Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Nyiradi za Asubuhi na Jioni.

Hadithi 6

Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeamka, na kwako tunashinda, na kwako tunakuwa hai, na kwako tutakufa, na kwako tutafufuliwa

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَنَّهُ كَانَ يَقُولُ إِذَا أَصْبَحَ: «اللهُمَّ بِكَ أَصْبَحْنَا، وَبِكَ أَمْسَيْنَا، وَبِكَ نَحْيَا، وَبِكَ نَمُوتُ، وَإِلَيْكَ النُّشُورُ» وَإِذَا أَمْسَى قَالَ: «بِكَ أَمْسَيْنَا، وَبِكَ أَصْبَحْنَا، وَبِكَ نَحْيَا، وَبِكَ نَمُوتُ، وَإِلَيْكَ النُّشُورُ» قَالَ: وَمَرَّةً أُخْرَى: «وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: Yakwamba yeye alikuwa akisema anapoamka: "Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeamka, na kwako tunashinda, na kwako tunakuwa hai, na kwako tutakufa, na kwako tutafufuliwa" Na anaposhinda jioni anasema: "Kwako tumeshinda, na kwako tumeamka, na kwako tunakuwa hai, na kwako tunakufa, na kwako tutafufuliwa" Akasema: Na mara nyingine: "Na kwako ndio marejeo".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn MajahDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Alikuwa rehema na amani ziwe juu yake anapofikiwa na asubuhi nayo ni mwanzo wa mchana pamoja na kuchomoza Alfajiri anasema: "Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeamka" tukiwa tumegubikwa na hifadhi yako na kufunikwa na neema zako, tukishughulika na kukutaja, tukitaka msaada kwa jina lako, tukienewa na taufiki yako, tukifanya harakati zenu kwa ujanja wako na nguvu zako, "na kwako tumeshinda, na kwako tunakuwa hai, na kwako tunakufa" yaani; hii ni kama lafudhi iliyotangulia isipokuwa hii imefanywa ya jioni, atasema: Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeshinda, na kwa jina lako Muhuishaji tunakuwa hai, na kwa jina lako Mfishaji tutakufa, "na kwako tutafufuliwa" na kufufuliwa baada ya kifo, na kusambaa baada ya kukusanywa, itaendelea hali yetu namna hii katika nyakati zote, na hali zingine zilizobakia, na wala sitoachana nayo wala sitoihama. Na ikimfikia jioni baada ya Lasiri atasema: "Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeshinda, na kwako tumeamka, na kwako tunakuwa hai, na kwako tutafuka, na marejeo ni kwako" na marejeo katika dunia, na mafikio katika mwisho, wewe ndiye unayenihuisha na wewe ndiye unayenifisha.

Mafunzo
  1. Inapendeza kusoma dua hii asubuhi na jioni, kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  2. Uhitaji wa mja kwa Mola wake Mlezi katika hali zake na nyakati zake zote.
  3. Kilicho bora katika kusoma Adhkari, asubuhi ni kuanzia kuchomoza kwa Alfajiri mpaka kuchomoza Jua mwanzo wa mchana, na baada ya Laasiri mpaka kabla ya kuzama, ikiwa atazisoma baada ya hapo, yaani: Asubuhi akazisoma baada ya Jua kunyanyuka itafaa, na hata akizisoma baada ya Adhuhuri itafaa pia, na akizisoma baada ya Magharibi itafaa, huo ndio wakati wa kufanya Adhkari.
  4. Mahusiano kati ya kauli yake "na kwako tutafufuliwa" na kusemwa asubuhi, kauli hii inamkumbusha kuhuishwa na kufufuliwa kukubwa pindi watapokufa watu na kufufuliwa siku ya Kiyama, huku ni kufufuliwa kupya, na siku mpya ambayo hurejeshwa roho ndani yake, na watu hutawanyika ndani yake, na wanapumua katika asubuhi hii mpya aliyoiumba Mwenyezi Mungu; ili iwe shahidi kwa mwanadam, na ili ziwe nyakati zake mida yake ni hazina ya matendo yetu.
  5. Mahusiano kati ya kauli yake "Na kwako ndio mafikio" na kusemwa jioni, ni pale watakaporejea watu katika matendo yao na kutawanyika kwa kwenda katika masilahi yao na maisha yao, wanarejea katika nyumba zao, na wanadumishwa katika raha baada yakuwa wametawanyika, inamkumbusha kurejea kwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka kwa hatima na marejeo na mafikio.
Marejeo

سنن أبي داود (7/ 404) (5068). سنن الترمذي (5/ 398) (3391). السنن الكبرى للنسائي (9/ 209) (10323). سنن ابن ماجه (5/ 35) (3868). مسند أحمد (14/ 290) (8649). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، لعبد الله البسام (7/ 576). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 458). فتح ذي الجلال والإكرام، لابن عثيمين (6/ 503). سبل السلام بشرح بلوغ المرام، لمحمد الصنعاني (2/ 714).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Bwana wa Istighfari (Dua ya kuomba msamaha)

عَنْ شَدَّادِ بْنِ أَوْسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «سَيِّدُ الِاسْتِغْفَارِ أَنْ تَقُولَ: اللَّهُمَّ أَنْتَ رَبِّي لاَ إِلَهَ إِلَّا أَنْتَ، خَلَقْتَنِي وَأَنَا عَبْدُكَ، وَأَنَا عَلَى عَهْدِكَ وَوَعْدِكَ مَا اسْتَطَعْتُ، أَعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّ مَا صَنَعْتُ، أَبُوءُ لَكَ بِنِعْمَتِكَ عَلَيَّ، وَأَبُوءُ لَكَ بِذَنْبِي فَاغْفِرْ لِي، فَإِنَّهُ لاَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا أَنْتَ» قَالَ: «وَمَنْ قَالَهَا مِنَ النَّهَارِ مُوقِنًا بِهَا، فَمَاتَ مِنْ يَوْمِهِ قَبْلَ أَنْ يُمْسِيَ، فَهُوَ مِنْ أَهْلِ الجَنَّةِ، وَمَنْ قَالَهَا مِنَ اللَّيْلِ وَهُوَ مُوقِنٌ بِهَا، فَمَاتَ قَبْلَ أَنْ يُصْبِحَ، فَهُوَ مِنْ أَهْلِ الجَنَّةِ».
Kutoka kwa Shadaad Bin Ausi Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake alisema: "Bwana wa Istighfari (Dua ya kuomba msamaha) Ni kusema: Allaahumma anta Rabbi Laa ilaaha illaa anta, khalaqtani wa anaa abduka wa ana a'laa a'hdika, wawa'dika mastatwa'tu, auudhubika min Sharri maa swana'tu, abuu ulaka bini'matika alaiyya, wa abuu ulaka bidhambi faghfirlii, fa innahuu laa yaghfirudh-dhunuuba illaa anta" Akasema: "Na atakayeisema dua hii mchana akiwa na yakini nayo, akafa katika mchana wake huo kabla hajafika jioni, basi atakuwa miongoni mwa watu wa peponi, na atakayeisema wakati wa usiku akiwa na yakini nayo, akafariki kabla hajafika asubuhi, basi huyo atakuwa miongoni mwa watu peponi".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Mtume rehema na amani ziwe juu yake anaeleza kuwa Istighfari (Kuomba msamaha) kuna matamshi mengi, nakuwa matamshi bora na makubwa zaidi ni mja kusema: "Ewe Mwenyezi Mungu wewe ndiye Mola Mlezi hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa wewe, umeniumba na mimi ni mja wako na mimi nipo juu ya ahadi yako na maonyo yako kwa kiasi niwezavyo, ninataka hifadhi kwako kutokana na shari niliyo ifanya, ninakiri kwa neema zako zilizo juu yangu, na ninakiri kwa madhambi yangu, basi nisamehe mimi, kwani hakuna afutae madhambi isipokuwa wewe. Hivyo basi mja anaanza kukiri upweke wa Mwenyezi Mungu, nakuwa Mwenyezi Mungu ndiye muumba wake na muabudiwa wake hana mshirika wake, na kuwa yeye yuko katika ahadi aliyomuahidi Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, miongoni mwa imani na utiifu kwake, kwa kadiri ya uwezo wake; kwa sababu mja kwa namna yoyote atakavyotekeleza ibada hawezi kutekeleza yote aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu, na wala hawezi kutimiza haki stahiki katika kushukuru neema, nakuwa yeye anajilinda kwa Mwenyezi Mungu, na anajikinga kwake, kwani yeye ndiye mwenye kutakwa ulinzi kutokana na shari zote alizozitengeneza mja, Nakuwa yeye anakiri na kukubali kwa hiari yake neema zake juu yake, na anairudia nafsi yake kwa kukiri na kukubali madhambi yake na maasi yake, Na baada ya kupitia kwa Mwenyezi Mungu, atamuomba Mola wake asitiri makosa yake na amkinge na dhambi zake kwa msamaha wake na fadhila zake na rehema zake, kwani hakuna awezaye kusamehe madhambi ila yeye Mtukufu. Kisha akaeleza rehema na amani ziwe juu yake kuwa dua hii ni katika dhikiri na dua za asubuhi na jioni, nakuwa atakayeisema kwa yakini na kwa kuhudhurisha moyo wake na kwa kuiamini, mwanzo wa siku yake, kwanzia kuchomoza kwa Jua mpaka kupinduka kwake, nao ni wakati wa mchana, akafa, ataingia peponi, Na atakayeisema usiku, nao ni kuanzia kuzama kwa jua mpaka kuchomoza kwa Alfajiri, akafariki kabla hajafika asubuhi, ataingia peponi.

Mafunzo
  1. Namna za kuomba msamaha zinatofautiana na baadhi yake ni bora kuliko zingine.
  2. Nakuwa ni wajibu kwa mja apupie kumuomba Mwenyezi Mungu kwa dua hii; kwani ndio bwana wa dua zote za kuomba msamaha.
Marejeo

صحيح البخاري (8/ 67) (6306). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، لعبد الله البسام (7/ 562). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 435). فتح ذي الجلال والإكرام، لابن عثيمين (6/ 486).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hakika ungesema maneno manne, mara tatu, kama ungeyapima kwa uliyo yasema toka siku ya leo yangeyazidi uzito

عَنْ جُوَيْرِيَةَ أُمِّ المؤْمنينَ رَضيَ اللهُ عنها: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خَرَجَ مِنْ عِنْدِهَا بُكْرَةً حِينَ صَلَّى الصُّبْحَ، وَهِيَ فِي مَسْجِدِهَا، ثُمَّ رَجَعَ بَعْدَ أَنْ أَضْحَى، وَهِيَ جَالِسَةٌ، فَقَالَ: «مَا زِلْتِ عَلَى الْحَالِ الَّتِي فَارَقْتُكِ عَلَيْهَا؟» قَالَتْ: نَعَمْ، قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَقَدْ قُلْتُ بَعْدَكِ أَرْبَعَ كَلِمَاتٍ، ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، لَوْ وُزِنَتْ بِمَا قُلْتِ مُنْذُ الْيَوْمِ لَوَزَنَتْهُنَّ: سُبْحَانَ اللهِ وَبِحَمْدِهِ، عَدَدَ خَلْقِهِ وَرِضَا نَفْسِهِ وَزِنَةَ عَرْشِهِ وَمِدَادَ كَلِمَاتِهِ».
Imenukuliwa kutoka kwa Juwairia mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku moja alitoka kwake asubuhi pindi alipo sali sala ya asubuhi, na yeye akiwa katika sehemu yake ya kusalia, kisha akarudi baada ya kuingia wakati wa dhuha, naye akiwa amekaa, akasema: "Bado upo kwenye hali yako niliyo kuacha nayo?" Akasema: "Ndio", Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika ungesema maneno manne, mara tatu, kama ungeyapima kwa uliyo yasema toka siku ya leo yangeyazidi uzito: Sub-haana llahi Wabihamdihi, Adada khalqihi, Waridhwaa nafsihi, Wazinata Arshihi, Wamidaada kalimaatihi" (Ametakasika Mwenyezi Mungu na sifa njema ni zake, kwa idadi ya viumbe vyake, na ridhaa ya nafsi yake, na uzito wa Arshi yake, na wino wa maneno yake)
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alitoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa mkewe mama wa waumini Juwairia radhi za Allah ziwe juu yake mwanzo wa asubuhi aliposwali swala ya Alfajiri, na Juwairia akiwa kakaa mahali aliposwalia, kisha akarejea baada ya mchana kufika kati kati wakati wa dhuha, naye akiwa bado kakaa katika mahali pake, akasema: Hivi bado uko katika hali niliyokuacha nayo? Akasema: Ndio, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hakika nimesema baada yako maneno manne, na nimeyakiriri mara tatu, lau yangelinganishwa kulingana na malipo na yale uliyoyasema kwa muda wote uliokaa hapa basi yangeliyazidi: "Ametakasika Mwenyezi Mungu" na kutakasika kwake kutokana na mapungufu, "na sifa njema ni zake" kiasi ambacho ana sifa nzuri ambazo amewaongoza kwazo, "idadi kubwa ya viumbe wake" ambazo hakuna awezaye kujua idadi yake isipokuwa Mwenyezi Mungu, "na ridhaa ya nafsi yake" kwa kiasi kinachomridhisha kutoka kwa wale aliowaridhia Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake nalo ni jambo lisiloelezeka, "na uzito wa Arshi yake" ambacho ndicho kiumbe kikubwa na kizito zaidi, "na wino wa maneno yake" na maneno ya Mwenyezi Mungu hayadhibitiki kwa idadi na wala hayamaliziki; na hii inakusanya migawanyiko yote mitatu na inazienea; kwani wino wa maneno yake Mtukufu hauna mwisho wa kiwango chake, wala sifa yake, wala idadi yake, lakini makusudio yake: Ni kupita kipimo katika wingi; kwa sababu yeye ametaja mengi mwanzoni yanayoweza kuhesabika miongoni mwa viumbe, kisha akapanda juu kwa makubwa zaidi katika hayo na akayaelezea kwa neno ridhaa ya nafsi yake, kisha uzito wa kiumbe kikubwa nacho ni Arshi; vya kwanza ni vya kuhesabika na kiwango maalumu, na vya pili ni kwa sifa na namna maalumu, na vya tatu ni kwa ukubwa na uzito.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa fadhila za maneno haya, na himizo la kuyasema.
  2. Dhikri zinazidiana ubora, ziko baadhi yake ni bora kuliko zingine.
  3. Amesema Nawawi kuhusu kauli yake "Ametakasika Mwenyezi Mungu na sifa njema ni zake kwa wino wa maneno yake": Na makusudio yake ni kupita kiasi katika wingi; kwa sababu ametaja mwanzo yanayoweza kudhitibiwa na idadi kubwa miongoni mwa idadi ya viumbe vyake, kisha uzito wa Arshi, kisha akapanda juu zaidi kwa viumbe vikubwa kuliko hivyo, na akavielezea kwa hili, yaani yale yasiyodhitiwa na idadi kama ambavyo hayahesabiki.
  4. Amesema bin Qayyim: Hakika kinaingia katika moyo wa mwenye kumtaja Mwenyezi Mungu wakati anaposema: Sub-haanallaahi wabihamdihi, adada khalqihi...mpaka mwisho wake katika kumjua kwake na kumtakasa kwake kwa kiasi hiki kilichotajwa cha idadi ni jambo kubwa kuliko kinachokita katika moyo wa msemaji, anaposema: "Sub-haanallaah" pekee.
  5. Tumeelekezwa katika maneno machache yanayokusanya maana pana, yanayobeba matamshi kidogo, na yanalipwa kwayo fadhila na thawabu kubwa.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2090) (2726). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، لعبد الله البسام (7/ 536). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (10/ 405). فتح ذي الجلال والإكرام، لابن عثيمين (6/ 471).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Sema Yeye ni Mwenyezi Mungu mmoja tu" na sura mbili za kinga unapofika nyakati za jioni na nyakati za asubuhi mara tatu, zitakutosheleza kila kitu

عَن عبدِ اللهِ بن خُبَيب رضي الله عنه أنه قال: خَرَجْنَا فِي لَيْلَةٍ مَطِيرَةٍ وَظُلْمَةٍ شَدِيدَةٍ، نَطْلُبُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؛ يُصَلِّي لَنَا، قَالَ: فَأَدْرَكْتُهُ، فَقَالَ: «قُلْ»، فَلَمْ أَقُلْ شَيْئًا، ثُمَّ قَالَ: «قُلْ»، فَلَمْ أَقُلْ شَيْئًا، قَالَ: «قُلْ»، فَقُلْتُ: مَا أَقُولُ؟ قَالَ: «{قُلْ هُوَ اللهُ أَحَدٌ} وَالْمُعَوِّذَتَيْنِ حِينَ تُمْسِي وَتُصْبِحُ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، تَكْفِيكَ مِنْ كُلِّ شَيْءٍ».
Kutoka kwa Abdillah Bin Khubaibi Radhi za Allah ziwe juu yake yakuwa yeye amesema: Tulitoka katika usiku wa mvua kubwa na giza nene, tukimtafuta Mtume rehema na amani ziwe juu yake; ili atusalishe, anasema: Nikampata, akasema: "Sema" Nikawa sikusema kitu, kisha akasema: "Sema", Nikawa sikusema kitu, akasema: "Sema" Nikasema: Niseme nini? Akasema: "Sema Yeye ni Mwenyezi Mungu mmoja tu" na sura mbili za kinga unapofika nyakati za jioni na nyakati za asubuhi mara tatu, zitakutosheleza kila kitu".
Imepokelewa na Abuu Daud, Tirmidhiy na NasaaiDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza swahaba mtukufu Abdullah Bin Khubaib radhi za Allah ziwe juu yake: Kuwa wao walitoka katika usiku wenye mvua kubwa, na giza lilikuwa nene, kwa ajili ya kumtafuta Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake; ili awasalishe, wakamkuta, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: "Sema" Yaani: Soma, akawa hakusoma kitu, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akarejea kauli yake kwake, Abdullah akasema: Nisome nini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Soma suratul Ikhlaswi (Qul-huwallaahu ahadi), na sura mbili za kinga (Qul-Audhubirabbil-falaq), na (Qul-Audhubirabbin-naas), wakati wa jioni, na wakati wa asubuhi, mara tatu tatu, zitakuhifadhi na kila shari, na zitakukinga na kila baya.

Mafunzo
  1. Sunna ya kusoma Suratul Ikhlasi na sura mbili za kinga asubuhi na jioni, nakuwa sura hizo ni kinga dhidi ya kila shari.
  2. Ubora wa kusoma suratul Ikhlasi na sura mbili za kinga.
Marejeo

سنن أبي داود (7/ 415) (5082). سنن الترمذي (5/ 535) (3575). سنن النسائي (8/ 250) (5428). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، (2/ 996). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (17/ 307). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (5/ 543).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Yeyote atakayesema: Bismillaahi lladhi laa yadhurru ma'asmihi shai un fil Ardhwi walaa fis samaai, wahuwas samiiu'l 'aliim, (Kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye hakuna kinachoweza kudhuru pamoja na jina lake kitu chochote ardhini wala mbinguni, naye ni msikivu na mjuzi) mara tatu, basi halitomfika balaa la ghafla, mpaka atakapoamka

عَنْ أَبَانَ بْنِ عُثْمَانَ قَالَ: سَمِعْتُ عُثْمَانَ ابْنِ عَفَّانَ رضي الله عنه يَقُولُ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «مَنْ قَالَ بِسْمِ اللَّهِ الَّذِي لَا يَضُرُّ مَعَ اسْمِهِ شَيْءٌ، فِي الْأَرْضِ، وَلَا فِي السَّمَاءِ، وَهُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ، ثَلَاثَ مَرَّاتٍ، لَمْ تُصِبْهُ فَجْأَةُ بَلَاءٍ، حَتَّى يُصْبِحَ، وَمَنْ قَالَهَا حِينَ يُصْبِحُ ثَلَاثُ مَرَّاتٍ، لَمْ تُصِبْهُ فَجْأَةُ بَلَاءٍ حَتَّى يُمْسِيَ»، قَالَ: فَأَصَابَ أَبَانَ بْنَ عُثْمَانَ الْفَالِجُ، فَجَعَلَ الرَّجُلُ الَّذِي سَمِعَ مِنْهُ الْحَدِيثَ يَنْظُرُ إِلَيْهِ، فَقَالَ لَهُ: مَا لَكَ تَنْظُرُ إِلَيَّ؟ فَوَاللَّهِ مَا كَذَبْتُ عَلَى عُثْمَانَ، وَلَا كَذَبَ عُثْمَانُ عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَلَكِنَّ الْيَوْمَ الَّذِي أَصَابَنِي فِيهِ مَا أَصَابَنِي غَضِبْتُ فَنَسِيتُ أَنْ أَقُولَهَا.
Kutoka kwa Abana bin Othman amesema: Nilimsikia Othman bin Affan radhi za Allah ziwe juu yake akisema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Yeyote atakayesema: Bismillaahi lladhi laa yadhurru ma'asmihi shai un fil Ardhwi walaa fis samaai, wahuwas samiiu'l 'aliim, (Kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye hakuna kinachoweza kudhuru pamoja na jina lake kitu chochote ardhini wala mbinguni, naye ni msikivu na mjuzi) mara tatu, basi halitomfika balaa la ghafla, mpaka atakapoamka, na atakayesema wakati wa asubuhi mara tatu, halitomfika balaa la ghafla mpaka atakapofika jioni" Akasema: Akapatwa na mtihani Abana bin Othman Al-Faaliji, basi yule bwana aliyesikia hadithi akawa anamtazama, akasema kumwambia: Vipi mbona unanitazama? Wallahi sijamsemea uongo Othman, wala Othman hajamsemea uongo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, lakini siku niliyofikwa na balaa, nilichukizwa na jambo fulani nikasahau kuisoma.
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Ameainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema asubuhi ya kila siku baada ya kuchomoza Alfajiri, na jioni ya kila usiku kabla ya kuzama jua mara tatu: "Bismillaah" Ninataka msaada na ninajilinda dhidi ya kila chenye kuudhi "ambaye hakidhuru" kwa kulitaja "pamoja na jina lake" yaani "chochote" vyovyote vile kitakavyokuwa kikubwa "katika ardhi" na vinavyotoka ndani yake miongoni mwa mabalaa "wala mbinguni" na kinachoshuka kutoka humo miongoni mwa mabalaa "naye ni msikivu" wa kauli zetu "mjuzi" wa hali zetu. Atakayesema wakati wa jioni halitomfika balaa la ghafla mpaka afike asubuhi, na atakayesema wakati wa asubuhi balaa halitomfika la ghafla mpaka afike jioni. Akaipatia riwaya ya hadithi ya Abana bin Othman Al-Falij; Nayo ni kudhoofika kwa baadhi ya upande wa mwili, yule bwana aliyesikia kwake hadithi akamtazama Abana kwa kustaajabu?! Abana akasema kumwambia yule bwana: Mbona wanitazama?! Wallah sijamzulia uongo Othman, wala Othman hajamzulia uongo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, lakini leo yamenifika yale aliyoyakadiria Mwenyezi Mungu kwangu kuyasema, nimepatwa na hasira nikasahau kusema maneno haya yaliyotajwa.

Mafunzo
  1. Inapendeza kuleta dhikri hii asubuhi na jioni; ili mwanadam ahifadhike kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu lisimfike balaa ghafla au madhara ya msiba au mfano wa hayo.
  2. Nguvu kubwa ya yakini kwa wema wa mwanzo kwa Mwenyezi Mungu na kuyasadikisha kwao yale aliyoyaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  3. Miongoni mwa faida za kufanywa dhikri ziwe za asubuhi na ajioni ni kuondoa hali ya kughafilika kwa muislamu na kuvuta kwake picha endelevu kuwa yeye ni mja wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  4. Kwa kadiri inavyokuwa imani ya mtajaji Mwenyezi Mungu na unyenyekevu wake na kuhudhurisha kwake moyo, pamoja na kutakasa nia na yakini ndivyo itakavyozidi kupatikana athari ya dhikri.
Marejeo

سنن أبي داود (7/ 419) (5088). سنن الترمذي (5/ 396) (3388). السنن الكبرى للنسائي (9/ 11) (9759). سنن ابن ماجه (5/ 35) (3869). مسند أحمد (1/ 498) (446). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 528). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 997). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (17/ 314). مرعاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، للمباركفوري (8/ 130). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، للقاري (4/ 1659).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayesoma aya mbili za mwisho wa suratul Baqara zitamtosheleza

عن أبي مسعود رضي الله عنه قال: قال النبي صلى الله عليه وسلم: «مَنْ قَرَأَ بِالْآيَتَيْنِ مِنْ آخِرِ سُورَةِ الْبَقَرَةِ فِي لَيْلَةٍ كَفَتَاهُ».
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayesoma aya mbili za mwisho wa suratul Baqara zitamtosheleza".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayesoma aya mbili za mwisho katika suratul-Baqara usiku, basi Mwenyezi Mungu atamtosheleza na shari na kila lenye kuchukiza, na imesemwa: Zitamtosheleza na kisimamo cha usiku, na imesemwa: Zita mtosha na nyiradi zote, na imesemwa kuwa: Ni kiwango kidogo kinachoweza kumtosheleza mtu na kusoma Qur'ani katika kisimamo cha usiku, na imesemwa kinyume na hivyo, na huenda yote yaliyotajwa yanakusanywa na tamko hilo.

Mafunzo
  1. Kumebainisha fadhila za mwisho wa suratul-Baqara, nazo ni kuanzia katika kauli yake Mtukufu: "Aamanarrasuulu..." mpaka mwisho wa sura.
  2. Mwisho wa suratul-Baqara humzuilia mabaya msomaji wake na shari na Shetani atakaposoma katika usiku.
  3. Usiku huanza kwa kuzama jua, na humalizika kwa kuchomoza Alfajiri.
Marejeo

صحيح البخاري (6/ 188) (5008-5009). صحيح مسلم (1/ 554) (807). فتح الباري بشرح صحيح البخاري، لابن حجر (9/ 56). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 240). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص593). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لملا علي القاري (4/ 1465). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخِن وغيره (2/ 757).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com