Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Adabu za kuvaa.

Hadithi 7

“Msivae hariri wala dibaji (Sufi) wala msinywe katika vyombo vya dhahabu au vya fedha, wala msile katika vyombo vilivyotengenezwa kwa dhahabu na fedha, kwani ni vyao (Makafiri) katika dunia na sisi ni vyetu Akhera

عَن عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي لَيْلَى أَنَّهُمْ كَانُوا عِنْدَ حُذَيْفَةَ، فَاسْتَسْقَى فَسَقَاهُ مَجُوسِيٌّ، فَلَمَّا وَضَعَ القَدَحَ فِي يَدِهِ رَمَاهُ بِهِ، وَقَالَ: لَوْلاَ أَنِّي نَهَيْتُهُ غَيْرَ مَرَّةٍ وَلاَ مَرَّتَيْنِ -كَأَنَّهُ يَقُولُ: لَمْ أَفْعَلْ هَذَا-، وَلَكِنِّي سَمِعْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: «لاَ تَلْبَسُوا الحَرِيرَ وَلاَ الدِّيبَاجَ، وَلاَ تَشْرَبُوا فِي آنِيَةِ الذَّهَبِ وَالفِضَّةِ، وَلاَ تَأْكُلُوا فِي صِحَافِهَا، فَإِنَّهَا لَهُمْ فِي الدُّنْيَا وَلَنَا فِي الآخِرَةِ».
Imesimuliwa kutoka kwa Abdul-Rahman bin Abi Laila, kuwa, siku moja walikuwa kwa Hudhaifa, akaomba maji, Mmajusi mmoja akampa kitu cha kunywa, alipokiweka kikombe mkononi mwake, akakitupa, na akasema: Kwani si nilishamkataza zaidi ya mara moja au mbili - kana kwamba anasema: Sikufanya hivi kwa matashi yangu - bali nilimsikia Mtume, rehema na amani ziwe juu yake akisema: “Msivae hariri wala dibaji (Sufi) wala msinywe katika vyombo vya dhahabu au vya fedha, wala msile katika vyombo vilivyotengenezwa kwa dhahabu na fedha, kwani ni vyao (Makafiri) katika dunia na sisi ni vyetu Akhera."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Mtume, Rehema na Amani zimshukie, amekataza wanaume kuvaa hariri za kila aina. Aliwakataza wanaume na wanawake kula na kunywa katika vyombo vya dhahabu na fedha. Akasema kuwa ni kwa ajili ya waumini tu Siku ya Kiyama; Kwa sababu waliviepuka katika ulimwengu huu kwa kumtii Mwenyezi Mungu, Ama makafiri wao si vyao huko akhera. Kwa sababu waliharakisha vizuri vyao katika maisha yao ya dunia kwa kuvitumia, na kuasi kwao amri ya Mwenyezi Mungu.

Mafunzo
  1. Katazo kwa wanaume la kuvaa hariri na dibaji, na kuwatishia vikali wale wenye kuvaa.
  2. Inafaa kwa wanawake kuvaa hariri na nguo iliyotengenezwa kwa hariri
  3. Uharamu wa kula na kunywa katika sahani za dhahabu na fedha na vyombo vyake, kwa wanaume na wanawake.
  4. Hudhaifa, Mwenyezi Mungu amuwie radhi, alikuwa mkali katika kukemea kwake, na akaeleza hayo kwa kusema kwamba alimkataza zaidi ya mara moja kutumia vyombo vya dhahabu na fedha, lakini hakuacha.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 77) (5426). صحيح مسلم (3/ 1638) (2067). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، عبد الله البسام (ص729).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayevaa hariri duniani hatoivaa Akhera

عَنْ عُمَرَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ لَبِسَ الحَرِيرَ فِي الدُّنْيَا لَمْ يَلْبَسْهُ فِي الآخِرَةِ».
Imepokelewa kutoka kwa Omari radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayevaa hariri duniani hatoivaa Akhera"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwanaume yeyote atakayevaa hariri duniani hatovaa Akhera endapo hatotubia, na hii ni adhabu kwake.

Mafunzo
  1. Makusudio ya hariri ni hariri halisi ya asili, ama hariri ya bandia ya viwandani haihusiki hapa katika hadithi.
  2. Katazo la kuvaa hariri kwa wanaume.
  3. Katazo la kuvaa hariri linahusu kuivaa na kuitandika.
  4. Wanaume wanaruhusiwa kutumia hariri katika nguo ila isizidi kiwango cha vidole viwili mpaka vinne, itakayofanywa kama mchoro au urembo wa nguo.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 150) (5834). صحيح مسلم (3/ 1641) (2069). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (4/ 207).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Mtakapo vaa, na mtakapo tawadha, basi anzeni na kuliani kwenu

عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعًا: «إِذَا لَبِسْتُم، وَإِذَا تَوَضَّأتُم، فَابْدَأُوا بَأَيَامِنُكُم».
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Mtakapo vaa, na mtakapo tawadha, basi anzeni na kuliani kwenu".
Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Imetilia mkazo hadithi ya Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake swala la kuanza na kulia katika mambo mazuri, ikapokelewa kuwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Mtakapo vaa" Yaani mkitaka kuvaa. "Na mtakapo tawadha" Yaani mkitaka kufanya. "Anzeni na kuliani kwenu" ni wingi wa kulia nacho ni kinyume cha kushoto, aingize upande wa kulia wa kanzu, kabla ya kushoto na atangulize kulia katika mikono yake na miguu yake katika udhu, kisha tambua kuwa katika viungo vya udhu vipo ambavyo si sunna kuanza na kulia, navyo ni masikio mawili na viganja viwili na mashavu mawili, bali husafishwa vyote kwa wakati mmoja, ikiwa litakuwa gumu hilo kama ilivyo kwa aliyekatwa mkono na mfano wake atatanguliza kulia.

Marejeo

بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي، ط1، دار ابن الجوزي، الدمام، 1415هـ. تطريز رياض الصالحين، للشيخ فيصل المبارك، ط1، تحقيق: عبد العزيز بن عبد الله آل حمد، دار العاصمة، الرياض، 1423هـ. جامع الترمذي، تحقيق وتعليق: أحمد محمد شاكر وآخرون، ط2، شركة مكتبة ومطبعة مصطفى البابي الحلبي ، مصر، 1395هـ. دليل الفالحين لطرق رياض الصالحين لمحمد علي بن محمد بن علان، ط4، اعتنى بها: خليل مأمون شيحا، دار المعرفة، بيروت، 1425هـ. رياض الصالحين للنووي، ط1، تحقيق: ماهر ياسين الفحل، دار ابن كثير، دمشق، بيروت، 1428هـ. رياض الصالحين، ط4، تحقيق: عصام هادي، وزارة الأوقاف والشؤون الإسلامية القطرية، دار الريان، بيروت، 1428هـ. سنن أبي داود ،تحقيق: محمد محيي الدين عبد الحميد، المكتبة العصرية، بيروت. سنن ابن ماجه، تحقيق: محمد فؤاد عبد الباقي، دار إحياء الكتب العربية، فيصل عيسى البابي الحلبي. الشرح الممتع على زاد المستقنع، لمحمد بن صالح بن محمد العثيمين، ط1، دار ابن الجوزي، 1422 - 1428هـ. كنوز رياض الصالحين، مجموعة من الباحثين برئاسة حمد بن ناصر العمار، ط1، كنوز إشبيليا، الرياض، 1430هـ. مسند الإمام أحمد بن حنبل، تحقيق: شعيب الأرنؤوط و عادل مرشد، وآخرون، تحت إشراف: د عبد الله بن عبد المحسن التركي، ط1، مؤسسة الرسالة، 1421هـ. مشكاة المصابيح للتبريزي، تحقيق: محمد ناصر الدين الألباني، ط3، المكتب الإسلامي، بيروت، 1985م. المنهاج شرح صحيح مسلم بن الحجاج، للنووي، ط2، دار إحياء التراث العربي - بيروت، 1392هـ. شرح رياض الصالحين، للشيخ ابن عثيمين، دار الوطن للنشر، الرياض، 1426هـ. نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين، ط14، مؤسسة الرسالة، 1407هـ.

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kikoi cha muislamu kifikie nusu ya muundi, na wala hakuna tabu wala hakuna ubaya kikiwa kati yake na kati ya fundo mbili za miguu, kitakachokuwa chini ya fundo mbili basi hicho ni motoni, na atakayeburuza kikoi chake kwa kiburi hatomtazama Mwenyezi Mungu

عَنْ أبي سَعيدٍ الخُدريَّ رضي الله عنه قال: قال رسولُ الله صلَّى الله عليه وسلم ِ: «إزْرَةُ المُسْلمِ إلى نصفِ السَّاق، وَلَا حَرَجَ -أو لا جُنَاحَ- فيما بينَهُ وبينَ الكعبينِ، وما كان أسفلَ منَ الكعبين فهو في النار، مَن جرَّ إزارَهُ بطرًا لم يَنْظُرِ اللهُ إليه».
Imepokelewa kutoka kwa Saidi Al-Khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Kikoi cha muislamu kifikie nusu ya muundi, na wala hakuna tabu wala hakuna ubaya kikiwa kati yake na kati ya fundo mbili za miguu, kitakachokuwa chini ya fundo mbili basi hicho ni motoni, na atakayeburuza kikoi chake kwa kiburi hatomtazama Mwenyezi Mungu".
Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwanaume muislamu katika kikoi chake, nacho ni kila kinachositiri nusu ya chini kwa wanaume, kwa hali tatu: Ya kwanza: Inayopendeza iwe kati kati ya muundi. Ya pili: Inayojuzu pasina karaha ni ile inayokuwa chini ya kongo mbili; nayo ni mifupa miwili iliyotokeza katika maungio ya muundi na mguu. Ya tatu: Iliyoharamishwa, nayo ni ile inayokuwa chini ya kongo mbili, na inahofiwa kwake kupatwa na adhabu ya moto, na ikiwa ni kwa kiburi na kwa kufurahia na ujeuri, Mwenyezi Mungu hatomtazama.

Mafunzo
  1. Sifa hii na ahadi hii ya adhabu ni maalumu kwa wanaume, ama wanawake, wanaondolewa katika hilo; kwa sababu wao wameamrishwa kusitiri mwili wao wote.
  2. Kila kinachositiri nusu ya chini kwa wanaume huitwa kikoi; kama suruali, na nguo na vinginevyo, na vyote hivyo vinaingia katika hukumu ya kisheria iliyotajwa katika hadithi.
Marejeo

سنن أبي داود (6/ 191) (4093). سنن ابن ماجه (4/ 583) (3573). مسند أحمد (17/ 52) (11010). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 637). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 95). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (10/ 582). المعجم الوسيط، (1/ 16).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hamtazami Mwenyezi Mungu mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi

عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لاَ يَنْظُرُ اللَّهُ إِلَى مَنْ جَرَّ ثَوْبَهُ خُيَلاَءَ».
Na imepokelewa kutoka kwa bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake - amesema: "Hamtazami Mwenyezi Mungu mwenye kuburuza nguo yake kwa kiburi".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuburuza nguo au kikoi chini ya kongo mbili kwa kiburi na kujiona, nakuwa mwenye kufanya hivyo atastahiki ahadi ya adhabu kali yakuwa Mwenyezi Mungu hatomtazama siku ya Kiyama mtazamo wa huruma.

Mafunzo
  1. Nguo inakusanya kila kinachositiri chini ya mwili, kuanzia suruali na nguo na kikoi na vinginevyo.
  2. Katazo la kupitiliza nguo mpaka chini ni maalumu kwa wanaume pekee, amesema Nawawi: Na wamekubaliana wanachuoni juu ya kufaa kuburuza nguo kwa wanawake, na imesihi kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwapa idhini ya kuburuza nguo zao kwa kiasi cha dhiraa moja.
  3. Amesema bin Bazi: Kupitiliza nguo kumekatazwa na ni haramu kwa mujibu wa ujumla wa hadithi, na ama adhabu, zinatofautiana, na wala si lazima zote ziwe sawa, kwa sababu aliyekusudia kujifaharisha hawezi kuwa sawa na ambaye hajakusudia.
  4. Amesema bin Bazi: Mwanamke ni uchi hakuna tatizo kwake kushusha nguo kwa kiasi cha nchi tano, ikiwa haitamtosha basi atashusha kiasi cha dhiraa (futi) kuanzia katika kongo mbili.
  5. Amesema Kadhi: Wamesema wanachuoni: Na kwa ujumla inachukiza kila kilichozidi juu ya haja na mazoea katika nguo, katika urefu na upana, na Allah ndiye Mjuzi zaidi.
  6. Amesema Nawawi: Kiasi kinachopendeza katika sehemu inayoshuka katika kanzu na kikoi ni nusu ya miundi, na hakuna ubaya kama kitakuwa kati yake na kongo mbili, na kitakachoshuka zaidi ya hapo ni sababu ya kuingia motoni, inayopendeza ni nusu ya miundi, na inayofaa pasina karaha ni chini yake mpaka katika kongo mbili, kitakachoshuka chini ya kongo mbili hicho kimekatazwa.
  7. Amesema bin Uthaimiin katika kauli yake: "Mwenyezi Mungu hatomtazama" Yaani mtazamo wa huruma na upole, na si makusudio yake: Kutazama kwa ujumla; kwa sababu Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na Kutukuka hakifichikani kwake kitu chochote, na wala hakitoweki machoni mwake chochote, lakini makusudio yake ni mtazamo wa huruma na upole.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 141) (5783). صحيح مسلم (3/ 1651) (2085). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 283). فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (6/ 268). توضيح الأحكام من بلوغ المرام، للبسام (7/ 313). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 87). فتاوى اللجنة الدائمة - المجموعة الأولى- (17/ 97).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Asiangalie mwanaume katika uchi wa mwanaume mwenzie, wala mwanamke kutazama uchi wa mwanamke mwenzie

عَن أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَا يَنْظُرُ الرَّجُلُ إِلَى عَوْرَةِ الرَّجُلِ، وَلَا الْمَرْأَةُ إِلَى عَوْرَةِ الْمَرْأَةِ، وَلَا يُفْضِي الرَّجُلُ إِلَى الرَّجُلِ فِي ثَوْبٍ وَاحِدٍ، وَلَا تُفْضِي الْمَرْأَةُ إِلَى الْمَرْأَةِ فِي الثَّوْبِ الْوَاحِدِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Asiangalie mwanaume katika uchi wa mwanaume mwenzie, wala mwanamke kutazama uchi wa mwanamke mwenzie, na wala asijifunike mwanaume na mwanaume mwenzie shuka moja, na wala mwanamke asijifunike na mwanamke mwenzie shuka moja".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwanaume kutazama uchi wa mwanaume mwenzie, au mwanamke kutazama uchi wa mwanamke mwenzie. Uchi: Ni kila kinachoonewa aibu kinapodhihiri, na uchi wa mwanaume ni kati ya kitovu chake na magoti yake, Na mwanamke mwili wake wote ni uchi kwa mwanamke asiye mume wake au ndugu wa damu, na upande wa wanawake kwa ndugu zao wa damu, anaweza kuonyesha viungo ambavyo kwa desturi ya kawaida huonekana wakati wa kufanya kazi zake za nyumbani. Na amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kukaa faragha mwanaume na mwanaume mwenzake ndani ya nguo moja, au ndani ya kifuniko kimoja wakiwa uchi, na mwanamke kukaa faragha na mwanamke mwenzie ndani ya nguo moja au ndani ya kifuniko kimoja wakiwa uchi; kwa sababu kitendo hicho huenda kikapelekea kila mmoja kugusa uchi wa mwenzie, na kuugusa ni haramu ni kama kuuangalia, bali hilo ni haramu zaidi; kwa sababu linapelekea katika uovu mkubwa.

Mafunzo
  1. Katazo la kutazama uchi, isipokuwa mume na mke wake.
  2. Hima ya Uislamu juu kuisafisha jamii, na kufunga njia zinazopelekea katika machafu.
  3. Inaruhusiwa kuangalia uchi kukiwa na haja ya kufanya hivyo, kama matibabu na mfano wake, na isiwe kwa matamanio.
  4. Muislamu ameamrishwa kusitiri uchi wake na kuinamisha macho yake kutotazama uchi wa mwenzie.
  5. Kumetajwa pekee wanaume kuwatazama wanaume wenzao na wanawake kuwatazama wanawake wenzao; kwa sababu ndio kishawishi kikubwa katika kutazama na kufunua uchi.
Marejeo

صحيح مسلم (1/ 266) (338). نزهة المتقين، مجموعة من الباحثين (2/ 1118). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (19/ 288). بهجة الناظرين، لسليم الهلالي (3/ 146). إكمال المعلم بفوائد مسلم، لعياض بن عياض (2/ 186). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (6/ 363).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Vaeni katika nguo zenu nguo nyeupe, kwani hizo ni katika nguo zenu bora, na wavisheni kwazo maiti wenu

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضيَ اللهُ عنهُما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «البَسُوا مِنْ ثِيَابِكُمُ البَيَاضَ، فَإِنَّهَا مِنْ خَيْرِ ثِيَابِكُمْ، وَكَفِّنُوا فِيهَا مَوْتَاكُمْ».
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Vaeni katika nguo zenu nguo nyeupe, kwani hizo ni katika nguo zenu bora, na wavisheni kwazo maiti wenu".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Ibn MajahDarajaSahihi
Maelezo

Anawaelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake wanaume kuvaa nguo zenye rangi nyeupe na kuwavisha maiti pia; kwani ni katika nguo bora.

Mafunzo
  1. Sunna ya kuvaa nguo nyeupe, na inafaa pia kuvaa rangi nyingine tofauti na hiyo.
  2. Sunna ya kuwavisha maiti nguo nyeupe.
  3. Amesema Shaukani: Na hadithi inaonyesha sheria ya kuvaa nguo nyeupe na kuwavisha nazo maiti pia; kwakuwa ni safi zaidi na ni nzuri zaidi, ama kuwa kwake ni nzuri hili liko wazi, na ama kuwa kwake ni safi ni kwa sababu kitu chochote hata kikwa kidogo kikidondokea juu yake huonekana, ndio maana inapendekezwa.
Marejeo

سنن أبي داود (6/ 27) (3878). سنن الترمذي (2/ 311) (994). سنن ابن ماجه (2/ 453) (1472). ذخيرة العقبى في شرح المجتبى (19/ 16).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com