Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kuyasema vibaya Maasi.

Hadithi 15

Hivi nikuelezeni madhambi makubwa?

عن أبي بكرة رضي الله عنه قال: قال النبي صلى الله عليه وسلم: «‌أَلَا ‌أُنَبِّئُكُمْ بِأَكْبَرِ الْكَبَائِرِ؟» ثَلَاثًا، قَالُوا: بَلَى يَا رَسُولَ اللهِ، قَالَ: «الْإِشْرَاكُ بِاللهِ، وَعُقُوقُ الْوَالِدَيْنِ» وَجَلَسَ وَكَانَ مُتَّكِئًا، فَقَالَ: «أَلَا وَقَوْلُ الزُّورِ»، قَالَ: فَمَا زَالَ يُكَرِّرُهَا حَتَّى قُلْنَا: لَيْتَهُ سَكَتَ.
Imepokewa kutoka kwa Abuu Bakra -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hivi nikuelezeni madhambi makubwa?" Kalisema hilo mara tatu, wakasema: Tueleze ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema: "Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu (na kitu kingine), na kuwaasi wazazi wawili" Na akakaa vizuri na alikuwa kaegemea, akasema: "Fahamuni, na kusema uongo", akasema: Akaendelea kulikariri neno hilo mpaka tukasema: Laiti angenyamaza.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anawaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Masahaba zake kuhusu madhambi makubwa, akataja haya matatu: 1- Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu: Nako ni kuielekeza aina yoyote katika aina za ibada kwa asiye Allah, na kumfanya kuwa sawa na Allah asiyekuwa Allah katika uungu wake na uumbaji na ulezi wake na majina yake na sifa zake. 2- Kuwaasi wazazi wawili: Nayo ni kila aina ya maudhi kwa wazazi wawili, sawa sawa iwe kwa kauli au kitendo, na kuacha kuwafanyia wema. 3- Kauli ya uongo ikiwemo ushahidi wa uongo: Nayo ni kila kauli ya kuzusha ya uongo, yenye lengo la kumdhalilisha yule anayekusudiwa kwa kuchukua mali yake au kumfanyia uadui katika heshima yake au mfano wa hayo. Alikariri Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- tahadhari hii ya kusema uongo ikiwa ni tahadhari juu ya ubaya wake na athari zake mbaya kwa jamii, mpaka wakasema Masahaba: Laiti angelinyamaza; Kwa sababu ya kumhurumia, na kwa kuchukia kile kinachompa kero Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.

Mafunzo
  1. Dhambi kubwa kabisa ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu; kwa sababu amelifanya kuwa dhambi kubwa la kwanza na kubwa kuliko yote, na inayotia mkazo katika hili ni kauli yake Mtukufu: "Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi pale anaposhirikishwa, na anasamehe yasiyokuwa hayo kwa amtakaye".
  2. Ukubwa wa haki ya wazazi wawili, pale alipoambatanisha haki zao na haki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  3. Madhambi yanagawanyika makubwa na madogo, na dhambi kubwa ni: Kila dhambi lenye adhabu duniani, kama kusimamishiwa sheria na laana, au ahadi ya adhabu ya Akhera, kama ahadi ya adhabu ya moto, pia madhambi makubwa yana daraja, baadhi yake ni mazito kuliko mengine katika uharamu, na madhambi madogo nayo ni yale yasiyokuwa makubwa.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 172) (2654)، (8/ 4) (5976)، (8/ 62) (6273-6274). صحيح مسلم (1/ 91) (87). عمدة الأحكام من كلام خير الأنام صلى الله عليه وسلم (ص257) (380). شرح النووي على مسلم (2/ 81). الإلمام بشرح عمدة الأحكام لإسماعيل الأنصاري (2/ 149). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام للبسام (ص703). أعلام السنة المنشورة لاعتقاد الطائفة الناجية المنصورة، لحافظ بن أحمد الحكمي (ص111).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kulikuwa na jeraha (kwa mmoja) katika wale waliokuwa kabla yenu, akakasirishwa nalo akachukua kisu akaukata mkono wake, damu ikachuruzika na wala haikukatika mpaka akafa, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kaniharakisha mja wangu yeye mwenyewe, na mimi nimemharamishia pepo

عَن الحَسَنِ قال: حَدَّثنا جُنْدَبُ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ رضي الله عنه، فِي هَذَا المَسْجِدِ، وَمَا نَسِينَا مُنْذُ حَدَّثَنَا، وَمَا نَخْشَى أَنْ يَكُونَ جُنْدُبٌ كَذَبَ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلّى الله عليه وسلم: «كَانَ فِيمَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ رَجُلٌ بِهِ جُرْحٌ، فَجَزِعَ، فَأَخَذَ سِكِّينًا فَحَزَّ بِهَا يَدَهُ، فَمَا رَقَأَ الدَّمُ حَتَّى مَاتَ، قَالَ اللَّهُ تَعَالَى: بَادَرَنِي عَبْدِي بِنَفْسِهِ، حَرَّمْتُ عَلَيْهِ الجَنَّةَ».
Kutoka kwa Hassan amesema: Alituhadithi Jundab bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake, ndani ya Msikiti huu, na hatujasahahu tangu alivyotuhadithia, na wala hatuhofii kuwa Jundab alimsemea uongo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, alisema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Kulikuwa na jeraha (kwa mmoja) katika wale waliokuwa kabla yenu, akakasirishwa nalo akachukua kisu akaukata mkono wake, damu ikachuruzika na wala haikukatika mpaka akafa, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kaniharakisha mja wangu yeye mwenyewe, na mimi nimemharamishia pepo".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kulikuwa na mtu katika wale waliokuwa kabla yetu alipatwa na jeraha, akakasirishwa nalo na wala hakuvumilia maumivu, akachukua kisu akaukata mkono wake na akakiharakisha kifo, damu haikukatika mpaka akafa, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kaniharakisha mja wangu yeye mwenyewe, basi nimemharamishia kwake pepo.

Mafunzo
  1. Fadhila za kuvumilia balaa, na kuacha kuchukia na kulalamikia maumivu, ili hilo lisipelekee katika jambo baya zaidi kuliko hilo.
  2. Kuhadithia kuhusu Umma zilizopita kwa yale ambayo yana kheri na mawaidha ndani yake.
  3. Amesema bin Hajari: Hapa kuna kusimama katika haki za Mwenyezi Mungu na rehema zake na kwa viumbe wake, kiasi ambacho amewaharamishia kujiua, na kwamba nafsi ni milki ya Mwenyezi Mungu.
  4. Uharamu wa kutumia sababu zinazopelekea katika kuia nafsi, na onyo kali katika hilo.
  5. Amesema bin Hajari: Na imeonyesha kuwa alijikata kwa ajili ya kujiua na si kwa kutaka kujitibu, ambayo inaweza kuwa dhana ya kunufaika na kitendo hicho.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 170) (3463). صحيح مسلم (1/ 107) (113). فتح الباري، لابن حجر (3/ 227). شرح النووي على مسلم (2/ 127). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص651).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Madhambi makubwa: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kuwaasi wazazi wawili, na kuuwa nafsi, na kiapo cha uongo

عن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «الْكَبَائِرُ: الْإِشْرَاكُ بِاللهِ، وَعُقُوقُ الْوَالِدَيْنِ، وَقَتْلُ النَّفْسِ، وَالْيَمِينُ الْغَمُوسُ».
Imepokewa kutoka kwa Abdillah Ibn Amri bin Aswi -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-amesema: "Madhambi makubwa: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kuwaasi wazazi wawili, na kuuwa nafsi, na kiapo cha uongo".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- madhambi makubwa, nayo ni yale aliyokemewa mfanyaji wake kwa kemeo la adhabu kali duniani au Akhera. La kwanza lake "Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu": Nalo ni kukielekeza chochote katika aina za ibada kwa asiyekuwa Allah, na kumfanya kuwa sawa na Allah asiyekuwa Allah katika yale ambayo ni maalumu kwa Allah katika uungu wake na uumbaji wake na majina yake na sifa zake. Na la pili lake "Ni kuwaasi wazazi wawili": Nalo ni kila linalopelekea kuwaudhi wazazi wawili sawa sawa iwe kauli au kitendo, na kuacha kuwatendea wema. Na la tatu lake: "Ni kuua nafsi": Bila hatia, kama kuuwa kwa dhulma na uadui. Na la nne lake "Kiapo cha uongo": Nako ni kuapia uongo huku ukijua kuwa ni uongo, umeitwa hivyo; Kwa sababu humzamisha mfanyaji wake katika madhambi au motoni.

Mafunzo
  1. Kiapo cha uongo hakina kafara; kwa ubaya wa hatari yake, bali kinatoba.
  2. Kuishia kutaja madhambi makubwa haya manne katika hadithi ni kwa sababu ya ukubwa wa dhambi zake, na si kwa kudhibiti idadi yake.
  3. Madhambi yanagawanyika makubwa na madogo, na dhambi kubwa ni: Kila dhambi lenye adhabu duniani, kama kusimamishiwa sheria na laana, au ahadi ya adhabu ya Akhera, kama ahadi ya adhabu ya moto, pia madhambi makubwa yana daraja, baadhi yake ni mazito kuliko mengine katika uharamu, na madhambi madogo nayo ni yale yasiyokuwa makubwa.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 137) (6675). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 408). رياض الصالحين للنووي (ص125) (337). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (5/ 610). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص964).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

“Mfano wa rafiki mwema na rafiki muovu ni mfano wa mbeba miski na mfua vyuma

عَنْ أَبِي مُوسَى رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّمَا مَثَلُ الْجَلِيسِ الصَّالِحِ وَالْجَلِيسِ السَّوْءِ كَحَامِلِ الْمِسْكِ وَنَافِخِ الْكِيرِ، فَحَامِلُ الْمِسْكِ: إِمَّا أَنْ يُحْذِيَكَ، وَإِمَّا أَنْ تَبْتَاعَ مِنْهُ، وَإِمَّا أَنْ تَجِدَ مِنْهُ رِيحًا طَيِّبَةً، وَنَافِخُ الْكِيرِ: إِمَّا أَنْ يُحْرِقَ ثِيَابَكَ، وَإِمَّا أَنْ تَجِدَ رِيحًا خَبِيثَةً».
Na kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: “Mfano wa rafiki mwema na rafiki muovu ni mfano wa mbeba miski na mfua vyuma. Mbeba miski: atakukaribia utapata harufu nzuri ya marashi yake, au utanunua kwake, na ama mfua vyuma: Ima atachoma nguo zako, au utasikia harufu mbaya.”
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amepiga mfano Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wa aina mbili za watu: Aina ya kwanza: Rafiki mwema anayemjulisha rafiki yake kwa Mwenyezi Mungu na yanayomridhisha, na kumsaidia katika utiifu, Mfano wake ni kama muuza miski, ima atakupa, au utanunua kwake, au utapata na kunusa harufu nzuri kutoka kwake. Aina ya pili: Rafiki na swahiba mbaya; Anayeziba njia ya Mwenyezi Mungu, na anasaidia katika kutenda maasi, na unaona wazi kwake matendo machafu, na wewe unasemwa vibaya kwa kufuatana naye na kukaa na mtu kama yeye. Mfano wake ni kama mhunzi apulizaye moto wake; ima itachoma nguo zako kutokana na cheche zake zinazoruka, au utasikia harufu mbaya kwa kukaa karibu naye.

Mafunzo
  1. Inaruhusiwa kutumia mifano ili kusogeza maana karibu kwa msikilizaji.
  2. Himizo na hamasisho kwa watu kuwa pamoja na watu watiifu na waadilifu, na kujiepusha na watu waovu na wenye maadili mabaya.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 96) (5534). صحيح مسلم (4/ 2026) (2628). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 431). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 339). شرح النووي على مسلم (16/ 178).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Yaepukeni mambo saba yenye kuangamiza

عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «اجْتَنِبُوا السَّبْعَ الْمُوبِقَاتِ»، قَالُوا: يَا رَسُولَ اللهِ وَمَا هُنَّ؟ قَالَ: «الشِّرْكُ بِاللهِ، وَالسِّحْرُ، وَقَتْلُ النَّفْسِ الَّتِي حَرَّمَ اللهُ إِلَّا بِالْحَقِّ، وَأَكْلُ الرِّبَا، وَأَكْلُ مَالِ الْيَتِيمِ، وَالتَّوَلِّي يَوْمَ الزَّحْفِ، وَقَذْفُ الْمُحْصَنَاتِ الْمُؤْمِنَاتِ الْغَافِلَاتِ».
Imepokelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Yaepukeni mambo saba yenye kuangamiza" Wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni yapi hayo? Akasema: "Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu (na kitu kingine), na uchawi, na kuua nafsi aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa haki, na kula riba, na kula mali ya yatima, na kukimbia siku ya vita, na kuwatuhumu machafu waumini wa kike waliojihifadhi wasiojua lolote (kuhusu huo uchafu)"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- umma wake kujitenga mbali na maovu saba na maasi yenye kuangamiza, na alipoulizwa ni yapi hayo? akayabainisha kuwa ni: La kwanza: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu kingine, kwa kujifanyia mshirika na mfano wake utakasifu ni wake kwa namna yoyote ile itakayokuwa, na kuielekeza aina yoyote ya ibada miongoni mwa ibada kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kaanza na ushirikina; kwa sababu ndio dhambi kubwa kuliko yote. La pili: Uchawi -Nao namna ya ufungaji mafundo na makombe na madawa na ufukishaji mioshi-, yanayoleta athari katika mwili wa mwenye kurogwa kwa kuua au kutia maradhi, au kuwatenganisha kati ya wana ndoa wawili, nayo ni kazi ya kishetani, na wengi wao hawaufikii uchawi isipokuwa kwa ushirikina na kujikurubisha kwa maruhani wachafu kwa kitu wanachokipenda. La tatu: Ni kuua nafsi aliyokataza Allah isiuliwe isipokuwa kwa kigezo cha kisheria, na hutekelezwa na hakimu. La nne: Kutumia riba kwa kula au kwa njia nyingine katika njia za kunufaika. La tano: Kufanya uadui katika mali ya mtoto mdogo aliyefiwa na baba yake naye akiwa chini ya umri wa kubalehe. La sita: Kukimbia katika vita kati ya waislamu na makafiri. La saba: Kuwatuhumu wanawake huru wenye kujizuia na machafu kwa uzinifu, na vile vile kuwatuhumu wanaume.

Mafunzo
  1. Nikuwa madhambi makubwa idadi yake siyo saba pekee, na kutajwa kwake pekee kuwa ni saba ni kwa sababu ya ukubwa wake na hatari yake.
  2. Ruhusa ya kuua nafsi ikiwa ni kwa haki kama kisasi na kuritadi na zinaa baada ya ndoa, na hii hutekelezwa na hakimu aliyewekwa kisheria.
Marejeo

صحيح البخاري (4/ 10) (2766). صحيح مسلم (1/ 92) (89). شرح صحيح البخارى لابن بطال (8/ 489). الملخص في شرح كتاب التوحيد، للشيخ صالح الفوزان (ص201).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Haitokei kuuliwa nafsi yoyote kwa dhulma isipokuwa hupata binadamu wa mwanzo fungu (la dhambi) kutoka katika damu hiyo, kwasababu yeye ndiye muanzilishi wa kwanza kuua.

عن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه مرفوعًا: «ليس مِنْ نَفْسٍ تُقْتَلُ ظُلماً إِلاَّ كَان على ابنِ آدَمَ الأَوَّل كِفْلٌ مِن دمِهَا؛ لِأَنَّه كان أوَّل مَن سَنَّ القَتْلَ».
Kutoka kwa Abdallah bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-Hadithi Marfu'u: "Haitokei kuuliwa nafsi yoyote kwa dhulma isipokuwa hupata binadamu wa mwanzo fungu (la dhambi) kutoka katika damu hiyo, kwasababu yeye ndiye muanzilishi wa kwanza kuua".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Inasimulia hadithi hii sababu ya kubebeshwa mmoja kati ya binadamu damu zinazofuatia ambazo zinazomwagwa baada yake, Inasemekana kuwa ni Qaabil alimuua ndugu yake Haabil kwasababu ya kumuhusudu, wao ndio muuliwa na muuwaji wa mwanzo katika watoto wa adamu; anabeba Qaabil fungu la madhambi ya damu ambazo zinazomwagwa baada yake; kwasababu yeye ndiye aliyeanzilisha kuuwa; kwasababu kila atakayefanya baada yake anaiga kwake.

Marejeo

تطريز رياض الصالحين، فيصل بن عبد العزيز المبارك، تحقيق: عبد العزيز بن عبد الله آل حمد، دار العاصمة للنشر والتوزيع، الرياض، الطبعة: الأولى 1423هـ، 2002م. دليل الفالحين لطرق رياض الصالحين، محمد علي بن البكري بن علان، اعتنى بها: خليل مأمون شيحا، دار المعرفة، بيروت، الطبعة: الرابعة 1425هـ. رياض الصالحين من كلام سيد المرسلين، أبو زكريا محيي الدين النووي، تحقيق ماهر الفحل، دار ابن كثير، دمشق، بيروت، الطبعة: الأولى 1428هـ. كنوز رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين برئاسة حمد بن ناصر العمار، كنوز إشبيليا، الرياض، الطبعة: الأولى 1430هـ. صحيح البخاري، محمد بن إسماعيل البخاري الجعفي، تحقيق: محمد زهير الناصر، دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم: محمد فؤاد عبد الباقي)، الطبعة: الأولى 1422هـ. صحيح مسلم، مسلم بن الحجاج القشيري النيسابوري، تحقيق محمد فؤاد عبد الباقي، دار إحياء التراث العربي، بيروت، الطبعة: 1423هـ.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi wasemaje endapo atakuja mtu anataka kuchukua mali yangu?

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: جَاءَ رَجُلٌ إِلَى رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللهِ، أَرَأَيْتَ إِنْ جَاءَ رَجُلٌ يُرِيدُ أَخْذَ مَالِي؟ قَالَ: «فَلَا تُعْطِهِ مَالَكَ» قَالَ: أَرَأَيْتَ إِنْ قَاتَلَنِي؟ قَالَ: «قَاتِلْهُ» قَالَ: أَرَأَيْتَ إِنْ قَتَلَنِي؟ قَالَ: «فَأَنْتَ شَهِيدٌ»، قَالَ: أَرَأَيْتَ إِنْ قَتَلْتُهُ؟ قَالَ: «هُوَ فِي النَّارِ».
Kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi wasemaje endapo atakuja mtu anataka kuchukua mali yangu? Akasema: "Usimpe mali yako" Akasema: Wasemaje kama akipigana nami? Akasema: "Pigana naye" Akasema: Wasemaje kama ataniuwa? Akasema: "Basi utakuwa umekufa shahidi". Akasema: Wasemaje kama nitamuuwa? Akasema: "Huyo ataingia Motoni".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alikuja mtu mmoja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wasemaje endapo atakuja mtu akataka kuchukua mali yangu? Akasema: Hutakiwi kujisalimilisha kwake na ukampatia mali yako, akasema: Wasemaje akipigana nami? Akasema: Inafaa kwako kupigana naye, akasema: Wasemaje endapo ataniuwa? Akasema: Basi wewe utakuwa shahidi, akasema: Wasemaje endapo nikimuuwa? Akasema: Basi yeye atastahiki kuadhibiwa motoni siku ya Kiyama.

Mafunzo
  1. Anasema Nawawi: Kupambana na kibaka ni wajibu bila pingamizi lolote, na katika kujitetea kwa kuuwa kuna kauli tofauti za wanachuoni katika madhehebu yetu na madhehebu wengine, na kutetea mali ni jambo linafaa na si wajibu.
  2. Hadithi ni ushahidi kuwa, elimu kwanza kabla ya matendo, kwa sababu Swahaba alimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yale yanayompasa kabla ya kufanya.
  3. Inatakiwa kwenda hatua kwa hatua katika kupambana na adui kwa mawaidha au kutaka msaada kabla ya kuanza kupigana naye, na ikiwa yeye ndio ataanza kupigana naye, basi hima yake kubwa iwe ni kumzuia na si kumpiga.
  4. Damu ya muislamu na mali yake na heshima yake ni haramu kudhuriwa.
  5. Amesema Nawawi: Tambua kuwa shahidi amegawanyika sehemu tatu; Sehemu ya kwanza ni yule aliyeuliwa katika vita na makafiri kwa sababu yoyote miongoni mwa sababu za kuuawa, huyu anahukumu ya waliokufa mashahidi katika thawabu za Akhera na katika hukumu za dini, nazo nikuwa haoshwi na wala haswaliwi, na wa pili ni shahidi katika thawabu pasina hukumu za kidunia, naye ni aliyekufa kwa maradhi ya tumbo, na aliyekufa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali, na aliyeangukiwa na jengo, na aliyeuliwa kwa kutetea mali yake, na wengineo katika wale ambao hadithi sahihi zimekuja kuwaita kuwa ni mashihidi, huyu anaoshwa na anaswaliwa na Akhera atakuwa na thawabu za waliokufa shahidi, na si lazima awe na thawabu sawa na yule wa kwanza, na wa tatu ni yule aliyechukua ngawira kwa siri, na mfano wake miongoni mwa wale ambao dalili zimekuja kuwaondoa kuitwa mashahidi, endapo watauawa katika vita na makafiri, huyu ana hukumu za mashahidi katika dunia, haoshwi, na wala haswaliwi, na wala hana thawabu zao Akhera.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 124) (140). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 449). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 936). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 389).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Umma wangu wote unasamehewa isipokuwa wenye kutangaza wazi madhambi

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «كُلُّ أُمَّتِي مُعَافًى إِلَّا المُجَاهِرِينَ، وَإِنَّ مِنَ المُجَاهَرَةِ أَنْ يَعْمَلَ الرَّجُلُ بِاللَّيْلِ عَمَلًا، ثُمَّ يُصْبِحَ وَقَدْ سَتَرَهُ اللَّهُ عَلَيْهِ، فَيَقُولَ: يَا فُلاَنُ، عَمِلْتُ البَارِحَةَ كَذَا وَكَذَا، وَقَدْ بَاتَ يَسْتُرُهُ رَبُّهُ، وَيُصْبِحُ يَكْشِفُ سِتْرَ اللَّهِ عَنْهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Umma wangu wote unasamehewa isipokuwa wenye kutangaza wazi madhambi, na hakika miongoni mwa kutangaza machafu, ni mtu kutenda dhambi usiku, kisha akaamka akiwa kasitiriwa na Mwenyezi Mungu juu ya dhambi hilo, akaanza kusema: We fulani, jana usiku mimi nilifanya kadhaa wa kadhaa, hali yakuwa alilala usiku kucha Mola wake Mlezi akimsitiri, kisha anaamka asubuhi anafunua pazia la Mwenyezi Mungu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa muislamu mtenda dhambi anatarajiwa kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu, isipokuwa mwenye kutangaza maasi kwa kutaka ufahari na jeuri, huyu hastahiki msamaha; anafanya maasi mchana, kisha anaamka hali yakuwa Mwenyezi Mungu kamsitiri, anaanza kumsimulia mwingine kuwa yeye jana alifanya maasi fulani, na hali yakuwa alilala Mola wake Mlezi akimsitiri, kisha anaamka anafunua pazia la Mwenyezi Mungu juu yake!!.

Mafunzo
  1. Ubaya wa kuweka wazi maasi baada ya kusitiriwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  2. Katika kutangaza maasi ni kusambaza machafu baina ya waumini.
  3. Mwenye kusitiriwa na Mwenyezi Mungu duniani atamsitiri pia Akhera, na hii ni katika upana wa huruma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake.
  4. Atakayepata mtihani wa maasi, anatakiwa ajifiche, na atubie kwa Mwenyezi Mungu.
  5. Ukubwa wa dhambi la kutangaza madhambi kwa wale wanaokusudia kuweka wazi maasi, na wanajikosesha wao wenyewe kusamehewa.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 20) (6069). صحيح مسلم (4/ 2291) (2990). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 15). منار القاري شرح مختصر صحيح البخاري، لحمزة قاسم (5/ 251). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 329). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 255).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
8 kati ya 15
Hadithi 15
  1. Hivi nikuelezeni madhambi makubwa?
  2. Kulikuwa na jeraha (kwa mmoja) katika wale waliokuwa kabla yenu, akakasirishwa nalo akachukua kisu akaukata mkono wake, damu ikachuruzika na wala haikukatika mpaka akafa, akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kaniharakisha mja wangu yeye mwenyewe, na mimi nimemharamishia pepo
  3. Madhambi makubwa: Ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na kuwaasi wazazi wawili, na kuuwa nafsi, na kiapo cha uongo
  4. “Mfano wa rafiki mwema na rafiki muovu ni mfano wa mbeba miski na mfua vyuma
  5. Yaepukeni mambo saba yenye kuangamiza
  6. Haitokei kuuliwa nafsi yoyote kwa dhulma isipokuwa hupata binadamu wa mwanzo fungu (la dhambi) kutoka katika damu hiyo, kwasababu yeye ndiye muanzilishi wa kwanza kuua.
  7. Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivi wasemaje endapo atakuja mtu anataka kuchukua mali yangu?
  8. Umma wangu wote unasamehewa isipokuwa wenye kutangaza wazi madhambi
  9. Pindi nilipopandishwa juu mbinguni, nilipita kwa watu wakiwa na kucha za shaba, wakizikwarua kwazo nyuso zao na vifua vyao
  10. Wakikutana waislamu wawili kwa mapanga yao, basi muuaji na muuliwaji wote motoni
  11. Watu wa aina tatu hatowasemesha Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama wala hatowatakasa na watakuwa na adhabu chungu
  12. Mambo manne yatakayekuwa kwake atakuwa mnafiki halisi, na itakayekuwa kwake sifa moja kati ya hizo, atakuwa na sifa ya unafiki mpaka aiache: Akizungumza husema uongo, na akiingia makubaliano hufanya hiyana, na akiahidi anakwenda kinyume, na akigombana huvuka mipaka
  13. Atakayejirusha kutoka juu ya mlima akajiua basi huyo atakuwa motoni akijirusha humo milele na milele
  14. Tahadharini na madhambi yenye kudharauliwa
  15. Mambo manne yatakayekuwa kwake atakuwa mnafiki halisi, na itakayekuwa kwake sifa moja kati ya hizo, atakuwa na sifa ya unafiki mpaka aiache: Akizungumza husema uongo, na akiingia makubaliano hufanya hiyana, na akiahidi anakwenda kinyume, na akigombana huvuka mipaka

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com