عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «السَّاعِي عَلَى الأَرْمَلَةِ وَالمِسْكِينِ، كَالْمُجَاهِدِ فِي سَبِيلِ اللَّهِ، أَوِ القَائِمِ اللَّيْلَ الصَّائِمِ النَّهَارَ».
Kutoka kwa Abuu Huraira amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Mwenye kwenda upesi kuwasaidia wajane na maskini ni kama mwenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, au mwenye kusimama usiku na kufunga mchana"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwenye kusimamia masilahi ya mwanamke aliyefiwa na mumewe na ikawa hakuna yeyote mwenye kusimamia mambo yake, na masikini muhitaji, na akawapa matumizi akitaraji malipo mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi mtu huyu katika malipo ni kama mpigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na ni kama mwenye kusimama katika swala ya tahajudi asiyechoka, na mfungaji asiyefungua.
Mafunzo
- Himizo la kusaidizana na kuhurumiana na kutatua haja za watu madhaifu.
- Ibada inakusanya kila amali njema, na miongoni mwa ibada ni kwenda haraka kuwasaidia wajane na masikini.
- Amesema Bin Hubaira: Na makusudio yake hapa nikuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu humkusanyia thawabu za mfungaji na msimamaji usiku kwa ajili ya ibada na mpigana Jihadi kwa mpigo mmoja; na hii ni kwa sababu amesimama na mjane nafasi ya mume wake..., na akasimama upande wa masikini aliyeshindwa kujimudu mwenyewe, akatoa hiki kilichozidi katika matumizi yake, na akatoa sadaka kwa kuikandamiza nafsi yake, ndio maana manufaa yake yakawa sawa na swaumu na kisimamo cha usiku na Jihadi.
Marejeo
صحيح البخاري (7/ 62) (5353).
صحيح مسلم (4/ 2286) (2982).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم بن عيد الهلالي (1/ 351).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل بن عبد العزيز المبارك (ص198).
رياض الصالحين (ص107) (265).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 99).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (275).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ ثَوْبَانَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَفْضَلُ دِينَارٍ يُنْفِقُهُ الرَّجُلُ، دِينَارٌ يُنْفِقُهُ عَلَى عِيَالِهِ، وَدِينَارٌ يُنْفِقُهُ الرَّجُلُ عَلَى دَابَّتِهِ فِي سَبِيلِ اللهِ، وَدِينَارٌ يُنْفِقُهُ عَلَى أَصْحَابِهِ فِي سَبِيلِ اللهِ» قَالَ أَبُو قِلَابَةَ: وَبَدَأَ بِالْعِيَالِ، ثُمَّ قَالَ أَبُو قِلَابَةَ: وَأَيُّ رَجُلٍ أَعْظَمُ أَجْرًا مِنْ رَجُلٍ يُنْفِقُ عَلَى عِيَالٍ صِغَارٍ، يُعِفُّهُمْ أَوْ يَنْفَعُهُمُ اللهُ بِهِ وَيُغْنِيهِمْ.
Kutoka kwa Thauban -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Allah- rehema na amani za Allah ziwe juu yake: "Dinari bora anayoitoa mtu: ni Dinari anayoitoa kwa familia yake, na dinari anayoitoa mtu kwa mnyama wake katika njia ya Mwenyezi Mungu, na dinari anayoitoa kwa watu wake katika njia ya Mwenyezi Mungu" Amesema Abuu Qilaba: Na ameanza na familia, kisha akasema Abuu Qilaba: Na ni mtu gani mwenye malipo bora kuliko yule anayetoa kwa familia yake wakiwa wadogo, akawazuia na machafu au akawanufaisha Mwenyezi Mungu kupitia hicho na akawatosheleza.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Alieleza Mtume rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, aina za matumizi, na akazipanga pale panapokuwa na namna nyingi za kutoa matumizi kulingana na kile ambacho ni wajibu zaidi kwako, hivyo alianza na muhimu zaidi na kisha muhimu zaidi. Akaeleza kuwa mali yenye malipo mengi ni ile anayoitoa muislamu kwa wale anaolazimika kuwahudumia; kwanzia mkewe na watoto, kisha kutoa katika kipando kilichoandaliwa kwa ajili vita katika njia ya Mwenyezi Mungu, kisha kuwahudumia jamaa zake na rafiki zake wanapokuwa Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu.
Mafunzo
- Mpangilio wa matumizi katika ubora ni kwa namna ulivyotajwa, lizingatiwe hilo panapokuwa na majukumu mengi.
- Kumebainishwa umuhimu wa kuanza na familia katika kutoa matumizi, na ndiko kuna fadhila nyingi kuliko kutoa sehemu zingine.
- Kuhudumia Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ni katika kutoa kukubwa, kama kuandaa vifaa na watu kwa ajili ya Jihadi.
- Inasemekana kuwa: Makusudio ya njia ya Mwenyezi Mungu ni kila jambo la ibada, mfano kama Hija.
Marejeo
صحيح مسلم (2/ 691) (994).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (5/ 315).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 156).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 291).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 374).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنهُ أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِذَا تَوَضَّأَ الْعَبْدُ الْمُسْلِمُ -أَوِ الْمُؤْمِنُ- فَغَسَلَ وَجْهَهُ خَرَجَ مِنْ وَجْهِهِ كُلُّ خَطِيئَةٍ نَظَرَ إِلَيْهَا بِعَيْنَيْهِ مَعَ الْمَاءِ -أَوْ مَعَ آخِرِ قَطْرِ الْمَاءِ-، فَإِذَا غَسَلَ يَدَيْهِ خَرَجَ مِنْ يَدَيْهِ كُلُّ خَطِيئَةٍ كَانَ بَطَشَتْهَا يَدَاهُ مَعَ الْمَاءِ -أَوْ مَعَ آخِرِ قَطْرِ الْمَاءِ-، فَإِذَا غَسَلَ رِجْلَيْهِ خَرَجَتْ كُلُّ خَطِيئَةٍ مَشَتْهَا رِجْلَاهُ مَعَ الْمَاءِ -أَوْ مَعَ آخِرِ قَطْرِ الْمَاءِ- حَتَّى يَخْرُجَ نَقِيًّا مِنَ الذُّنُوبِ».
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Pindi mja muislamu au muumini atakapotawadha akaosha uso wake, madhambi yake yote yanayotokana na kuangalia yanaondoka na tone la maji au tone la mwisho usoni mwake, akiosha mikono yake yanaondoka madhambi yote yatokanayo na mikono pamoja na tone la mwisho, akiosha miguu yake madhambi yote yatokanayo na kutembea yanaondoka na tone la mwisho, mpaka muislamu anabaki msafi hana madhambi".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakapotawadha muislamu au muumini akaosha uso wake wakati wa udhu, yanatoka katika uso wake makosa yote madogo madogo aliyoyatazama kwa macho yake pamoja na maji ya yanayodondoka baada ya kuosha, au pamoja na tone la mwisho la maji, akiosha mikono yake yanatoka katika mikono yake makosa yote madogo madogo iliyoyachuma mikono yake au pamoja na tone la mwisho la maji, na akiosha miguu yake yanatoka makosa yake yote madogo madogo iliyotembea kuyafuata miguu yake, mpaka atoke akiwa kasafishika na madhambi madogo madogo kwa kumalizika kwa udhu.
Mafunzo
- Fadhila za kuhifadhi udhu, nakuwa unafuta madhambi.
- Miongoni mwa muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kuwahimiza watu katika utiifu na ibada, na kutaja malipo na thawabu zake.
- Kila kiungo miogoni mwa viungo vya mwanadamu huingia katika baadhi ya madhambi, na ndio maana madhambi hukifuata kila kiungo kilichoyafanya, na hutoka na kila kiungo kilichotubia kwayo.
- Udhu una usafi wa wazi, na unakuwa pale vinapooshwa viungo vya udhu, na usafi usioonekana; na unakuwa kutokana na madhambi yaliyotokea kupitia viungo.
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 215) (244).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (3/ 108).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (2/ 181).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 208).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 157).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا تَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ حَتَّى تُؤْمِنُوا، وَلَا تُؤْمِنُوا حَتَّى تَحَابُّوا، أَوَلَا أَدُلُّكُمْ عَلَى شَيْءٍ إِذَا فَعَلْتُمُوهُ تَحَابَبْتُمْ؟ أَفْشُوا السَّلَامَ بَيْنَكُمْ».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -sala na amani ziwe juu yake-: "Hamtoingia peponi mpaka muamini, na hamtoamini mpaka mpendane, je nisikufahamisheni juu ya jambo ambalo mkilifanya mtapendana? toleaneni salamu kwa wingi kati yenu".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume Rehema na amani ziwe juu yake yakuwa hatoingia peponi ila muumini, na wala haikamiliki imani na wala haitengemai hali ya jamii ya kiislamu mpaka wapendane baina yao. Kisha akaelekeza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake katika jambo muhimu zaidi ambalo litaleta mapenzi kwa wote, nalo ni waislamu kutoleana salam baina yao, aliyoifanya Mwenyezi Mungu kuwa ni salam kwa waja wake.
Mafunzo
- Kuingia peponi hakui ila kwa imani.
- Katika ukamilifu wa imani ni muislamu kumpendelea muislamu mwenzake yale anayoyapenda yeye.
- Ni sunna kutoa salam na kuisambaza kwa waislamu; kwa sababu kuisambaza ni kusambaza mapenzi na amani baina ya watu.
- Salam haitolewi ila kwa muislamu; kwa kauli yake Rehema na amani ziwe juu yake: "Baina yenu".
- Kutoa salam kunaondoa chuki na kuhamana na vifundo.
- Umuhimu wa mapenzi kati ya waislamu nakuwa hilo ni katika ukamilifu wa imani.
- Imekuja katika hadithi nyingine kuwa namna ya salam kamili ni: "As-salaam alaikum warahmatullahi wabarakaatuh", na inatosha: "Assalaam alaikum".
Marejeo
صحيح مسلم (1/ 74) (54).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 129).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل المبارك (ص515).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 394).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 661).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ خُرَيْمِ بْنِ فَاتِكٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «الْأَعْمَالُ سِتَّةٌ، وَالنَّاسُ أَرْبَعَةٌ، فَمُوجِبَتَانِ، وَمِثْلٌ بِمِثْلٍ، وَحَسَنَةٌ بِعَشْرِ أَمْثَالِهَا، وَحَسَنَةٌ بِسَبْعِ مِائَةٍ، فَأَمَّا الْمُوجِبَتَانِ: فَمَنْ مَاتَ لَا يُشْرِكُ بِاللهِ شَيْئًا دَخَلَ الْجَنَّةَ، وَمَنْ مَاتَ يُشْرِكُ بِاللهِ شَيْئًا دَخَلَ النَّارَ، وَأَمَّا مِثْلٌ بِمِثْلٍ: فَمَنْ هَمَّ بِحَسَنَةٍ حَتَّى يَشْعُرَهَا قَلْبُهُ، وَيَعْلَمَهَا اللهُ مِنْهُ كُتِبَتْ لَهُ حَسَنَةً، وَمَنْ عَمِلَ سَيِّئَةً، كُتِبَتْ عَلَيْهِ سَيِّئَةً، وَمَنْ عَمِلَ حَسَنَةً فَبِعَشْرِ أَمْثَالِهَا، وَمَنْ أَنْفَقَ نَفَقَةً فِي سَبِيلِ اللهِ فَحَسَنَةٌ بِسَبْعِ مِائَةٍ، وَأَمَّا النَّاسُ، فَمُوَسَّعٌ عَلَيْهِ فِي الدُّنْيَا مَقْتُورٌ عَلَيْهِ فِي الْآخِرَةِ، وَمَقْتُورٌ عَلَيْهِ فِي الدُّنْيَا مُوَسَّعٌ عَلَيْهِ فِي الْآخِرَةِ، وَمَقْتُورٌ عَلَيْهِ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، وَمُوَسَّعٌ عَلَيْهِ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ».
Imepokelewa kutoka kwa Khuraimu Bin Faatik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Matendo yapo ya aina sita na watu wapo wako aina nne, basi kuna watu wa aina mbili wanaostahiki malipo, na malipo yao huwa sawa na matendo yao, na jema moja hulipwa kwa kumi mfano wake, na jema moja huzidishwa mpaka kufikia mema mia saba, Basi wawili wenye kustahiki malipo ni: Yeyote atakaye kufa hali yakuwa hajamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia Peponi, na atakaye kufa hali ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote basi ataingia Motoni, na ama yule ambaye atalipwa kwa namna alivyokusudia ni yeyote atakaye kusudia kufanya jambo jema mpaka moyo wake ukahisi kuwa umetenda na Mwenyezi Mungu akajua kutenda kwake huko basi mtu huyo ataandikiwa jema moja, na atakaye fanya kosa ataandikiwa kosa moja, na atakaye fanya jema moja basi hulipwa kwa kumi mfano wake, na mwenye kutoa chochote katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi atalipwa kwa kila kimoja kwa mara mia saba, ama watu walivyogawanyika kuna miongoni mwao waliokunjuliwa mambo yao hapa Duniani na wakawa na maisha duni huko Akhera, na kuna wenye maisha Duni hapa duniani na wakakunjuliwa maisha yao huko Akhera, na kuna wenye maisha duni hapa duniani na pia Akhera, na wakakunjuliwa maisha yao hapa duniani na kesho Akhera."
Imepokelewa na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Alieleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa matendo yapo aina sita, na watu wamegawanyika katika makundi manne, nayo ni:
Kundi la kwanza: Yeyote atakaye kufa na hakumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote anastahiki kuingia peponi.
Kundi la pili: Yeyote atakaye kufa hali yakuwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu kingine anastahiki kuingia motoni na atakaa humo milele.
Na matendo hayo mawili ndiyo haki mbili za msingi.
Kundi la tatu: Kukusudia kufanya wema, basi yeyote atakaye kusudia kufanya jema na akawa mkweli katika makusudio yake mpaka akahisi kweye moyo wake kuwa hili ndilo kusudio langu, kisha likamtokea jambo la kumzuia asifanye alichokikusudia katika wema huu, basi huandikiwa thawabu za wema kamili.
Kundi la nne: Kufanya tendo baya; Yeyote atakaye fanya tendo baya basi huandikiwa kosa moja.
Na matendo hayo mawili: Ndiyo hulipwa sawa sawa bila ya kuzidisha.
Kundi la Tano: Jema moja hulipwa kwa kumi mfano wake, na malipo hayo ni kwa mwenye kukusudia kufanya wema na akaufanya wema huo, basi huandikiwa mema kumi.
kundi la sita: Jema moja hulipwa sawa na mema mia saba, na malipo hayo ni kwa mwenye kutoa kitu kimoja katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi hulipwa kwa kitu hiki kimoja kwa mema mia saba, na haya ni kutokana na fadhila za Mwenyezi Mungu aliyetakasika na Kutukuka, na ukarimu wake kwa waja wake.
Ama aina Nne ya watu ni hawa:
Aina ya kwanza: Ni mtu ambaye amekunjuliwa mambo yake hapa Duniani kwa upande wa riziki, ananeemeka humo na hupata akitakacho, lakini ni mwenye dhiki na tabu kubwa Akhera na mwisho wake ni kuingia motoni, na huyo ni tajiri wa kikafiri.
Aina ya pili: Ni mtu mwenye dhiki hapa Duniani upande wa riziki, lakini amekunjuliwa huko Akhera, na mwisho wake ni kuingia Motoni, na huyo ni muumini fakiri.
Aina ya tatu: Ni mtu mwenye dhiki hapa Duniani na Akhera, naye ni kafiri fukara.
Aina ya nne: Ni mtu aliyekunjuliwa mambo yake hapa Duniani na Akhera, naye ni muumini tajiri.
Mafunzo
- Ukubwa wa fadhila za Mwenyezi Mungu kwa waja wake na kuwazidishia mambo mema.
- Uadilifu wa Mwenyezi Mungu na ukarimu wake, pale alipo amiliana nasi kwenye makosa kwa uadilifu, hivyo basi akafanya malipo ya kosa moja ni moja hivyo hivyo.
- Ukubwa wa dhambi ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu, katika hilo kunapelekea kuharamishiwa kuingia peponi.
- Kumewekwa wazi utukufu na ubora wa kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu.
- Ongozeko la thawabu za kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu, linaanzia ziada ya mia saba; Kwa sababu kutoa kunasaidia kuliinua neno la Mwenyezi Mungu.
- Kumewekwa wazi aina za watu na tofauti zao.
- Mwenyezi Mungu humkunjulia muumini na asiyekuwa mumini hapa Duniani, na wala hamkunjulii Akhera isipokuwa muumini tu.
Marejeo
مسند أحمد (31/ 196) (18900)، (31/ 384)، الفتح الرباني لترتيب مسند أحمد بن حنبل الشيباني (19/198).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com