عَنْ عُمَرَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ لَبِسَ الحَرِيرَ فِي الدُّنْيَا لَمْ يَلْبَسْهُ فِي الآخِرَةِ».
Imepokelewa kutoka kwa Omari radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Atakayevaa hariri duniani hatoivaa Akhera"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwanaume yeyote atakayevaa hariri duniani hatovaa Akhera endapo hatotubia, na hii ni adhabu kwake.
Mafunzo
- Makusudio ya hariri ni hariri halisi ya asili, ama hariri ya bandia ya viwandani haihusiki hapa katika hadithi.
- Katazo la kuvaa hariri kwa wanaume.
- Katazo la kuvaa hariri linahusu kuivaa na kuitandika.
- Wanaume wanaruhusiwa kutumia hariri katika nguo ila isizidi kiwango cha vidole viwili mpaka vinne, itakayofanywa kama mchoro au urembo wa nguo.
Marejeo
صحيح البخاري (7/ 150) (5834). صحيح مسلم (3/ 1641) (2069). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (4/ 207).