Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Mwenye kwenda upesi kuwasaidia wajane na maskini ni kama mwenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, au mwenye kusimama usiku na kufunga mchana

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «السَّاعِي عَلَى الأَرْمَلَةِ وَالمِسْكِينِ، كَالْمُجَاهِدِ فِي سَبِيلِ اللَّهِ، أَوِ القَائِمِ اللَّيْلَ الصَّائِمِ النَّهَارَ».
Kutoka kwa Abuu Huraira amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Mwenye kwenda upesi kuwasaidia wajane na maskini ni kama mwenye kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu, au mwenye kusimama usiku na kufunga mchana"
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwenye kusimamia masilahi ya mwanamke aliyefiwa na mumewe na ikawa hakuna yeyote mwenye kusimamia mambo yake, na masikini muhitaji, na akawapa matumizi akitaraji malipo mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi mtu huyu katika malipo ni kama mpigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na ni kama mwenye kusimama katika swala ya tahajudi asiyechoka, na mfungaji asiyefungua.

Mafunzo
  1. Himizo la kusaidizana na kuhurumiana na kutatua haja za watu madhaifu.
  2. Ibada inakusanya kila amali njema, na miongoni mwa ibada ni kwenda haraka kuwasaidia wajane na masikini.
  3. Amesema Bin Hubaira: Na makusudio yake hapa nikuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu humkusanyia thawabu za mfungaji na msimamaji usiku kwa ajili ya ibada na mpigana Jihadi kwa mpigo mmoja; na hii ni kwa sababu amesimama na mjane nafasi ya mume wake..., na akasimama upande wa masikini aliyeshindwa kujimudu mwenyewe, akatoa hiki kilichozidi katika matumizi yake, na akatoa sadaka kwa kuikandamiza nafsi yake, ndio maana manufaa yake yakawa sawa na swaumu na kisimamo cha usiku na Jihadi.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 62) (5353). صحيح مسلم (4/ 2286) (2982). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم بن عيد الهلالي (1/ 351). تطريز رياض الصالحين، لفيصل بن عبد العزيز المبارك (ص198). رياض الصالحين (ص107) (265). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 99). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (275).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
fadhila za matendo ya viungo.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com