Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Rulings of the Ritual Bath

Hadithi 1

Ni haki kwa kila muislamu aoge katika kila siku saba walau siku moja, aoshe ndani yake kichwa chake na mwili wake

عن أبي هريرة قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «حَقٌّ عَلَى كُلِّ مُسْلِمٍ أَنْ يَغْتَسِلَ فِي كُلِّ سَبْعَةِ أَيَّامٍ يَوْمًا، يَغْسِلُ فِيهِ رَأْسَهُ وَجَسَدَهُ».
Na imepokelewa katika sahihi Bukhari kutoka kwa Abuu Huraira Amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Ni haki kwa kila muislamu aoge katika kila siku saba walau siku moja, aoshe ndani yake kichwa chake na mwili wake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ni haki iliyotiwa mkazo kwa kila muislamu aliyebalehe mwenye akili timamu aoge katika kila siku saba za wiki siku moja, aoshe katika siku hiyo kichwa chake na mwili wake, kwa kutafuta twahara na usafi, na siku bora katika siku hizi ni siku ya Ijumaa, kama inavyojulikana kutoka katika baadhi ya riwaya, na kuoga siku ya Ijumaa kabla ya swala ni sunna iliyotiwa mkazo, hata kama atakuwa alioga siku ya Alhamisi kwa mfano, na kinachoiondoa katika uwajibu ni kauli ya Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake-: "Watu walikuwa wakifanya kazi na shughuli mbali mbali za kimaisha, na walikuwa wanapokwenda katika Ijumaa wanakwenda katika muonekano wao huo huo: Wakaambiwa: Basi mngeoga (Ingekuwa kheri)", kaipokea Bukhari, na katika riwaya yake nyingine: "Wakiwa na harufu" Yaani: Harufu ya jasho na mfano wake, lakini pamoja na hivyo wakaambiwa (Lau mgeoga ingekuwa bora), hivyo kwa wasiokuwa Masahaba wanahaja kubwa ya kulitekeleza hili.

Mafunzo
  1. Kutilia umuhimu na kujali kwa Uislamu swala la usafi na twahara.
  2. Kuoga siku ya Ijumaa kumependekezwa sana tena kwa mkazo kwa ajili ya swala.
  3. Kimetajwa kichwa, pamoja nakuwa kutajwa mwili kungetosha kukusanya na kichwa; Lakini ni kwa ajili ya kukitilia maanani.
  4. Ni wajibu kuoga kwa kila aliyepatwa na harufu mbaya, inayo waudhi watu.
  5. Siku muhimu zaidi kwa ajili ya kuoga ni siku ya Ijumaa; kwa sababu ya fadhila zake.
Marejeo

صحيح البخاري (2/ 5) (897)، (2/ 7) (903)، صحيح مسلم (2/ 582) (849)، عمدة القاري شرح صحيح البخاري (6/ 193)، إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (2/ 169)، التيسير بشرح الجامع الصغير للمناوي (1/951).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com