Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa muislamu mtenda dhambi anatarajiwa kupata msamaha wa Mwenyezi Mungu, isipokuwa mwenye kutangaza maasi kwa kutaka ufahari na jeuri, huyu hastahiki msamaha; anafanya maasi mchana, kisha anaamka hali yakuwa Mwenyezi Mungu kamsitiri, anaanza kumsimulia mwingine kuwa yeye jana alifanya maasi fulani, na hali yakuwa alilala Mola wake Mlezi akimsitiri, kisha anaamka anafunua pazia la Mwenyezi Mungu juu yake!!.
- Ubaya wa kuweka wazi maasi baada ya kusitiriwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Katika kutangaza maasi ni kusambaza machafu baina ya waumini.
- Mwenye kusitiriwa na Mwenyezi Mungu duniani atamsitiri pia Akhera, na hii ni katika upana wa huruma ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa waja wake.
- Atakayepata mtihani wa maasi, anatakiwa ajifiche, na atubie kwa Mwenyezi Mungu.
- Ukubwa wa dhambi la kutangaza madhambi kwa wale wanaokusudia kuweka wazi maasi, na wanajikosesha wao wenyewe kusamehewa.
صحيح البخاري (8/ 20) (6069). صحيح مسلم (4/ 2291) (2990). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 15). منار القاري شرح مختصر صحيح البخاري، لحمزة قاسم (5/ 251). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 329). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 255).