Kutoka kwa Mus'abu bin Saadi amesema: Alijiona Saadi radhi za Allah ziwe juu yake kuwa yeye ana thamani kuliko aliye chini yake, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakuna msaada na riziki mnayopewa nyinyi isipokuwa ni kupitia kwa watu madhaifu wenu".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Alidhania Saadi bin Abii Waqas radhi za Allah ziwe juu yake kuwa yeye ana ubora kuliko aliye chini yake katika watu madhaifu, kwa sababu ya ushujaa wake na mfano wa hilo!. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Tambueni kuwa hamnusuriwi wala hampewi riziki isipokuwa kwa watu wenu madhaifu kwa dua zao na swala zao na utakasifu wao wa nia; kwani wao mara nyingi ndio hutakasa dua zaidi, na huwa na unyenyekevu zaidi katika ibada kwa sababu nyoyo zao ziko tupu hazifungamani na mapambo ya dunia.
Mafunzo
Himizo la kuwa mnyenyekevu na katazo la kujiona bora kwa watu wengine.
Amesema bin Hajari: Ikiwa mwenye nguvu anakuwa na hadhi kwa ubora wa ushujaa wake, basi mtu dhaifu anakuwa bora kwa dua yake na utakasifu wa nia yake (Ikhlas yake).
Himizo la kutenda wema kwa mafakiri na kuwapa haki zao, kwani hilo ni katika sababu za kupata rehema ya Mwenyezi Mungu kwako na msaada wake.
Marejeo
صحيح البخاري (4/ 36) (2896).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 354).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 111).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 279).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com
Hakuna msaada na riziki mnayopewa nyinyi isipokuwa ni kupitia kwa watu madhaifu wenu · Hadithi zenye maelezo · Sabīl