Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Waamrisheni watoto wenu kuswali nao wakiwa watoto wa miaka saba, na wapigeni kwa ajili yake nao wakiwa watoto wa miaka kumi, na watenganisheni baina yao katika malazi

عن عمرو بن شُعيب عن أبيه عن جدِّه قال: قال رسولُ الله صلى الله عليه وسلم: «مُرُوا أولادكمِ بالصلاةِ وهم أبناءُ سبعِ سِنينَ، واضرِبوهم عليها وهم أبناءُ عَشرٍ، وفرِّقوا بينهم في المَضاجِعِ».
Kutoka kwa Amri Bin Shuab kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Waamrisheni watoto wenu kuswali nao wakiwa watoto wa miaka saba, na wapigeni kwa ajili yake nao wakiwa watoto wa miaka kumi, na watenganisheni baina yao katika malazi".
Imepokelewa na Abu DaudDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa baba awaamrishe watoto wake wa kiume na wa kike kusali na umri wao ukiwa mikaa saba, na awafundishe wanayoyahitaji kwa ajili ya kuitekeleza. Na wakifikisha miaka kumi azidi kutilia mkazo, awapige wanapofanya uzembe, na awatenganishe katika vitanda.

Mafunzo
  1. Kuwafundisha dini watoto wadogo kabla hawajabalehe, na hasa hasa swala.
  2. Kipigo kinakuwa ni kwa ajili kutia adabu, nasi kwa kuadhibu, apige kipigo kinachoendana na hali yake.
  3. Sheria imetilia umuhimu kuhifadhi heshima, na kuziba kila njia inayopelekea kuiharibu.
Marejeo

سنن أبي داود (1/ 367) (495، 496). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 299). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 382).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Wajibu wa Swala na Hukumu ya Mwenye kuiacha.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com