Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kuyasema vibaya matamanio ya nafsi na ya kimwili.

Hadithi 7

Hajawahi kujaza mwanadamu yeyote chombo chenye shari zaidi kama tumbo, kinamtosha mwanadamu kiasi kidogo cha chakula kinachoweza kumpa nguvu, ikiwa hakuna namna, basi theluthi moja (ya tumbo lake) iwe kwa ajili ya chakula chake, na theluthi moja ya kinywaji chake, na theluthi moja kwa ajili ya pumzi yake

عَنْ المِقْدَامِ بْنِ مَعْدِي كَرِبَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «مَا مَلأَ آدَمِيٌّ وِعَاءً شَرًّا مِنْ بَطْنٍ، بِحَسْبِ ابْنِ آدَمَ أَكَلاَتٌ يُقِمْنَ صُلْبَهُ، فَإِنْ كَانَ لَا مَحَالَةَ، فَثُلُثٌ لِطَعَامِهِ، وَثُلُثٌ لِشَرَابِهِ، وَثُلُثٌ لِنَفَسِهِ».
Kutoka kwa Mikidadi bin Ma'di Karibi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hajawahi kujaza mwanadamu yeyote chombo chenye shari zaidi kama tumbo, kinamtosha mwanadamu kiasi kidogo cha chakula kinachoweza kumpa nguvu, ikiwa hakuna namna, basi theluthi moja (ya tumbo lake) iwe kwa ajili ya chakula chake, na theluthi moja ya kinywaji chake, na theluthi moja kwa ajili ya pumzi yake".
Imepokelewa na Imamu Ahmad, Tirmidhiy, Nasai na Ibn MajahDarajaSahihi
Maelezo

Anatuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika msingi miongoni mwa misingi ya tiba, nayo ni kinga ambayo mtu analinda kwayo afya yake, ambayo ni kupunguza kula, bali ale kwa kiasi cha kuziba tumbo lake na kupata nguvu ya kufanya kazi zake za lazima, na hakika chombo cha shari zaidi kilichowahi kujazwa ni tumbo, na hii ni kwa sababu ya matokeo ya shibe, kama maradhi mabaya yasiyohesabika yanayokuja haraka au kwa baadaye, ya siri au ya wazi. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Ikiwa mtu hana namna zaidi ya kushiba, basi afanye kula kuwe kwa kiasi cha theluthi, na theluthi nyingine ya kinywaji, na theluthi nyingine ya pumzi ili asipate dhiki na madhara, na uvivu wa kutekeleza aliyomuwajibishia Mwenyezi Mungu juu yake katika swala la dini yake au dunia yake.

Mafunzo
  1. Kutozidisha katika kula na kunywa, na huu ni msingi unaokusanya misingi yote ya tiba, kwa kuwa katika kuzidisha kula kuna maradhi na magonjwa.
  2. Lengo la kula, ni kuhifadhi afya na nguvu ambayo ndio usalama wa maisha.
  3. Kujaza tumbo kwa chakula kuna madhara ya mwili na ya dini, amesema Omari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Tahadharini na kuvimbewa, kwani ni madhara kwa mwili na hutia uvivu wa kuswali".
  4. Kula kwa mujibu wa hukumu kuna gawanyika: 1- Wajibu: Nako ni kule kunakohifadhi uhai na kuacha kwake kunaweza kupelekea madhara. 2- Inafaa: Nako ni kule kunakozidi katika kiwango cha wajibu na wala hakuna madhara kama ataacha. 3- Inachukiza: Nako ni kule kunakohofiwa madhara. 4- Haramu: Nako ni kule kunakojulikana kuwa kuna madhara. 5- Inapendeza: Nako ni kule kunakoweza kuwa msaada wa kufanya ibada na kumtii Mwenyezi Mungu, na imekusanywa vizuri katika hadithi katika daraja tatu: Ya kwanza: Kujaza tumbo. Ya pili: Matonge kadhaa yanayoweza kumpa nguvu ya kusimama. Ya tatu: Kauli yake: "Theluthi moja iwe kwa ajili ya chakula chake na theluthi nyingine kwa ajili ya kinywaji chake na theluthi nyingine kwa ajili ya pumzi yake" Na hii yote ikiwa kama aina ya chakula ni cha halali.
  5. Hadithi hii ni kanuni miongoni mwa kanuni za tiba, kiasi ambacho hata elimu ya udaktari inazunguka katika misingi mitatu: Kuhifadhi nguvu, na kuilinda, na kuacha nafasi ya kupumua, hadithi imekusanya mambo mawili ya mwanzo katika hayo, kama ilivyokuja katika kauli yake Mtukufu: "Na kuleni na mnywe wala msifanye fujo kwani hakika Yeye hawapendi wafanyao fujo" [Al-Araf: 31].
  6. Ukamilifu wa sheria hii, kiasi ambacho imekusanya masilahi yote ya mwanadamu katika dini yake na dunia yake.
  7. Miongoni mwa elimu za sheria ni misingi ya udaktari na aina zake, kama ilivyokuja katika Asali na Habbati Saudaa.
  8. Hukumu za sheria kujawa na hekima, na kwamba zimejengeka katika kuzuia madhara na kuleta manufaa.
Marejeo

سنن الترمذي (4/ 188) (2380). سنن ابن ماجه (4/ 448) (3349). مسند أحمد (28/ 422) (17186). فتح الباري لابن حجر (9/ 528). جامع العلوم والحكم في شرح خمسين حديثا من جوامع الكلم، لابن رجب (2/ 467). التحفة الربانية في شرح الأربعين حديثًا النووية، لإسماعيل الأنصاري (ص100). فتح القوي المتين في شرح الأربعين وتتمة الخمسين، لعبد المحسن العباد (ص148).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Sikuacha baada yangu fitina yenye madhara zaidi kwa wanaume kuliko wanawake

عن أسامة بن زيد رضي الله عنهما عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «مَا تَرَكْتُ بَعْدِي فِتْنَةً أَضَرَّ عَلَى الرِّجَالِ مِنَ النِّسَاءِ».
Kutoka kwa Osama bin Zaidi -Radhi za Allah ziwe juu yao- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Sikuacha baada yangu fitina yenye madhara zaidi kwa wanaume kuliko wanawake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hakuacha baada yake majaribu na mtihani wenye madhara makubwa kwa wanaume kuliko wanawake; Mwanamke akiwa ni katika familia yake huenda mume akamfuata mwanamke katika kwenda kinyume na sheria, na akiwa ni mwanamke wa kando yaweza kuwa ni kwa sababu ya kuchanganyika naye na kukaa naye faragha, na maovu mengine yanayoweza kusababishwa na hilo.

Mafunzo
  1. Ni lazima kwa muislamu kutahadhari na fitina ya wanawake, na kuziba njia zote zinazopelekea kufitinika nao.
  2. Ni lazima kwa muumini ashikamane na Mwenyezi Mungu, na kujiweka karibu naye katika kutaka kusalimika na fitina.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 8) (5096). صحيح مسلم (4/ 2097) (2740). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (373). فتح الباري لابن حجر (9/ 138).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Msijifunze elimu kwa ajili ya kujifaharisha kuwa ni katika maulama, wala kwa kujadiliana na wasiokuwa na elimu

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رضي الله عنهما أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَا تَعَلَّمُوا الْعِلْمَ لِتُبَاهُوا بِهِ الْعُلَمَاءَ، وَلَا لِتُمَارُوا بِهِ السُّفَهَاءَ، وَلَا تَخَيَّرُوا بِهِ الْمَجَالِسَ، فَمَنْ فَعَلَ ذَلِكَ، فَالنَّارُ النَّارُ».
Imepokelewa kutoka kwa Jaabir -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Msijifunze elimu kwa ajili ya kujifaharisha kuwa ni katika maulama, wala kwa kujadiliana na wasiokuwa na elimu, wala kuonekana ni mtu bora kwenye vikao, na yeyote atakaye fanya hivyo basi anastahiki kuingia motoni."
Imepokelewa na Ibnu MaajahDarajaSahihi
Maelezo

Ametahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutafuta elimu kwa lengo la kujifaharisha kuwa naye ni katika Maulamaa, na kujitangaza kuwa mimi ni mjuzi kama nyinyi, au kwa ajili ya kujadiliana na wasiokuwa na ujuzi katika dini wenye upungufu wa maarifa, au anajifunza ili aonekane kuwa mtu bora kwenye vikao na kupewa kipaumbele kuliko mtu mwingine, Basi yeyote atakaye fanya hivyo; Bila shaka anastahiki kuchomwa katika moto kwa sababu ya kujionesha kwake na kukosa Ikhlaas katika kuitafuta elimu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.

Mafunzo
  1. Vitisho vikali vya kuingizwa motoni kwa mwenye kujifunza elimu ili ajifaharishe au ajadiliane kwa elimu yake au aonekane kuwa ni mtu bora kwenye vikao na mfano wa hayo.
  2. Umuhimu wa kuitakasa nia kwa kila mwenye kuitafuta elimu na kuifundisha.
  3. Nia ni msingi wa matendo, na kwa kupitia nia ndipo hupatikana malipo.
Marejeo

سنن ابن ماجه (1/ 170) (254)، مرشد ذوي الحجا والحاجة (2/378)، مشارق الأنوار الوهاجة ومطالع الأسرار البهاجة في شرح سنن الإمام ابن ماجه (4/ 482).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Amepigia mfano Mwenyezi Mungu wa njia iliyonyooka

عَنْ النَّوَّاسِ بْنِ سَمْعَانَ الْأَنْصَارِيِّ رضي الله عنه عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «ضَرَبَ اللهُ مَثَلًا صِرَاطًا مُسْتَقِيمًا، وَعَلَى جَنْبَتَيْ الصِّرَاطِ سُورَانِ، فِيهِمَا أَبْوَابٌ مُفَتَّحَةٌ، وَعَلَى الْأَبْوَابِ سُتُورٌ مُرْخَاةٌ، وَعَلَى بَابِ الصِّرَاطِ دَاعٍ يَقُولُ: أَيُّهَا النَّاسُ، ادْخُلُوا الصِّرَاطَ جَمِيعًا، وَلَا تَتَعَرَّجُوا، وَدَاعٍ يَدْعُو مِنْ فَوْقِ الصِّرَاطِ، فَإِذَا أَرَادَ يَفْتَحُ شَيْئًا مِنْ تِلْكَ الْأَبْوَابِ، قَالَ: وَيْحَكَ لَا تَفْتَحْهُ، فَإِنَّكَ إِنْ تَفْتَحْهُ تَلِجْهُ، وَالصِّرَاطُ الْإِسْلَامُ، وَالسُّورَانِ: حُدُودُ اللهِ، وَالْأَبْوَابُ الْمُفَتَّحَةُ: مَحَارِمُ اللهِ، وَذَلِكَ الدَّاعِي عَلَى رَأْسِ الصِّرَاطِ: كِتَابُ اللهِ، وَالدَّاعِي مِنِ فَوْقَ الصِّرَاطِ: وَاعِظُ اللهِ فِي قَلْبِ كُلِّ مُسْلِمٍ».
Imepokelewa kutoka kwa Nawwaas bin Sam'aan Al-Answaariy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kapokea kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Amepigia mfano Mwenyezi Mungu wa njia iliyonyooka ,na pambizoni mwa njia kuna kuta mbili, kuta hizo zina milango ilikuwa wazi, na kwenye milango kuna pazia isiyomuonesha mwenyekupita, na mbele ya kila mlango kuna mwenye kuita akisema: Enyi watu, ingieni nyote moja kwa moja wala msipinde kwenda kwingine, na juu ya huyu muitaji kuna muitaji mwingine akiita juu ya njia, na kila mja anapotaka kufungua kidogo milango hiyo anasema: Ole wako wacha usiufungue mlango huo, ikiwa utaufungua tu hutoweza kujizuia, na njia hapa ni Uislamu, na kuta mbili: Ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, na milango iliyofunguliwa: Ni maharamisho ya Mwenyezi Mungu, na huyo muitaji aliyopo mwanzo wa mlango ni kitabu cha Mwenyezi Mungu, na muitaji aliyepo juu: Ni Mlinganiaji wa Mwenyezi Mungu katika moyo wa kila Muislamu."
Imepokelewa na Tirmidhiy na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Ameweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Kuwa Mwenyezi Mungu alitolea mfano wa Uislamu na njia iliyonyooka pana isiyokuwa na konakona, na pambizoni mwa njia hii kuna kuta mbili zimeizunguka njia hii katika pande zake mbili, na njia hizo ni mipaka ya Mwenyezi Mungu, katikati ya hizi kuta mbili kuna milango iliyofunguliwa, na hiyo milango ni makatazo ya Mwenyezi Mungu, na katika milango hiyo kuna mapazia ambayo humzuia mwenye kupita kumuona aliye ndani, na mwanzo wa njia kuna mwenye kuita akielekeza watu na kuwaongoza na akiwaambia: Ingieni nyote moja kwa moja wala msipinde kwenda kwingine, na huyu mwenye kuita ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na juu ya njia kuna muitaji mwingine, na huyu muitaji humkemea kila mwenye kutembea katika njia hii ambaye anaelekea kutaka kufunua pazia za milango hiyo humkemea na kumwambia Ole wako usiufungue mlango huo! kwa hakika ukiufungua mlango huo utaingia na wala hutoweza kuizuia nafsi yako isiingie humo, na huyu mwenye kuita ni mlinganiaji wa Mwenyezi Mungu katika moyo wa kila Muislamu.

Mafunzo
  1. Uislamu ndiyo Dini ya kweli, na ndiyo njia iliyonyooka ambayo hutufikisha peponi.
  2. Ni wajibu kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu, na kuchunga yale aliyoyahalalisha na yale aliyoyaharamisha, na kuyapuuzia hayo kunapelekea maangamivu.
  3. Ubora wa Qur'ani tukufu, na kuhimizwa kuifanyia kazi, kwakuwa ndani yake kuna muongozo, mwanga na mafanikio.
  4. Huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na kwa namna alivyoweka kwenye nyoyo za waumini kitu ambacho kinawazuia na kuwapa mawaidha ya kuwaepusha kuingia kwenye maangamivu.
  5. Mwenyezi Mungu kwa huruma zake amewawekea waja wake kizuizi kinachowazuia kutumbukia kwenye maasi.
  6. Miongoni mwa nyenzo za kufundishia ni kupiga mifano ili kuliweka jambo karibu na kuliweka wazi.
Marejeo

سنن الترمذي (4/ 539) (2859)، مسند أحمد (29/ 181، 183) (17634)، جامع العلوم والحكم (2/161)، فيض القدير (4/253)، التنوير شرح الجامع الصغير (7/100)، الفتح الرباني لترتيب مسند الإمام أحمد بن حنبل الشيباني (1/ 83).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ikiwa utawaona wenye kufuata Aya zenye kutatiza basi hao ndiyo ambao Mwenyezi Mungu amewataja katika aya

عَنْ ‌عَائِشَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا قَالَتْ: تَلَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ هَذِهِ الْآيَةَ: {هُوَ الَّذِي أَنْزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ، وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّهُ، وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِنْ عِنْدِ رَبِّنَا وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ} [آل عمران: 7]. قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «فَإِذَا رَأَيْتِ الَّذِينَ يَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ فَأُولَئِكَ الَّذِينَ سَمَّى اللهُ، فَاحْذَرُوهُمْ».
Imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alisoma Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake Aya hii :{Yeye ndiye ambaye alikuteremshia kitabu hiki ndani yake kuna Aya muhkam -zilizo wazi- aya hizo ambazo ndiyo msingi wa kitabu hiki na zipo nyingine zinatatiza, wale ambao nyoyoni mwao kuna upotofu watafuata zile zenye kutatiza kwa kutaka kufitinisha na kutaka kujua uhakika wa maana yake, na hakuna ajuaye uhakika wa maana yake isipokuwa Mwenyezi Mungu, na wale wabobezi katika elimu wanasema tumeziamini zote zimetoka kwa Mola wetu na hawakumbuki isipokuwa wenye akili} (Al- imaraan 7) Anasema Aisha: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Ikiwa utawaona wenye kufuata Aya zenye kutatiza basi hao ndiyo ambao Mwenyezi Mungu amewataja katika aya"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alisoma aya hii: {Huwal ladhii Anzala alaikal kitaab minhu aayaatu muhkamaatun hunnaa ummul kitaab,wa ukharu mutashaabihaat,fa-ammal ladhiina fii quluubihim zaighun fayattabiuuna maatashaabaha minhu ib-tighaal fitnat wabtighaa taawiilihi,wamaa yaalamu taawilahu illa llahu warrasikhuuna fil ilmi yaquuluuna aamanna bihi kullu min in-di rabbinaa wamaa yaddhakkaru illa ulul al-baab}, Ndani ya aya hii Mwenyezi Mungu Mtukufu amefahamisha kuwa yeye ndiye aliyeteremsha Qur'ani kwa Mtume wake Qur'ani ambayo kuna aya zinazofahamika kwa uwazi, hukumu zake zinafahamika na hazitatizi, na aya hizo ni msingi wa kitabu hiki na ndiyo marejeo yake, nayo Qur'ani ndiyo marejeo inapotokea kutofautiana, na katika Qur'ani hiyo kuna aya zingine zinachukuwa maana zaidi ya moja maana zake zinawatatiza baadhi ya watu, au wanadhani kuwa kati ya aya na aya nyingine kuna mgongano, kisha akaweka wazi Mwenyezi Mungu namna watu wanavyozifanyia kazi aya hizi, basi wale ambao katika nyoyo zao kuna upotofu wa kuiwacha haki huziwacha aya zilizokuwa wazi, na wanachukuwa zile zenye kutatiza wakitaka kuibua utata na kuwatatiza watu, na kufanya hivyo wanataka kwa kutumia maana hiyo iafikiane na matamanio ya nafsi zao, ama wale ambao wamebobea kwenye elimu wanaujua utata huu, na wanazirudisha kwenye maana zilizo wazi na wanaziamini kuwa aya hizo zimetoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na haiwezekani zikapingana lakini hilo hawalikumbuki wala kupata mawaidha isipokuwa wale wenye akili iliyo salama, kisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamwambia mama wa waumini Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- kuwa ikiwa atawaona wenye kufuata aya zenye kutatiza basi hao ndio wale ambao Mwenyezi Mungu amewataja katika maneno yake aliposema: {Basi wale ambao katika nyoyo zao kuna maradhi} basi tahadhari nao na wala usiwasikilize.

Mafunzo
  1. Al-muhkam katika aya za Qur'ani: Ni zile ambazo ni nyepesi kuzifahamu maana zake zipo wazi, na zenye kutatiza ni zile zenye kuchukua zaidi ya maana moja na zinahitajia uchunguzi wa kina na ufahamu.
  2. Kuchukua tahadhari ya kutochanganyikana na watu waliopotoka, na watu wazushi na wenye kuleta mambo yenye kutatiza kwa ajili ya kuwapoteza watu na kuwatia mashaka.
  3. Katika kumalizia aya kwa maneno yake Mwenyezi Mungu Mtukufu "Na hawakumbuki isipokuwa wenye akili" Inaashiria kuwapinga wapotofu na kuwasifia waliojikita katika elimu, yaani asiyekumbuka wala kupata mawaidha, na akafuata matamanio ya nafsi yake huyo si miongoni mwa wenye kutumia akili.
  4. Kufuata mambo yenye kutatiza ni sababu ya kuupotosha moyo.
  5. Ni wajibu kuzirudisha aya ambazo maana zake zinatatiza na hazifahamiki maana zake, katika aya ambazo maana yake ni nyepesi kufahamika.
  6. Mwenyezi Mungu Mtukufu amezifanya baadhi ya aya kuwa ni nyepesi na zingine ni zenye kutatiza; Ili awajaribu watu na kuwapambanua wenye imani na watu waliopotea.
  7. Kwa kutokea aya zenye kutatiza katika Qur'ani: Ni kudhihirisha ubora wa maulamaa kuliko watu wengine, na kuifahamisha akili kuhusu mapungufu yake; ili ijisalimishe kwa muumba wake na ikubali kushindwa kwake.
  8. Ubora wa kujikita katika elimu na ulazima wa kudumu katika elimu.
  9. Na maulamaa wa tafsiri kwenye kusimama katika neno (Allah) katika maneno yake aliposema {Wamaa ya'alamu taawilahuu illa llahu warraasikhuuna fil ilmi} kuna kauli mbili, kwa yule atakayesimama katika neno (Allah), basi yanakuwa makusudio ya neno Taawiil ni ujuzi wa uhakika wa kitu kwa namna ambayo hakuna njia ya kuujua, kama vile jambo linalohusu roho na kiyama katika mambo ambayo Mwenyezi Mungu ameyaficha katika elimu yake, na wale wabobezi katika elimu wao wanaziamini na wanaegemeza uhakika wake kwa Mwenyezi Mungu, hivyo basi wanajisalimisha na wanasalimika, na mwenye kupitiliza bila ya kusimama kwenye neno( Allah) basi inakuwa maana ya neno Taawili ni tafsiri na kuweka wazi, hivyo inakuwa Mwenyezi Mungu anajua na waliobobea katika elimu vilevile wanajua, hivyo wanakuwa ni wenye kuziamini na wana zirudisha kwenye aya zilizo nyepesi.
Marejeo

صحيح البخاري (6/ 33) (4547)، صحيح مسلم (4/ 2053) (2665)، فتح الباري (8/211)، شرح النووي على مسلم (16/217)، النهاية في غريب الحديث والأثر (ص 407، 465)، فتح الودود في شرح سنن أبي داود (4/415)، تحفة الأبرار شرح مصابيح السنّة (1/129)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (41/ 559).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hupitishwa fitina katika nyoyo (kama ufumwavyo mkeka) ukindu (kijiti) kimoja kimoja

عَنْ حُذَيْفَةَ رضي الله عنه قَالَ: كُنَّا عِنْدَ عُمَرَ رضي الله عنه، فَقَالَ: أَيُّكُمْ سَمِعَ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَذْكُرُ الْفِتَنَ؟ فَقَالَ قوْمٌ: نَحْنُ سَمِعْنَاهُ، فَقَالَ: لَعَلَّكُمْ تَعْنُونَ فِتْنَةَ الرَّجُلِ فِي أَهْلِهِ وَجَارِهِ؟ قَالُوا: أَجَلْ، قَالَ: تِلْكَ تُكَفِّرُهَا الصَّلَاةُ وَالصِّيَامُ وَالصَّدَقَةُ، وَلَكِنْ أَيُّكُمْ سَمِعَ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَذْكُرُ الَّتِي تَمُوجُ مَوْجَ الْبَحْرِ؟ قَالَ حُذَيْفَةُ: فَأَسْكَتَ الْقَوْمُ، فَقُلْتُ: أَنَا، قَالَ: أَنْتَ لِلَّهِ أَبُوكَ، قَالَ حُذَيْفَةُ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «تُعْرَضُ الْفِتَنُ عَلَى الْقُلُوبِ كَالْحَصِيرِ عُودًا عُودًا، فَأَيُّ قَلْبٍ أُشْرِبَهَا نُكِتَ فِيهِ نُكْتَةٌ سَوْدَاءُ، وَأَيُّ قَلْبٍ أَنْكَرَهَا نُكِتَ فِيهِ نُكْتَةٌ بَيْضَاءُ، حَتَّى تَصِيرَ عَلَى قَلْبَيْنِ، عَلَى أَبْيَضَ مِثْلِ الصَّفَا فَلَا تَضُرُّهُ فِتْنَةٌ مَا دَامَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ، وَالْآخَرُ أَسْوَدُ مُرْبَادًّا كَالْكُوزِ، مُجَخِّيًا لَا يَعْرِفُ مَعْرُوفًا، وَلَا يُنْكِرُ مُنْكَرًا، إِلَّا مَا أُشْرِبَ مِنْ هَوَاهُ»، قَالَ حُذَيْفَةُ: وَحَدَّثْتُهُ، أَنَّ بَيْنَكَ وَبَيْنَهَا بَابًا مُغْلَقًا يُوشِكُ أَنْ يُكْسَرَ، قَالَ عُمَرُ: أَكَسْرًا لَا أَبَا لَكَ؟ فَلَوْ أَنَّهُ فُتِحَ لَعَلَّهُ كَانَ يُعَادُ، قُلْتُ: لَا بَلْ يُكْسَرُ، وَحَدَّثْتُهُ أَنَّ ذَلِكَ الْبَابَ رَجُلٌ يُقْتَلُ أَوْ يَمُوتُ حَدِيثًا لَيْسَ بِالْأَغَالِيطِ. قَالَ أَبُو خَالِدٍ: فَقُلْتُ لِسَعْدٍ: يَا أَبَا مَالِكٍ، مَا أَسْوَدُ مُرْبَادٌّ؟ قَالَ: شِدَّةُ الْبَيَاضِ فِي سَوَادٍ، قَالَ: قُلْتُ: فَمَا الْكُوزُ مُجَخِّيًا؟ قَالَ: مَنْكُوسًا.
Kutoka kwa Hudhaifa radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Siku moja tulikuwa kwa Omari radhi za Allah ziwe juu yake, akasema: Ni nani miongoni mwenu aliyemsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akieleza kuhusu fitina? Watu wakasema: Sisi tulimsikia, akasema: Huenda nyinyi mnakusudia fitina ya mtu kwa familia yake na jirani yake? Wakasema: Ndivyo, akasema: Fitina hiyo inafutwa na swala na swaumu na sadaka, lakini ni nani miongoni mwenu aliyemsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akieleza fitina ambayo inapiga kama mawimbi ya Bahari? Akasema Hudhaifa: Akawanyamazisha watu wote kwa hilo, nikasema: Mimi, akasema: Nakuapiza kwa Mwenyezi Mungu, umkose baba yako, ni wewe kweli, Hudhaifa, nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Hupitishwa fitina katika nyoyo (kama ufumwavyo mkeka) ukindu (kijiti) kimoja kimoja, moyo wowote utakaozifyonza basi hutiwa ndani yake doa jeusi, na moyo wowote unaozikataa hutiwa doa jeupe, moyo huo mpaka unakuwa katika (hadhi ya) mioyo miwili, katika weupe mfano wa jiwe jeupe, hivyo hakuna fitina yoyote inayoweza kuudhuru milele kwa muda wote mbingu na ardhi zitakapoendelea kubakia kwake, na moyo mwingine ni mweusi ti! kama chungu kilichofunikwa, haukubali jema, wala haukatai ovu, isipokuwa matamanio ulionyweshwa", Hudhaifa akasema: Na nikamsimulia kuwa hakika kati yako wewe na fitina hiyo kuna mlango uliofungwa, na hivi karibuni utavunjwa, Omari akasema: Hivi utavunjwa? umepata hasara ya kumkosa baba, na lau ungelifunguliwa basi huenda ungelirejeshwa tena, nikasema: Hapana, bali utavunjwa, na nikamsimulia kuwa mlango huo ni mtu atauawa au kufa, na ni mazungumzo ya kweli wala si maneno ya kubumba. Akasema Abuu Khalidi, nikasema kumwambia Saa'di: Ewe Abuu Maaliki nini maana ya nyeusi ti!? Akasema: Ni weupe ung'aao katika weusi, anasema, nikasema: Na nini maana ya chungu kilichofunikwa? Akasema: Kilichogeuzwa juu chini.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa kiongozi wa waumini Omari bin Khattwab radhi za Allah ziwe juu yake katika kikao chake akiwa pamoja na kundi la Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, akasema kuwaambia: Ni nani kati yenu aliyemsikia Mtume rehema na amni ziwe juu yake akieleza kuhusu fitina? Wakasema baadhi yao: Sisi tulimsikia akieleza kuhusu fitina, akasema Omari radhi za Allah ziwe juu yake: Huenda nyinyi mnakusudia fitina na mtihani wa mtu katika mambo yake maalumu; kwa mke wake na mtoto wake, kwa kuchupa mipaka katika kuwapenda, na pupa yake kwao, na kushughulishwa nao sana kuliko mambo ya kheri, au kwa uzembe wake, kwa kutotekeleza mambo ya lazima kwake kuyasimamia katika haki, na kuwaadabisha na kuwasomesha, na vile vile fitina ya mtu kwa jirani yake na mfano wake, huenda nyinyi mnakusudia hiyo? Wakasema: Ndiyo, akasema: Hiyo ni fitina inayopelekea kuihesabu nafsi, ikiwa ni pamoja na madhambi ambayo yanatarajiwa kufutwa kwa mema, kama swala na swaumu na sadaka. Lakini ni nani kati yenu aliyemsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiitaja fitina inayowakumba watu wote kwa sababu ya ukubwa wake na wingi wa kusambaa kwake, inayowavuruga watu kama yanavyovurugika mawimbi ya Bahari? Watu wote wakanyamaza: Akasema Hudhaifa bin Yamani radhi za Allah ziwe juu yake: Mimi nilimsikia, Omari radhi za Allah ziwe juu yake akafurahi, na akasema kumwambia: Umenishangaza kwa haya aliyokuja nayo mtu mfano wako!: Basi hebu sema: Hudhaifa akasema: Amesema rehema na amani ziwe juu yake: Fitina itatokea na itafungamana na mwili na upande wa moyo wa mtu kama godoro linavyonasa udongo katika mbavu za aliyelala hapo, na zitamuathiri katika moyo kwa kushikamana nazo sana, na kutoziacha fitina hizi, na kujirejea rejea kwake fitina baada ya fitina, moyo wowote utakaoingia ndani yake, na ukazipenda, na zikachanganyika nao, kama kuchanganyikana na kinywaji na kuingia ndani yake; basi litapigwa ndani ya moyo wake doa jeusi; na moyo wowote utakaozikataa, basi utapigwa ndani yake doa jeupe, mpaka nyoyo zitakuwa katika aina mbili; katika moyo mweupe kwa sababu ya kushikamana na imani kisawasawa, na kusalimika kwake na mapungufu, na kwamba fitina haijaambatana nao, na wala hazijauathiri mfano wa jiwe gumu jeupe ambalo hakuna kitu kinaweza kunasa hapo, hakuna fitina inayoweza kumdhuru mpaka mtu atakapokutana na Mwenyezi Mungu. Na moyo mwingine ni moyo uliobadilika rangi yake na kuwa mweusi kwa sababu ya fitina, ni kama birika lililolala upande, au lililogeuzwa ambalo hakuna maji yanayoweza kutulizana ndani yake, basi vile vile moyo huu hakuna kheri wala hekima yoyote inayoweza kunasa ndani yake, haukubali jema, na wala haukatai baya, isipokuwa yale aliyoyapenda, na nafsi yake kuegemea kwayo. Na akasema Hudhaifa kumwambia Omari: Hakika fitina hiyo hakuna chochote kitakachotokea katika zama za uhai wako, lakini kati yako wewe na fitina hiyo kuna mlango uliofungwa na unakaribia kuvunjwa, akasema: Yaani utavunjwa kwa nguvu? na lau kama ungelifunguliwa basi ungelirejeshewa ukafungwa tena, akasema Hudhaifa: Hapana, bali utavunjwa, na kwamba mlango huo ni mtu atauawa au atakufa. Na niliyoyaeleza ni habari za kweli na si katika habari za Mayahudi na Wakristo, na wala si jitihada za mtu mwenye mtazamo wa mbali, bali ni katika hadithi za Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Mafunzo
  1. Hatari ya fitina ya watu wote; kwa sababu ya yale yanayotokea ndani yake kama umwagwaji wa damu na kupoteza mali na kutoweka kwa amani.
  2. Fitina binafsi ikiwa inahusiana na dini basi hapa mtu kasemwa vibaya; kwa sababu ima iwe ni uzushi au maasi, na ikiwa inafungamana na mambo ya kidunia, basi huu kwake ni mtihani, na la wajibu kwake ni kuwa subira.
  3. Moyo unaathirika kwa fitina zinazopitishwa, na mwenye kuwezeshwa ni yule aliyeongozwa na Mwenyezi Mungu kudumu katika uongofu.
  4. Amesema Nawawi: Amesema Mtunzi wa kitabu Attahriiri: Maana ya hadithi: Nikuwa mtu atakapofuata matamanio yake na akafanya maasi, moyo wake huingia giza kwa kila maasi anayoyafanya, na akiendelea hivyo basi hufitinika na kuondoka nuru ya Uislamu, na moyo kuwa kama mfano wa chungu kikijifunika humwagika kilichomo, na hakiwezi kuingia kitu tena baada ya hapo.
  5. Kauli ya Omari kwa Hudhaifa: (Umkose baba yake) Maana yake: Umedhamiria kweli katika jambo hili, na kaza na ujiandae kujiandaa kwa mtu asiyekuwa na msaidizi.
  6. Ubora wa Omari radhi za Allah ziwe juu yake, na kwamba yeye ni mlango uliofungwa baina ya watu na fitina
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 128-129) (144). النهاية في غريب الحديث والأثر (606) (649) (471) (521) (340) (139). شرح النووي على مسلم (2/ 171).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hatokuwa na imani mmoja wenu mpaka yawe matamanio yake ni yenye kufuata yale niliyokujua nayo

عَنْ أَبِي مُحَمَّدٍ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ العَاصِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى يَكُونَ هَوَاهُ تَبَعًا لِمَا جِئْتُ بِهِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Muhammadi Abdallahi bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hatokuwa na imani mmoja wenu mpaka yawe matamanio yake ni yenye kufuata yale niliyokujua nayo".
Imepokelewa na katika kitabu cha Al-Hujjah kwa msururu sahihi wa wasimuliziDarajaAmesema Nawawi: Hadithi hii ni sahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwanadam hawezi kuwa muumini mwenye imani kamili ya wajibu mpaka mapenzi yake yafuate yale aliyokuja nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake miongoni mwa amri na makatazo na mengineyo, ayapende aliyoamrishwa, na ayachukie aliyokatazwa.

Mafunzo
  1. Hadithi hii ni kanuni ya kujisalimisha katika sheria na kutii.
  2. Tahadhari kwa mwanadamu kuwa yeyote mwenye kuipa kipaumbele akili au mazoea na akaitanguliza kuliko yale aliyokuja nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, basi huyu imani kwake imekanushwa.
  3. Ulazima wa kuifanya sheria kuwa ndio muamuzi katika kila kitu, kwa kauli yake: "Yale niliyokuja nayo".
  4. Nikuwa imani inaongezeka kwa kumtii Mwenyezi Mungu na inapungua kwa kumuasi.
Marejeo

الحجة على تارك المحجة لأبي الفتح نصر بن إبراهيم المقدسي، برقم (25). فتح الباري لابن حجر (13/289). جامع العلوم والحكم (3/1146). شرح النووي على مسلم (1/77).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com