Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Vyenye kuwajibisha kutawadha.

Hadithi 1

Nilimwendea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nikitaka kuwa muislamu, akaniamrisha nioge kwa maji na mkunazi

عن قيس بن عاصم رضي الله عنه قال: أتيتُ النبيَّ صلى الله عليه وسلم أُريدُ الإسلامَ، فأَمَرَني أن أغتَسِلَ بماءٍ وسِدرٍ.
Kutoka kwa Kaisi bin Aswim -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimwendea Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nikitaka kuwa muislamu, akaniamrisha nioge kwa maji na mkunazi.
Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na NasaaiDarajaSahihi
Maelezo

Alikuja Kaisi bin Aswim kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akitaka kusilimu, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamuamrisha aoge kwa maji na mti wa mkunazi; kwakuwa majani yake hutumika katika usafi; na kwakuwa yana harufu nzuri.

Mafunzo
  1. Sheria ya kafiri kuoga anapoingia katika Uislamu.
  2. Thamani ya Uislamu na kutilia kwake umuhimu mwili na roho vyote kwa pamoja.
  3. Maji kuchanganyika na vitu safi haviyatoa katika twahara yake.
  4. Visimama badala ya mkunazi vifaa vya usafi vya kisasa, kama sabuni na mfano wake.
Marejeo

سنن أبي داود (1/ 266) (355)، سنن الترمذي (1/ 595) (605)، سنن النسائي (1/ 109) (188)، معالم السنن (1/111)، ذخيرة العقبى (4/131)، شرح سنن أبي داود للعباد (54/ 10).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com