Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Ewe Mwenyezi Mungu nikinge na adhabu yako siku utakapowakusanya au kuwafufua waja wako

عَنْ حُذَيْفَةَ بْنِ اليَمَانِ رَضيَ اللهُ عنه: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ إِذَا أَرَادَ أَنْ يَنَامَ وَضَعَ يَدَهُ تَحْتَ رَأْسِهِ، ثُمَّ قَالَ: «اللَّهُمَّ قِنِي عَذَابَكَ يَوْمَ تَجْمَعُ أَوْ تَبْعَثُ عِبَادَكَ».
Kutoka kwa Hudheifa bin Yamaani -radhi za Allah ziwe juu yake-: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anapotaka kulala anaweka mkono wake chini ya kichwa chake, kisha anasema: "Ewe Mwenyezi Mungu nikinge na adhabu yako siku utakapowakusanya au kuwafufua waja wako".
Imepokelewa Imamu TirmidhiyDarajaSahihi
Maelezo

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapochukua malazi yake kwa ajili ya kulala, anauchegemea mkono wake wa kulia na anauwekea shavu lake la kulia, akasema: "Ewe Mwenyezi Mungu" Mola wangu Mlezi "Nikinge" na unihifadhi kutokana na "adhabu yako" na mateso yako "siku utakapowakusanya au kuwafufua waja wako" katika siku ya hesabu, siku ya Kiyama.

Mafunzo
  1. Fadhila za dua hii yenye baraka, na sunna ya kudumu nayo kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  2. Sunna ya kulalia upande wa kulia.
  3. Amesema Assanadi: Kauli yake "Ewe Mwenyezi Mungu nikinge na adhabu yako" Inaonyesha kuwa inampasa mwenye akili aufanye usingizi kuwa nyenzo ya kukumbuka kifo na kufufuliwa kunakofuata baada yake.
  4. Kinga dhidi ya adhabu ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama inakuwa kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake, kwa kumuwezesha mja kufanya matendo mema na msamaha wa Mwenyezi Mungu kwa madhambi yake.
  5. Unyenyekevu wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Mola wake Mlezi na Mmiliki wake Mtukufu.
  6. Kumethibitishwa kukusanywa na kurejea, na kwamba watu watarejea kwa Mola wao Mlezi ili awahesabu juu ya matendo yao, atakayekuta kheri basi na amshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu, na atakayekuta kinyume na hivyo basi asimlaumu yeyote isipokuwa nafsi yake, bali haya ni matendo ya waja anawakusanyia Mwenyezi Mungu kwao.
  7. Pupa ya Maswahaba radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao katika kubainisha hali za Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kulala kwake.
  8. Kauli yake: "Aliweka mkono wake wa kulia chini ya shavu lake" nayo ni katika kawaida yake rehema na amani ziwe juu yake kuanzia kulia katika kila kitu isipokuwa yale yaliyokuwa kinyume chake.
  9. Kulalia upande wa kulia hurahisisha kuzinduka, kwa sababu moyo huwa hautulii katika hali hiyo, na huustarehesha moyo; kwa sababu huwa uko upande wa kushoto, endapo mja atalala kwa upande wa kushoto ataudhuru moyo kwa sababu ya viungo kuuelemea.
Marejeo

سنن الترمذي (5/ 404) (3398). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 533). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (17/ 335). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 1001).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Adabu za kulala na Kuamka.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com