عَنْ أَبِي مُوسَى رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّمَا مَثَلُ الْجَلِيسِ الصَّالِحِ وَالْجَلِيسِ السَّوْءِ كَحَامِلِ الْمِسْكِ وَنَافِخِ الْكِيرِ، فَحَامِلُ الْمِسْكِ: إِمَّا أَنْ يُحْذِيَكَ، وَإِمَّا أَنْ تَبْتَاعَ مِنْهُ، وَإِمَّا أَنْ تَجِدَ مِنْهُ رِيحًا طَيِّبَةً، وَنَافِخُ الْكِيرِ: إِمَّا أَنْ يُحْرِقَ ثِيَابَكَ، وَإِمَّا أَنْ تَجِدَ رِيحًا خَبِيثَةً».
Na kutoka kwa Abuu Musa Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na amani za Allah ziwe juu yake amesema: “Mfano wa rafiki mwema na rafiki muovu ni mfano wa mbeba miski na mfua vyuma. Mbeba miski: atakukaribia utapata harufu nzuri ya marashi yake, au utanunua kwake, na ama mfua vyuma: Ima atachoma nguo zako, au utasikia harufu mbaya.”
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amepiga mfano Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wa aina mbili za watu:
Aina ya kwanza: Rafiki mwema anayemjulisha rafiki yake kwa Mwenyezi Mungu na yanayomridhisha, na kumsaidia katika utiifu, Mfano wake ni kama muuza miski, ima atakupa, au utanunua kwake, au utapata na kunusa harufu nzuri kutoka kwake.
Aina ya pili: Rafiki na swahiba mbaya; Anayeziba njia ya Mwenyezi Mungu, na anasaidia katika kutenda maasi, na unaona wazi kwake matendo machafu, na wewe unasemwa vibaya kwa kufuatana naye na kukaa na mtu kama yeye. Mfano wake ni kama mhunzi apulizaye moto wake; ima itachoma nguo zako kutokana na cheche zake zinazoruka, au utasikia harufu mbaya kwa kukaa karibu naye.
Mafunzo
- Inaruhusiwa kutumia mifano ili kusogeza maana karibu kwa msikilizaji.
- Himizo na hamasisho kwa watu kuwa pamoja na watu watiifu na waadilifu, na kujiepusha na watu waovu na wenye maadili mabaya.
Marejeo
صحيح البخاري (7/ 96) (5534).
صحيح مسلم (4/ 2026) (2628).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 431).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين (1/ 339).
شرح النووي على مسلم (16/ 178).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ مُصْعَبِ بْنِ سَعْدٍ قَالَ: رَأَى سَعْدٌ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ لَهُ فَضْلًا عَلَى مَنْ دُونَهُ، فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «هَلْ تُنْصَرُونَ وَتُرْزَقُونَ إِلَّا بِضُعَفَائِكُمْ».
Kutoka kwa Mus'abu bin Saadi amesema: Alijiona Saadi radhi za Allah ziwe juu yake kuwa yeye ana thamani kuliko aliye chini yake, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakuna msaada na riziki mnayopewa nyinyi isipokuwa ni kupitia kwa watu madhaifu wenu".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Alidhania Saadi bin Abii Waqas radhi za Allah ziwe juu yake kuwa yeye ana ubora kuliko aliye chini yake katika watu madhaifu, kwa sababu ya ushujaa wake na mfano wa hilo!. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Tambueni kuwa hamnusuriwi wala hampewi riziki isipokuwa kwa watu wenu madhaifu kwa dua zao na swala zao na utakasifu wao wa nia; kwani wao mara nyingi ndio hutakasa dua zaidi, na huwa na unyenyekevu zaidi katika ibada kwa sababu nyoyo zao ziko tupu hazifungamani na mapambo ya dunia.
Mafunzo
- Himizo la kuwa mnyenyekevu na katazo la kujiona bora kwa watu wengine.
- Amesema bin Hajari: Ikiwa mwenye nguvu anakuwa na hadhi kwa ubora wa ushujaa wake, basi mtu dhaifu anakuwa bora kwa dua yake na utakasifu wa nia yake (Ikhlas yake).
- Himizo la kutenda wema kwa mafakiri na kuwapa haki zao, kwani hilo ni katika sababu za kupata rehema ya Mwenyezi Mungu kwako na msaada wake.
Marejeo
صحيح البخاري (4/ 36) (2896).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 354).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 111).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 279).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لاَ تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يَمُرَّ الرَّجُلُ بِقَبْرِ الرَّجُلِ فَيَقُولُ: يَا لَيْتَنِي مَكَانَهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakitosimama Kiyama mpaka apite mtu juu ya kaburi la mtu aseme: Natamani ningekua nafasi yake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Kiyama hakitosimama mpaka mtu apite katika kaburi atamani laiti angelikuwa maiti mfano wake, na sababu ni kuihofia nafsi yake kwa kutoweka dini yake kwa kuzidiwa na batili na waovu, na kudhihiri kwa fitina na maasi na maovu.
Mafunzo
- Kuna ishara ya kudhihiri maasi na fitina zama za mwisho.
- Himizo la kuchukua tahadhari na kujiandaa na mauti kwa imani na matendo mema, na kujiweka mbali na mazingira ya fitina na balaa.
Marejeo
صحيح البخاري (9/ 58) (7115)، صحيح مسلم (4/ 2231) (157)، إكمال المعلم (8/451)، شرح ابن بطال (10/58)، الإفصاح عن معاني الصحاح (6/295)، البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (44/ 388).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ الزُّبَيْرِ بْنِ الْعَوَّامِ قَالَ: لَمَّا نَزَلَتْ: {ثُمَّ لَتُسْأَلُنَّ يَوْمَئِذٍ عَنِ النَّعِيمِ} [التكاثر: 8]، قَالَ الزُّبَيْرُ: يَا رَسُولَ اللهِ، وَأَيُّ النَّعِيمِ نُسْأَلُ عَنْهُ، وَإِنَّمَا هُمَا الْأَسْوَدَانِ التَّمْرُ وَالْمَاءُ؟ قَالَ: «أَمَا إِنَّهُ سَيَكُونُ».
Kutoka kwa Zubairi bin Awwam amesema: Ilipoteremka: "Kisha hakika bila shaka mtakuja kuulizwa kuhusu neema" [Takathur: 8], akasema Zubairi: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni neema zipi tutakazooulizwa juu yake, au ni hivi vyeusi viwili tende na maji (Vyakula na vinywaji kwa ujumla)? Akasema: "Hakika bila shaka zitakuwa hizo".
Imepokelewa na Tirmidhi na bin MajahDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Ilipoteremka aya: "Kisha hakika bila shaka mtaulizwa siku hiyo kuhusu neema" Yaani: Mtakuja kuulizwa kuhusu kutekeleza shukurani kwa yale aliyowaneemesha Mwenyezi Mungu juu yenu miongoni mwa neema, akasema Zubairi bin Awwam radhi za Allah ziwe juu yake: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni neema zipi tutakazoulizwa juu yake?! Ni neema mbili ambazo hazihitaji kuziomba ambazo ni tende na maji!.
Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ama hakika nyinyi mtaulizwa kuhusu neema pamoja hali hii iliyo nayo, ni hizi neema mbili kubwa katika neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Mafunzo
- Msisitizo wa kumshukuru Mwenyezi Mungu juu ya neema.
- Neema ni miongoni mwa vile ambavyo mja ataulizwa kwavyo siku ya Kiyama.
Marejeo
سنن الترمذي (5/ 375) (3356)، سنن ابن ماجه (5/ 262) (4158)، شرح سنن ابن ماجه للسيوطي (ص: 307)، تحفة الأحوذي (9/203)، مرشد ذوي الحجا والحاجة إلى سنن ابن ماجه والقول المكتفى على سنن المصطفى (25/ 251).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «بَدَأَ الْإِسْلَامُ غَرِيبًا، وَسَيَعُودُ كَمَا بَدَأَ غَرِيبًا، فَطُوبَى لِلْغُرَبَاءِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Ulianza Uislamu ukiwa ni mgeni na utarudi kuwa mgeni kama ulivyo anza, basi shangwe kwa wale wanaoonekana kuwa ni wageni".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Uislamu ulianza ukiwa kwa mtu mmoja mmoja na uchache wa watu wake, na utarejea ukiwa mgeni kwa uchache wa wenye kuutekeleza kama ulivyoanza, twawatamani, na uzuri ulioje kwa wageni, na furaha na kitulizo cha jicho kwao.
Mafunzo
- Habari kuhusu kutokea ugeni wa Uislamu baada ya kuenea kwake na umaarufu wake.
- Hapa kuna alama miongoni mwa alama za utume, kiasi kwamba ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yale yatakayotokea baada yake, na ikatokea kama alivyoeleza.
- Fadhila ya atakayehama nchi yake na familia yake; na kwamba atakuwa na Pepo.
- Wageni ni wale wanaotengemaa watu wanapoharibika, nao ni wale wanaorekebisha yale waliyoyaharibu watu.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 130) (145).
البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (4/ 142).
إكمال المعلم بفوائد مسلم (1/ 456).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com