofanya uzembe, na awatenganishe katika vitanda.
Mafunzo
Kuwafundisha dini watoto wadogo kabla hawajabalehe, na hasa hasa swala.
Kipigo kinakuwa ni kwa ajili kutia adabu, nasi kwa kuadhibu, apige kipigo kinachoendana na hali yake.
Sheria imetilia umuhimu kuhifadhi heshima, na kuziba kila njia inayopelekea kuiharibu.
Marejeo
سنن أبي داود (1/ 367) (495، 496).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 299).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 382).
عن بريدة بن الحصيب رضي الله عنه أنه قال: بَكِّرُوا بِصَلَاةِ الْعَصْرِ، فَإِنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ تَرَكَ صَلَاةَ الْعَصْرِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ».
Kutoka kwa Buraida -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa amesema: Iswalini mapema swala ya Lasiri, kwani Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayeacha swala ya Lasiri basi yameporomoka matendo yake".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Ametahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuchelewesha swala ya Lasiri nje ya wakati wake kwa makusudi, nakuwa mwenye kufanya hivyo yatakuwa yamebatilika matendo yake na yameharibika matendo yake na yameenda patupu.
Mafunzo
Himizo la kuihifadhi swala ya Lasiri mwanzo wa wakati wake na kuiharakisha.
Ahadi ya dhabu kali kwa atakayeiacha swala ya Lasiri ambayo ni swala ya kati kati, na kuitoa nje ya wakati wake maalum kwa amri iliyokuja katika kauli yake Mtukufu: "Zihifadhini swala na swala ya kati kati" [Al-Baqara: 238].
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 115) (553).
مسند أحمد (38/ 152) (23045).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 56).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (2/ 777).
فيض القدير شرح الجامع الصغير (3/ 206).
بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (2/ 260).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص614).
عَنْ عَبْدِ اللهِ بنِ عُمَر رضي الله عنهما قال: قال رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: «بُنِيَ الْإِسْلَامُ عَلَى خَمْسٍ: شَهَادَةِ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، وَإِقَامِ الصَّلَاةِ، وَإِيتَاءِ الزَّكَاةِ، وَحَجِّ الْبَيْتِ، وَصَوْمِ رَمَضَانَ».
kutoka kwa Abdullahi bin Amry -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Umejengwa uislamu kwa mambo matano: Kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, nakuwa Muhammadi ni Mja wake na Mtume wake, na kusimamisha swala, na kutoa zaka, na kuhiji nyumba tukufu, na kufunga ramadhani".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameufananisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Uislamu na jengo madhubuti kwa nguzo zake tano zenye kulibeba jengo hilo, na mambo mengine ya Uislamu kama nyenzo zenye kulikamilisha jengo hilo, Na nguzo ya kwanza katika nguzo hizo ni: Shahada mbili; Kushuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nakuwa Muhammadi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hizo mbili ni nguzo moja; kila moja haitengani na nyingine, mja anazitamka kwa kukiri umoja wa Mwenyezi Mungu na kustahiki kwake kuabudiwa yeye pekee pasina mwingine, na kufanyia kazi makusudio ya nguzo hii, na kwa kuamini utume wa Muhammadi -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa kumfuata yeye. Na nguzo ya pili: Ni kusimamisha swala, nazo ni swala tano za faradhi usiku na mchana: Alfajiri, Adhuhuri, lasiri, Maghribi, na Ishaa, kwa sharti zake na nguzo zake na wajibu wake. Na nguzo ya tatu: Ni kutoa zaka ya lazima, nayo ni ibada ya mali ya wajibu katika kila mali iliyofikia kiwango maalumu katika sheria, ambayo hupewa wastahiki wake. Na nguzo ya nne: Ni Hija, nayo nikutia nia ya kwenda Makka kwa ajili ya kutekeleza ibada, kwa kumuabudu Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka. Na nguzo ya tano: Ni kufunga mwezi wa Ramadhani, nako ni kujizuia na kula na kunywa na vinginevyo miongoni mwa vyenye kufunguza kwa nia ya kumuabudu Mwenyezi Mungu, kuanzia kuchomoza kwa Alfajiri mpaka kuzama jua.
Mafunzo
Nguzo mbili zinakwenda sambamba, haikubaliki moja mpaka iwe na nyingine; ndio maana akazifanya kuwa nguzo moja.
Shahada mbili ndio msingi wa Dini, haikubaliki kauli wala amali ila kwa shahada hizo.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 11) (8)، صحيح مسلم (1/ 45) (16)، و(1/ 88) (82)، فتح الباري لابن رجب (1/ 22)، جامع العلوم والحكم (1/147)، شرح الأربعين لابن العطّار (ص 62)، شرح الأربعين النووية لعبد الكريم الخضير (ص 87)، فتح القوي المتين في شرح الأربعين للعباد (ص 29)، شرح الأربعين النووية لصالح آل الشيخ (ص 91 - 95)، التحفة الربانية لإسماعيل الأنصاري (ص 12).
عن أَنَسَ بْنَ مَالِكٍ رضي الله عنه قال: بينما نحن جلوس مع النبي صلى الله عليه وسلم في المسجد دخل رجل على جمل، فأناخه في المسجد ثم عقله، ثم قال لهم: أيكم محمد؟ والنبي صلى الله عليه وسلم متكئ بين ظهرانيهم، فقلنا: هذا الرجل الأبيض المتكئ. فقال له الرجل: يا ابن عبد المطلب فقال له النبي صلى الله عليه وسلم: «قد أجبتك». فقال الرجل للنبي صلى الله عليه وسلم: إني سائلك فمشدد عليك في المسألة، فلا تجد علي في نفسك؟ فقال: «سل عما بدا لك» فقال: أسألك بربك ورب من قبلك، آلله أرسلك إلى الناس كلهم؟ فقال: «اللهم نعم». قال: أنشدك بالله، آلله أمرك أن نصلي الصلوات الخمس في اليوم والليلة؟ قال: «اللهم نعم». قال: أنشدك بالله، آلله أمرك أن نصوم هذا الشهر من السنة؟ قال: «اللهم نعم». قال: أنشدك بالله، آلله أمرك أن تأخذ هذه الصدقة من أغنيائنا فتقسمها على فقرائنا؟ فقال النبي صلى الله عليه وسلم: «اللهم نعم». فقال الرجل: آمنت بما جئت به، وأنا رسول من ورائي من قومي، وأنا ضمام بن ثعلبة أخو بني سعد بن بكر.
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Wakati mmoja tulipokuwa tumekaa Msikitini pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- aliingia mtu mmoja akiwa juu ya Ngamia, akampigisha magoti Ngamia ndani ya Msikiti kisha akamfunga, kisha akawaambia Maswahaba: Kati yenu Muhammad ni nani? Na wakati huo Mtume -Rehema na mani ziwe juu yake- akiwa kati yao amekaa kwa kuegemea, tukasema ni huyu mtu mweupe aliyeegemea, yule mtu akamwambia: Ewe mtoto wa Abdul Muttwalib, basi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-akasema: "Nimekuitikia" Yule bwana akamwambia Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake- Hakika mimi nitakuuliza nanitatia mkazo katika kuuliza, hivyo usinichukie kwenye moyo wako, na wala usiona tabu kunijibu, akasema: "Uliza unachotaka" Akasema: Nanakuuliza kwa jina la Mola wako na Mola wa waliokuwa kabla yako, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekutuma kwa watu wote? Akasema: "Ndiyo, ni kweli" Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu ametuamrisha sisi tusali sala tano usiku na mchana? Akasema:"Ndiyo, ni kweli" Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha kuwa sisi tufunge Mwezi huu kila Mwaka? Akasema: "Ndiyo, ni kweli" Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha kuwa uchukue hizi sadaka kutoka kwa matajiri na uzigawanye kwa mafukara wetu? Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Ndiyo, ni kweli" Basi yule bwana akasema: Nimeamini yote yale uliyokuja nayo, na mimi ni mjumbe kuna wanaonifuata nyuma yangu, na mimi ndiye ninaitwa Dhwamam Bin Thaalaba ndugu wa Banii Saad Bin Bakri."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anatoa habari Anas Bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Wakati mmoja Maswahaba walikuwa wamekaa pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Msikitini aliingia mtu mmoja akiwa juu ya Ngamia, basi akampigisha magoti kisha akamfunga Ngamia wake, Kisha akawauliza: Kati yenu Muhammad ni nani? Na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa amekaa kati ya watu na ameegemea, tukamwambia: Ni mtu huyu mweupe aliyeegemea, Yule bwana akamwambia: Ewe mtoto wa Abdul Muttwalib, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Nimekusikia, basi uliza nitakujibu. Yule bwana akamwambia Mtume -Rehema na mani ziwe juu yake-: Mimi nitakuuliza na nitakuuliza kwa msisitizo mkubwa hivyo usinichukie wala usione dhiki katika nafsi yako. Yaani: Usinikasirikie wala usione dhiki, Akasema: Uliza unachotaka, Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mola wako na Mola wa waliokuwa kabla yako, Je ni kweli Mwenyezi Mungu amekutuma kwa watu wote? Akasema: Ndiyo ni kweli, hali ya kutilia mkazo ukweli wake, Yule bwana akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha yakuwa sisi tusali sala tano usiku na mchana? Nazo ni sala za faradhi, Akasema: Ndiyo ni kweli, Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha yakuwa sisi tuufunge Mwezi huu katika kila Mwaka? Yaani Mwezi wa Ramadhan, Akasema: Ndiyo ni kweli, Akasema: Ninakuuliza kwa jina la Mwenyezi Mungu, je ni kweli Mwenyezi Mungu amekuamrisha kuwa uchukue hizi sadaka kutoka kwa matajiri wetu kisha uzigawe kwa mafukara wetu? Na sadaka hiyo ni Zaka, Basi akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-Ndiyo ni kweli, Basi Dhwamamu akasilimu, na akamwambia Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yeye atawalingania watu wake kuingia kwenye uislamu, kisha akajitambulisha kuwa yeye ni Dhwammam Bin Thaalabah atokanae na kabila la Banii Saad Bin Bakri.
Mafunzo
Unyenyekevu wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa namna ambayo hakuweza mtu yule kumtofautisha kati ya Mtume na Maswahaba zake.
Uzuri wa tabia za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- upole wake katika kumjibu muulizaji, na kuwa kurudisha majibu mazuri ni miongoni mwa sababu ya kukubalika Daawa.
Inafaa mtu kujitambulisha kwa sifa ya rangi ya weupe au wekundu, na urefu na ufupi, na mfano wa sifa hizo ikiwa haikusudiwi kuaibisha, ikiwa msifiwa hatochukia sifa hizo.
Yafaa kwa Kafiri kuingia Msikitini kwa haja maalumu.
Haikutajwa Hijja katika hadithi kwa sababu hueda ikawa Hijja ilikuwa haijafaradhishwa wakati wakuja kwake.
Pupa ya Maswahaba ya kuwalingania watu; Basi kwa muda mfupi tu baada ya kusilimu kwake alikuwa na pupa ya kuwalingania watu wake.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 23) (63)، صحيح مسلم (1/ 41) (12)، شرح ابن بطال (1/145)، عمدة القاري شرح صحيح البخاري (2/ 22).
عن أنس بن مالك رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ نَسِيَ صَلَاةً فَلْيُصَلِّ إِذَا ذَكَرَهَا، لَا كَفَّارَةَ لَهَا إِلَّا ذَلِكَ: {وَأَقِمِ الصَّلاةَ لِذِكْرِي} [طه: 14]».
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakayeisahau swala, basi aiswali atakapoikumbuka, haina kafara nyingine isipokuwa hiyo: "Na simamisha swala kwa ajili ya kunitaja mimi" [Twaha: 14].
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayesahau kutekeleza swala ya faradhi mpaka ukatoka wakati wakati wake, basi anatakiwa aende mbio na afanye haraka kuilipa pale anapoikumbuka, amesema Allah katika kitabu chake kitukufu: "Na usimamishe swala kwa ajili ya kunitaja" [Twaha: 14] Simamisha swala zilizosahaulika unapozikumbuka.
Mafunzo
Umuhimu swala na kutozembea katika kuitekeleza na kuilipa.
Haitakiwi kuichelewesha swala nje ya wakati wake kwa makusudi bila udhuru.
Uwajibu wa kulipa swala kwa aliyesahau na aliyesinzia mpaka atakapo amka.
Uwajibu wa kulipa swala haraka hata kama ni katika nyakati zilizoharamishwa.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 122) (597)، صحيح مسلم (1/ 477) (684)، فتح الباري لابن حجر (2/ 71)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (14/ 612).
عن جابرٍ رضي الله عنه قال: سمعت النبي صلى الله عليه وسلم يقول: «إِنَّ بَيْنَ الرَّجُلِ وَبَيْنَ الشِّرْكِ وَالْكُفْرِ تَرْكَ الصَّلَاةِ».
Imepokewa kutoka kwa Jabiri -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika kilicho kati ya mtu na ushirikina na ukafiri ni kuacha swala".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anatahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuacha swala ya faradhi, na akaeleza kuwa kati ya mtu na baina ya kuingia katika shirki na ukafiri ni kuacha swala, swala ni nguzo ya pili katika nguzo za Uislamu, na jambo lake ni kubwa katika Uislamu, atakayeiacha kwa kupinga uwajibu wake amekufuru kwa makubaliano ya waislamu, na akiiacha moja kwa moja kwa uzembe na uvivu pia ni kafiri, na yamenukuliwa makubaliano ya Masahaba juu ya hilo, na ikiwa anaiacha baadhi ya wakati na wakati mwingine anaswali, basi anajitia katika makemeo haya makubwa.
Mafunzo
Umuhimu wa swala na kuihifadhi, kwani ndio inayotenganisha kati ya ukafiri na imani.
Tahadhari kubwa kwa atakayeacha swala na akaitelekeza.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 88) (82)، المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (1/ 271)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (2/ 622).
عن بريدة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «إِنَّ الْعَهْدَ الَّذِي بَيْنَنَا وَبَيْنَهُمُ الصَّلَاةُ، فَمَنْ تَرَكَهَا فَقَدْ كَفَرَ».
Kutoka kwa Buraida -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Hakika ahadi iliyopo kati yetu na wasiokuwa waislamu ni sala, na atakayeiacha sala basi huyo ni kafiri".
Imepokelewa na Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa ahadi na mkataba kati ya waislamu na wasiokuwa wao katika makafiri na wanafiki ni swala, atakayeiacha atakuwa amekufuru.
Mafunzo
Ukubwa wa jambo la swala, nakuwa ndio kitenganishi kati ya waumini na makafiri.
Kudhihiri hukumu za Uislamu kwa muonekano wa hali ya mtu pasina ndani ya moyo wake.
Marejeo
سنن النسائي (1/ 231) (463)، سنن الترمذي (4/ 365) (2621)، سنن ابن ماجه (2/ 181) (1079)، مسند أحمد (38/ 20) (22937)، فيض القدير (4/ 395)، ذخيرة العقبى في شرح المجتبى (6/ 192) (6/ 193).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com