Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kuoga.

Hadithi 9

Sub-haana llaah, ametakasika Mwenyezi Mungu, hakika muumini hanajisiki

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنه: أَنَّهُ لَقِيَهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي طَرِيقٍ مِنْ طُرُقِ الْمَدِينَةِ وَهُوَ جُنُبٌ، فَانْسَلَّ فَذَهَبَ فَاغْتَسَلَ، فَتَفَقَّدَهُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَلَمَّا جَاءَهُ قَالَ: «أَيْنَ كُنْتَ يَا أَبَا هُرَيْرَةَ؟» قَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، لَقِيتَنِي وَأَنَا جُنُبٌ فَكَرِهْتُ أَنْ أُجَالِسَكَ حَتَّى أَغْتَسِلَ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «سُبْحَانَ اللهِ، إِنَّ الْمُؤْمِنَ لَا يَنْجُسُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Ya kwamba alikutana na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika barabara miongoni mwa barabara za mji wa Madina huku akiwa na janaba, akamkwepa na akaenda kuoga, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamtafuta hakumpata, alipomjia akasema: "Ulikuwa wapi ewe Abuu Huraira?" Akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ulikutana nami, nami nikiwa na janaba, sikufurahishwa kukaa na wewe mpaka nioge, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Sub-haana llaah, ametakasika Mwenyezi Mungu, hakika muumini hanajisiki".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alikutana Mtume rehema na amani ziwe juu yake na Abuu Huraira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake katika baadhi ya njia za Madina, na Abuu Huraira alikuwa na janaba, na kwa sababu ya kumuheshimu kwake Mtume rehema na amani ziwe juu yake alichukia kukaa naye na kuzungumza naye hali yakuwa yuko katika hali ile, kwa kudhani kwake kuwa yeye ni najisi, akaenda kwa uficho na akaoga, kisha akarejea na akakaa, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuuliza kuwa alikwenda wapi? Akamueleza kuhusu hali yake, na kwamba yeye alichukia kukaa naye hali yakuwa yeye ni najisi kwa sababu ya janaba, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akastaajabu, na akasema: Hakika muumini ni msafi na wala hanajisiki kwa hali yoyote; akiwa hai na hata wakiwa maiti.

Mafunzo
  1. Janaba linamzuia mtu kuswali na kugusa msahafu na kukaa msikitini, na wala halizuii kukaa pamoja na Waislamu na kukutana nao, na wala mwenye janaba hawi najisi.
  2. Usafi wa muumini akiwa hai au maiti.
  3. Kuwaheshimu watu wenye heshima, na elimu, na utengefu, na kukaa nao kwa muonekano mzuri.
  4. Hapa kuna sheria ya mfuasi kumuomba idhini ya kuondoka anayemfuata, kwani Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimkemea Abuu Huraira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kwa kuondoka kwake pasina yeye kujua, na hii ni kwa sababu kuomba ruhusa ni katika adabu nzuri.
  5. Kusema: Sub-haana llaah, ametakasika Mwenyezi Mungu, wakati wa kustaajabu.
  6. Kufaa mtu kusimulia mambo yake binafsi katika yale ya aibu, kwa ajili ya masilahi.
  7. Kafiri ni najisi, lakini najisi yake si ya kuonekana, kwa sababu ya uchafu wa itikadi yake.
  8. Amesema Nawawi: Na katika hadithi hii pia kuna adabu, ya kwamba msomi atakapoona kwa anayemfuata jambo analohofia kwake kwenda kinyume na usahihi basi amuulize, na amwambie lililo sahihi, na ambainishie hukumu yake, na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 65) (285). صحيح مسلم (1/ 282) (371). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 46). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص61). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 74).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Namna ya kuoga janaba

عَنْ مَيْمُونَةُ أُمِّ المؤمِنينَ رضي الله عنها قَالتْ: وَضَعْتُ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ غُسْلًا، فَسَتَرْتُهُ بِثَوْبٍ، وَصَبَّ عَلَى يَدَيْهِ، فَغَسَلَهُمَا، ثُمَّ صَبَّ بِيَمِينِهِ عَلَى شِمَالِهِ، فَغَسَلَ فَرْجَهُ، فَضَرَبَ بِيَدِهِ الأَرْضَ، فَمَسَحَهَا، ثُمَّ غَسَلَهَا، فَمَضْمَضَ وَاسْتَنْشَقَ، وَغَسَلَ وَجْهَهُ وَذِرَاعَيْهِ، ثُمَّ صَبَّ عَلَى رَأْسِهِ وَأَفَاضَ عَلَى جَسَدِهِ، ثُمَّ تَنَحَّى، فَغَسَلَ قَدَمَيْهِ، فَنَاوَلْتُهُ ثَوْبًا فَلَمْ يَأْخُذْهُ، فَانْطَلَقَ وَهُوَ يَنْفُضُ يَدَيْهِ.
Imepokelewa kutoka kwa Maimuna mama wa waumini Radhi za Allah ziwe juu yake, amesema: Nilimuandalia kuoga Mtume rehema na amani ziwe juu yake, nikamfunika nguo, na akamimina maji juu ya mikono yake na akaiosha, kisha akamimina maji kwa mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto, kwa hiyo, akaosha sehemu zake za siri na kuzisafisha, akapiga ardhi kwa mkono wake, akaufuta, kisha akauosha, kisha akasukutua kinywa chake na akapandisha maji puani, na akaosha uso na mikono, kisha akamwagia maji kichwani kwake na akaeneza mwili mzima, kisha akasogea pembeni na akaosha miguu yake, nikampa nguo, lakini hakuichukua, akaondoka huku akifuta mikono yake.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Mama wa Waumini Maimuna Mwenyezi Mungu amuwie radhi, alitueleza jinsi Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake alivyokuwa akioga janaba, kiasi kwamba alimuwekea maji ya kuoga, na akamfunika kwa pazia, basi Mtume, Rehema na amani ziwe juu yake, akafanya yafuatayo: Kwanza: Alimimina maji kwenye mikono yake na akaiosha kabla ya kuiingiza katika chombo. Pili: Alimimina maji kwa mkono wake wa kulia juu ya mkono wake wa kushoto na kuosha sehemu zake za siri ili kuisafisha kutokana na athari yoyote ya janaba. Tatu: Aliipiga ardhi kwa mkono wake, akaufuta, kisha akauosha ili kuondoa udhia. Nne: Alisukutukua; Kwa kuingiza maji katika kinywa chake na kuyazungusha, kisha kuyatema; na akavuta maji puani kwa pumzi yake, kisha akayatoa nje ili kuisafisha. Tano: Aliosha uso wake na mikono yake. Sita: Alimimina maji juu ya kichwa chake. Saba: Alimimina maji katika mwili wake mzima. Nane: Alitoka mahali alipoogea na akaosha miguu yake katika mahali pengine, kwani hakuiosha mwanzo. Kisha akamletea kitambaa ili ajifute kwacho, akawa hakukichukua, na akaanza kufuta maji kutoka mwilini kwake kwa mkono wake, na anayapangusa.

Mafunzo
  1. Wake za Mtume Rehema na amani ziwe juu yake, walitilia umuhimu wa kutoa sifa nyeti kabisa ya maisha yake; kwa ajili ya kuufundisha umma.
  2. Namna hii ya kuoga ni miongoni mwa namna ambazo zimethibiti kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika sifa kamili ya kuoga janaba. Ama namna inayotosheleza ni mtu kueneza mwili wake maji, pamoja na kusukutua na kupandisha maji puani.
  3. Kufuta mwili kwa kitambaa au kuacha baada ya kuoga au kutia udhu ni halali.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 63) (276). صحيح مسلم (1/ 254) (317). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص64). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (1/ 78).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapooga kwa ajili ya janaba, anaosha mikono yake, na anatawadha udhu wake ule wa swala, kisha anaoga

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المؤمنين رضي الله عنها قَالَتْ: كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا اغْتَسَلَ مِنَ الجَنَابَةِ، غَسَلَ يَدَيْهِ، وَتَوَضَّأَ وُضُوءَهُ لِلصَّلاَةِ، ثُمَّ اغْتَسَلَ، ثُمَّ يُخَلِّلُ بِيَدِهِ شَعَرَهُ، حَتَّى إِذَا ظَنَّ أَنَّهُ قَدْ أَرْوَى بَشَرَتَهُ، أَفَاضَ عَلَيْهِ المَاءَ ثَلاَثَ مَرَّاتٍ، ثُمَّ غَسَلَ سَائِرَ جَسَدِهِ، وَقَالَتْ: كُنْتُ أَغْتَسِلُ أَنَا وَرَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنْ إِنَاءٍ وَاحِدٍ، نَغْرِفُ مِنْهُ جَمِيعًا.
Imepokewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini Radhi za Allah ziwe juu yake: Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapooga kwa ajili ya janaba, anaosha mikono yake, na anatawadha udhu wake ule wa swala, kisha anaoga, kisha anaachanisha nywele zake kwa mkono wake, mpaka pale anapohisi kuwa ngozi yake yote imeenea maji, anajimwagia maji kwa michoto mitatu, kisha anaosha mwili wake wote uliobakia, na Aisha akasema: Nilikuwa nikioga mimi na Mtume Rehema na amani ziwe juu yake katika chombo kimoja, tukichota sote katika chombo hicho.
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake anapotaka kuoga janaba anaanza kwa kuosha mikono yake, kisha anatawadha kama anavyotawadha udhu wa swala, kisha anajimwagia maji katika mwili wake kisha anaachanisha nywele za kichwa chake kwa mikono yake, mpaka anapohisi kuwa maji yamefika katika maoteo ya nywele zake, na yameloanisha ngozi, anajimwagia maji kichwani mara tatu kisha anaosha mwili mzima. Na akasema Aisha Radhi za Allah ziwe juu yake: Nilikuwa nikioga mimi pamoja na Mtume Rehema na amani ziwe juu yake kutoka katika chombo kimoja, tukichota sote.

Mafunzo
  1. Josho lina aina mbili: Linalotosheleza na lilokuwa kamili, ama josho linalotosheleza ni mtu kunuia twahara, kisha akaeneza maji katika mwili wake ikiwa ni pamoja na kupandisha maji puani na kusukutua, na ama josho lilokuwa kuwa kamili ataoga kama alivyo oga Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika hadithi hii.
  2. Neno Janaba hutumika kwa kila aliyetoa manii, au kafanya tendo la ndoa hata kama hajamtoka.
  3. Inaruhusiwa mwanandoa kutazama uchi wa mwenzake, na kuoga pamoja katika chombo kimoja.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 63) (272، 273). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 48). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص62). خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص33).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayekuja miongoni mwenu kwa ajili ya Ijumaa basi na aoge

عن عَبْدِ اللهِ بْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: «‌مَنْ ‌جَاءَ ‌مِنْكُمُ ‌الْجُمُعَةَ فَلْيَغْتَسِلْ».
kutoka kwa Abdullahi bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Atakayekuja miongoni mwenu kwa ajili ya Ijumaa basi na aoge".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anasisitiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa atakayetaka kuja kwa ajili ya swala ya Ijumaa basi inapendeza kwake kuoga, mfano wa kuoga kwake josho la janaba.

Mafunzo
  1. Mkazo wa kuoga kwa ajili ya Ijumaa, nakuwa hilo ni sunna kwa muumini siku ya Ijumaa na ikiwa wakati anataka kwenda kuswali ndio bora zaidi.
  2. Kutilia manani swala la usafi na harufu nzuri ni katika tabia njema za muislamu na adabu zake, na amri inakuwa na mkazo zaidi wakati wa kukutana na watu na kukaa nao, hasa hasa katika mikusanyiko na swala za jamaa.
  3. Tamko katika hadithi linamuhusu mwenye uwajibu wa kuswali Ijumaa; kwa sababu yeye ndiye anayekwenda kuswali.
  4. Ni lazima kwa mwenye kwenda katika swala ya Ijumaa awe msafi, aoge ili harufu iondoke katika mwili wake na ajitie manukato, na ikiwa atatawadha pekee pia itatosha.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 81) (1294). صحيح مسلم (1/ 99) (103). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص239). تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، لابن عثيمين (2/ 302). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 192).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ni haki kwa kila muislamu aoge katika kila siku saba walau siku moja, aoshe ndani yake kichwa chake na mwili wake

عن أبي هريرة قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «حَقٌّ عَلَى كُلِّ مُسْلِمٍ أَنْ يَغْتَسِلَ فِي كُلِّ سَبْعَةِ أَيَّامٍ يَوْمًا، يَغْسِلُ فِيهِ رَأْسَهُ وَجَسَدَهُ».
Na imepokelewa katika sahihi Bukhari kutoka kwa Abuu Huraira Amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Ni haki kwa kila muislamu aoge katika kila siku saba walau siku moja, aoshe ndani yake kichwa chake na mwili wake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ni haki iliyotiwa mkazo kwa kila muislamu aliyebalehe mwenye akili timamu aoge katika kila siku saba za wiki siku moja, aoshe katika siku hiyo kichwa chake na mwili wake, kwa kutafuta twahara na usafi, na siku bora katika siku hizi ni siku ya Ijumaa, kama inavyojulikana kutoka katika baadhi ya riwaya, na kuoga siku ya Ijumaa kabla ya swala ni sunna iliyotiwa mkazo, hata kama atakuwa alioga siku ya Alhamisi kwa mfano, na kinachoiondoa katika uwajibu ni kauli ya Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake-: "Watu walikuwa wakifanya kazi na shughuli mbali mbali za kimaisha, na walikuwa wanapokwenda katika Ijumaa wanakwenda katika muonekano wao huo huo: Wakaambiwa: Basi mngeoga (Ingekuwa kheri)", kaipokea Bukhari, na katika riwaya yake nyingine: "Wakiwa na harufu" Yaani: Harufu ya jasho na mfano wake, lakini pamoja na hivyo wakaambiwa (Lau mgeoga ingekuwa bora), hivyo kwa wasiokuwa Masahaba wanahaja kubwa ya kulitekeleza hili.

Mafunzo
  1. Kutilia umuhimu na kujali kwa Uislamu swala la usafi na twahara.
  2. Kuoga siku ya Ijumaa kumependekezwa sana tena kwa mkazo kwa ajili ya swala.
  3. Kimetajwa kichwa, pamoja nakuwa kutajwa mwili kungetosha kukusanya na kichwa; Lakini ni kwa ajili ya kukitilia maanani.
  4. Ni wajibu kuoga kwa kila aliyepatwa na harufu mbaya, inayo waudhi watu.
  5. Siku muhimu zaidi kwa ajili ya kuoga ni siku ya Ijumaa; kwa sababu ya fadhila zake.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 5) (897)، (2/ 7) (903)، صحيح مسلم (2/ 582) (849)، عمدة القاري شرح صحيح البخاري (6/ 193)، إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (2/ 169)، التيسير بشرح الجامع الصغير للمناوي (1/951).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitusomesha Qur'ani katika kila hali madamu hana janaba

عَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُقْرِئُنَا القُرْآنَ عَلَى كُلِّ حَالٍ مَا لَمْ يَكُنْ جُنُبًا.
Kutoka kwa Ally radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitusomesha Qur'ani katika kila hali madamu hana janaba.
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Nasai, Ibn Majah na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwafundisha Maswahaba zake Qur'ani na akiwasomesha yeye mwenyewe katika hali zote madam hajawa katika hali ya janaba litokanalo na tendo la ndoa kwa wakeze.

Mafunzo
  1. Kutofaa kusoma Qur'ani kwa mwenye janaba mpaka aoge.
  2. Kufundisha kwa vitendo.
Marejeo

سنن الترمذي (1/ 214) (146). سنن أبي داود (1/ 164) (229). سنن النسائي (1/ 144) (265). سنن ابن ماجه (1/ 375) (594). مسند أحمد (2/ 61) (627). النهاية في غريب الحديث والأثر (917-167).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com