Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Adh-kaar za kutoka na kuingia Msikitini.

Hadithi 2

alikuwa anapoingia msikitini anasema: "Najilinda kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa uso wake mkarimu, na kwa mamlaka yake ya tangu, kutokana na shetani aliyelaaniwa

عن عبد الله بن عمرو بن العاص رضي الله عنهما: عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه كان إذا دخل المسجد قال: «أعوذ بالله العظيم، وبوجهه الكريم، وسلطانه القديم، من الشيطان الرَّجِيم»، قال: أَقَطُّ؟ قلت: نعم، قال: فإذا قال ذلك قال الشيطان: حُفِظَ منِّي سائر اليوم.
Kutoka kwa Abdallahi bin Amru bin A'swi -radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake: Kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, yakwamba yeye alikuwa anapoingia msikitini anasema: "Najilinda kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa uso wake mkarimu, na kwa mamlaka yake ya tangu, kutokana na shetani aliyelaaniwa" Akasema: Hivyo tu? Nikasema ndiyo. Akasema: Mtu anaposema hivyo shetani husema: Huyu kalindwa nami siku yake nzima.
Imepokelewa na Abu DaudDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoingia msikitini anasema: "Najilinda kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu" Yaani: Ninashikamana na kuegemea kwa Mwenyezi Mungu na sifa zake. "Na kwa uso wake Mkarimu" Yaani: Mkarim mtoaji, "Na kwa mamlaka yake) Yaani: Ushindi wake na uweza wake kwa amtakaye katika viumbe wake "Wa tangu" Yaani: Wa zamani na wa milele. "Kutokana na Shetani aliyelaaniwa" Yaani: Aliyetengwa na kufukuzwa kutoka katika rehema ya Mwenyezi Mungu, yaani: Ewe Mwenyezi Mungu nihifadhi kutokana na wasi wasi wake na upotoshaji wake na hatua zake na hatari zake, na udanganyifu wake na upotoshaji wake, kwani yeye ndiye sababu ya upotofu, na ndio mchochezi wa upotofu na ujinga, akaulizwa Abdillah bin Amri "Hivyo tu" Yaani: Je, alivyosema Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni hivyo tu? Akasema: Ndio. Atakaposema dua hii mwenye kuingia msikitini; Shetani husema: Muingiaji kaihifadhi nafsi yake dhidi yangu wakati wake wote, mchana wake na usiku wake.

Mafunzo
  1. Fadhila za kuomba kwa dua hii wakati wa kuingia msikitini, nakuwa dua hii humkinga msemaji wake kutokana na Shetani siku nzima.
  2. Tahadhari kutokana na Shetani, nakuwa humuwinda Muislamu; kwa ajili ya kumpoteza na kumshawishi.
  3. Mtu atalindwa kutokana na upotofu na udanganyifu wa Shetani kwa kiwango ambacho moyo wake unamwamini Mwenyezi Mungu na kuihudhurisha dua hii, na kuamini kwake ahadi za Mwenyezi Mungu zinazotokana nayo.
Marejeo

سنن أبي داود (1/ 349) (466). شرح سنن أبي داود، لبدر الدين العيني (2/ 374). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (2/ 627).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakapoingia mmoja wenu msikitini basi aseme: Allaahummaf-tah lii abwaaba rahmatika (Ewe Mola wangu, nifungulie milango ya rehema zako), na akitoka aseme: Allaahumma innii as-aluka min fadhlika (Ewe Mola wangu ninakuomba unipe katika fadhila zako)

عَنْ ‌أَبِي حُمَيْدٍ أَوْ عَنْ ‌أَبِي أُسَيْدٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِذَا دَخَلَ أَحَدُكُمُ الْمَسْجِدَ فَلْيَقُلِ: اللَّهُمَّ افْتَحْ لِي أَبْوَابَ رَحْمَتِكَ، وَإِذَا خَرَجَ فَلْيَقُلِ: اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ فَضْلِكَ».
Kutoka kwa Abuu Humaidi au kutoka kwa Abuu Usaidi Amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakapoingia mmoja wenu msikitini basi aseme: Allaahummaf-tah lii abwaaba rahmatika (Ewe Mola wangu, nifungulie milango ya rehema zako), na akitoka aseme: Allaahumma innii as-aluka min fadhlika (Ewe Mola wangu ninakuomba unipe katika fadhila zako)".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Ameuelekeza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- umma wake katika dua ambayo husemwa wakati wa kuingia msikitini: "Allaahummaf-tah lii abwaaba rahmatika (Ewe Mola wangu, nifungulie milango ya rehema zako), amuombe Mwenyezi Mungu Mtukufu amuandalie sababu za kupata rehema zake, na akitaka kutoka aseme: Allaahumma innii as-aluka min fadhlika (Ewe Mola wangu ninakuomba unipe katika fadhila zako), amuombe Mwenyezi Mungu Mtukufu ampe katika fadhila zake na ziada ya hisani zake miongoni mwa riziki ya halali.

Mafunzo
  1. Sunna ya dua hii wakati wa kuingia msikitini na wakati wa kutoka.
  2. Zimetengwa rehema wakati wa kuingia, na fadhila wakati wa kutoka: Kwani mwenye kuingia hushughulika na yale yanayomkurubisha kwa Allah na katika Pepo yake ikawa ni bora ataje rehema, na anapotoka hutembea katika Ardhi kwa ajili ya kutafuta fadhila za Allah miongoni mwa riziki, ikawa ni bora kwake kutaja fadhila.
  3. Dua hizi husomwa wakati wa kutaka kuingia msikitini, na wakati wa kutaka kutoka.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 494) (713)، الكاشف عن حقائق السُّنن (3/935)، فيض القدير (1/ 336)، ذخيرة العقبى (9/153).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com