عن عبد الله بنِ عمر رضي الله عنهما أن عمرَ بْن الخطاب رضي الله عنه قال: ((يا رسول الله، أّيَرقُدُ أَحَدُنا وهو جُنُب؟ قال: نعم، إِذَا تَوَضَّأ أَحَدُكُم فَليَرقُد)).
Kutoka kwa Abdillahi bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Yakwamba Omar bin Khattwab -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Alisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Je anaweza kulala mmoja wetu akiwa na janaba? Akasema: "Ndiyo, atakapotawadha mmoja wenu basi na alale"
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Alimuuliza Omar bin Khattwab -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ikiwa mmoja wao atapatwa na janaba mwanzoni mwa usiku, kwa kumuingilia mke wake hata kama hakumwaga au akajiotea, Je alale nayeye akiwa na janaba? Akawaruhusu -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa hilo, kwa kupunguza hadathi (uchafu) huu mkubwa kwa udhu wa kisheria; na hapo haina tatizo mtu kulala na janaba.
Marejeo
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، عبد الله بن عبد الرحمن البسام، تحقيق: محمد صبحي حلاق، مكتبة الصحابة، الإمارات، مكتبة التابعين، القاهرة، الطبعة: العاشرة 1426هـ.
تنبيه الأفهام شرح عمدة الأحكام، محمد بن صالح العثيمين، مكتبة الصحابة، الإمارات، الطبعة: الأولى 1426هـ.
الإلمام بشرح عمدة الأحكام، إسماعيل بن محمد الأنصاري، دار الفكر، دمشق، الطبعة: الأولى 1381هـ.
صحيح البخاري، محمد بن إسماعيل البخاري الجعفي، تحقيق: محمد زهير الناصر، دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم: محمد فؤاد عبد الباقي)، الطبعة: الأولى 1422هـ.
صحيح مسلم، مسلم بن الحجاج القشيري النيسابوري، تحقيق محمد فؤاد عبد الباقي، دار إحياء التراث العربي، بيروت، الطبعة: 1423هـ.
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِذَا تَوَضَّأَ أَحَدُكُمْ فَلْيَجْعَلْ فِي أَنْفِهِ ثُمَّ لِيَنْثُرْ، وَمَنِ اسْتَجْمَرَ فَلْيُوتِرْ، وَإِذَا اسْتَيْقَظَ أَحَدُكُمْ مِنْ نَوْمِهِ فَلْيَغْسِلْ يَدَهُ قَبْلَ أَنْ يُدْخِلَهَا فِي وَضُوئِهِ، فَإِنَّ أَحَدَكُمْ لاَ يَدْرِي أَيْنَ بَاتَتْ يَدُهُ».
ولفظ مسلم: «إِذَا اسْتَيْقَظَ أَحَدُكُمْ مِنْ نَوْمِهِ فَلَا يَغْمِسْ يَدَهُ فِي الْإِنَاءِ حَتَّى يَغْسِلَهَا ثَلَاثًا، فَإِنَّهُ لَا يَدْرِي أَيْنَ بَاتَتْ يَدُهُ».
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Atakapotawadha mmoja wenu basi na aweke maji puani mwake kisha ayapenge, na atakayestanji kwa mawe basi afanye yawe witiri, na atakapo amka mmoja wenu toka usingizini basi na aoshe mikono yake kabla ya kuingiza ndani ya chombo chake, kwani mmoja wenu hajui ni wapi ulilala mkono wake". Na lafudhi ya Muslim: "Atakapoamka mmoja wenu kutoka usingizini kwake basi asizamishe mkono wake ndani ya chombo mpaka auoshe mara tatu, kwani hajui ni wapi ulilala mkono wake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baadhi ya hukumu za twahara, miongoni mwake: Ya kwanza: Nikuwa mwenye kutawadha ni lazima aingize maji puani mwake kwa kuyavuta kwa pumzi, kisha ayatoe kwa pumzi pia. Ya pili: Nikuwa atakayetaka kusafisha udhia uliomtoka na kuuondoa pasina kutumia maji kama kwa jiwe na mfano wake, basi kusafisha kwake kuwe kwa idadi ya mamoja (witiri) kwa uchache tatu na kuendelea yatakayoweza kutakatisha kilichotoka na kusafisha mahali. Ya tatu: Kuwa atakayeamka kutoka katika usingizi wa usiku asiingize kiganja chake ndani ya chombo ili atawadhe mpaka akioshe mara tatu nje ya chombo, kwani hajui ni mahali gani ulilala mkono wake, hauwezi kuaminika na kutokuwa na najisi, na huenda shetani aliuchezea na akaubebesha vitu vyenye kumdhuru mwanadamu au vyenye kuharibu maji.
Mafunzo
- Ni wajibu kupandisha maji puani wakati wa udhu, nako ni: Kuingiza maji puani kwa njia ya pumzi, na pia ni wajibu kuyapenga, nako ni: Kuyatoa maji puani kwa njia ya pumzi.
- Inapendeza kupenga kwa witiri.
- Ni sheria kuosha mikono miwili baada ya kutoka usingizini mara tatu.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 43) (162).
صحيح مسلم (1/ 233) (278).
تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص19).
الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (1/ 11).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ حُذَيْفَةَ بْنِ اليَمَانِ رَضيَ اللهُ عنه: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ إِذَا أَرَادَ أَنْ يَنَامَ وَضَعَ يَدَهُ تَحْتَ رَأْسِهِ، ثُمَّ قَالَ: «اللَّهُمَّ قِنِي عَذَابَكَ يَوْمَ تَجْمَعُ أَوْ تَبْعَثُ عِبَادَكَ».
Kutoka kwa Hudheifa bin Yamaani -radhi za Allah ziwe juu yake-: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anapotaka kulala anaweka mkono wake chini ya kichwa chake, kisha anasema: "Ewe Mwenyezi Mungu nikinge na adhabu yako siku utakapowakusanya au kuwafufua waja wako".
Imepokelewa Imamu TirmidhiyDarajaSahihi
Maelezo
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapochukua malazi yake kwa ajili ya kulala, anauchegemea mkono wake wa kulia na anauwekea shavu lake la kulia, akasema: "Ewe Mwenyezi Mungu" Mola wangu Mlezi "Nikinge" na unihifadhi kutokana na "adhabu yako" na mateso yako "siku utakapowakusanya au kuwafufua waja wako" katika siku ya hesabu, siku ya Kiyama.
Mafunzo
- Fadhila za dua hii yenye baraka, na sunna ya kudumu nayo kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
- Sunna ya kulalia upande wa kulia.
- Amesema Assanadi: Kauli yake "Ewe Mwenyezi Mungu nikinge na adhabu yako" Inaonyesha kuwa inampasa mwenye akili aufanye usingizi kuwa nyenzo ya kukumbuka kifo na kufufuliwa kunakofuata baada yake.
- Kinga dhidi ya adhabu ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama inakuwa kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake, kwa kumuwezesha mja kufanya matendo mema na msamaha wa Mwenyezi Mungu kwa madhambi yake.
- Unyenyekevu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Mola wake Mlezi na Mmiliki wake Mtukufu.
- Kumethibitishwa kukusanywa na kurejea, na kwamba watu watarejea kwa Mola wao Mlezi ili awahesabu juu ya matendo yao, atakayekuta kheri basi na amshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, na atakayekuta kinyume na hivyo basi asimlaumu yeyote isipokuwa nafsi yake, bali haya ni matendo ya waja anawakusanyia Mwenyezi Mungu kwao.
- Pupa ya Maswahaba radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao katika kubainisha hali za Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kulala kwake.
- Kauli yake: "Aliweka mkono wake wa kulia chini ya shavu lake" nayo ni katika kawaida yake rehema na amani ziwe juu yake kuanzia kulia katika kila kitu isipokuwa yale yaliyokuwa kinyume chake.
- Kulalia upande wa kulia hurahisisha kuzinduka, kwa sababu moyo huwa hautulii katika hali hiyo, na huustarehesha moyo; kwa sababu huwa uko upande wa kushoto, endapo mja atalala kwa upande wa kushoto ataudhuru moyo kwa sababu ya viungo kuuelemea.
Marejeo
سنن الترمذي (5/ 404) (3398).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 533).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (17/ 335).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1001).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ إِذَا أَوَى إِلَى فِرَاشِهِ كُلَّ لَيْلَةٍ جَمَعَ كَفَّيْهِ، ثُمَّ نَفَثَ فِيهِمَا فَقَرَأَ فِيهِمَا: {قُلْ هُوَ اللهُ أَحَدٌ}، وَ{قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ الْفَلَقِ}، وَ{قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ}، ثُمَّ يَمْسَحُ بِهِمَا مَا اسْتَطَاعَ مِنْ جَسَدِهِ، يَبْدَأُ بِهِمَا عَلَى رَأْسِهِ وَوَجْهِهِ وَمَا أَقْبَلَ مِنْ جَسَدِهِ، يَفْعَلُ ذَلِكَ ثَلَاثَ مَرَّاتٍ.
Imepokelewa kutoka kwa Aisha -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa anapolala kitandani kwake wakati wa kila usiku alikuwa akikusanya viganja vyake, kisha akivipuliza na kuvisomea : {Qul-huwallahu Ahad}, na {Qul-A uudhu birabbil falaq} na (Qul-Auudhu birabbi naas } Kisha hujipaka kwa viganja hivyo sehemu awezayo katika mwili wake, anaanza kupaka kichwa chake na uso wake na sehemu ya mbele ya mwili wake, anafanya hivyo mara tatu.
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Ilikuwa katika miongozo yake Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- pindi anapopanda kitandani kwake kwa ajili ya kulala, ni kukusanya viganja vyake na kuviinua juu kama anavyofanya mwenye kuomba-na huvipuliza viganja hivyo kwa mdomo wake upulizaji wa taratibu pamoja na kutemea matemate kidogo na anasoma Sura tatu {Qul-huwallahu Ahadu} na {Qul-audhu birabbil falaq} na {Qul-auudhu birabbi naas} Kisha hupaka kwa kutumia viganja vyake sehemu anayoweza katika mwili wake; Kwa kuanzia kichwa chake na uso wake na sehemu ya mbele katika mwili wake, na hurudia kitendo hicho mara tatu.
Mafunzo
- Ni sunna kusoma suratul Ikhlaas na Muawidhataini (Sura mbili za kinga) kabla ya kulala na kupuliza kwa sura hizo, na kupakaa sehemu aiwezayo katika mwili wake.
Marejeo
صحيح البخاري (6/ 190) (5017)، (7/ 133) (5748)، الكاشف عن حقائق السُّنن (5/1651)، عمدة القاري شرح صحيح البخاري (20/ 35)، التوضيح لشرح الجامع الصحيح ( 24/ 91)، النهاية في غريب الحديث والأثر (ص 929)، شرح سنن أبي داود لابن رسلان (19/268).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com