Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Vinywaji vilivyoharamishwa.

Hadithi 4

kila kilevi ni haramu, na atakayekunywa pombe duniani na akafa akiwa mlevi kupindukia na hakutubia, hatoinywa huko akhera

عن ابن عمر رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «كل مُسْكِرٍ خَمْرٌ، وكل مُسْكِرٍ حرام، ومن شرِب الخمر في الدنيا فمات وهو يُدْمِنُهَا لَمْ يَتُبْ، لَمْ يَشْرَبْهَا في الآخرة».
kutoka kwa bin Omar -Radhi za Allah ziwe juu yao- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- "kila kilevi ni haramu, na atakayekunywa pombe duniani na akafa akiwa mlevi kupindukia na hakutubia, hatoinywa huko akhera"
Imepokelewa na Muslim, vile vile Bukhari ikiwa na ibara ya mwisho ndani ya kitabu chakeDarajaSahihi
Maelezo

Amebainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kila kinachoondosha akili na kuiondoa hicho ni pombe yenye kulewesha, sawa iwe ni kunywa, au kula, au kuvuta kwa pumzi au vinginevyo, na kuwa kila kinacholevya na kuondoa akili Mwenyezi Mungu Mtukufu amekiharamisha na amekataza, kiwe kidogo au kingi, Na kuwa kila mwenye kunywa aina yoyote ya vileo, na akaendelea kuvinywa, wala hakutubia mpaka akafa; Anastahiki adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kumnyima kuinywa Peponi.

Mafunzo
  1. Sababu ya kuharamishwa pombe ni kilevi, hivyo, kila chenye kulevya kiwe kwa aina yoyote ile ni haramu.
  2. Mwenyezi Mungu Mtukufu ameharamisha pombe; kwakuwa imekusanya madhara na maovu makubwa.
  3. Kunywa pombe peponi ni katika ukamilifu wa ladha na utimilifu wa neema.
  4. Ambaye hakuizuia nafsi yake na unywaji pombe duniani Mwenyezi Mungu atamharamishia kuinywa peponi, kwani malipo huendana na matendo.
  5. Hili ni himizo la kufanya haraka kutubia dhidi ya madhambi kabla ya kifo.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 104) (5575). صحيح مسلم (3/ 1587) (2003). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (8/ 519). فتح ذي الجلال والاكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (5/ 418). توضِيحُ الأحكَامِ مِن بُلوُغ المَرَام، للبسام (6/ 307). معالم السنن، وهو شرح سنن أبي داود، للخطابي (4/ 264). الفتح الرباني لترتيب مسند الإمام أحمد بن حنبل الشيباني، للساعاتي (16/ 116). فيض القدير شرح الجامع الصغير، للمناوي (5/ 30). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (6/ 2382).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Tambueni kuwa pombe imekwisha haramishwa

عَنْ أَنَسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: كُنْتُ سَاقِيَ القَوْمِ فِي مَنْزِلِ أَبِي طَلْحَةَ، وَكَانَ خَمْرُهُمْ يَوْمَئِذٍ الفَضِيخَ، فَأَمَرَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مُنَادِيًا يُنَادِي: أَلاَ إِنَّ الخَمْرَ قَدْ حُرِّمَتْ، قَالَ: فَقَالَ لِي أَبُو طَلْحَةَ: اخْرُجْ، فَأَهْرِقْهَا، فَخَرَجْتُ فَهَرَقْتُهَا، فَجَرَتْ فِي سِكَكِ المَدِينَةِ، فَقَالَ بَعْضُ القَوْمِ: قَدْ قُتِلَ قَوْمٌ وَهِيَ فِي بُطُونِهِمْ، فَأَنْزَلَ اللَّهُ: {لَيْسَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ جُنَاحٌ فِيمَا طَعِمُوا} [المائدة: 93] الآيَةَ.
Imepokewa kutoka kwa Anas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake amesema: Nilikuwa nikihudumia watu vinywaji katika nyumba ya Abuu Twalha, na pombe yao wakati huo ilikuwa ni mchanganyiko, akaamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mwenye kunadi akanadi: Tambueni kuwa pombe imekwisha haramishwa, akasema: Abuu Twalha akasema kuniambia: Toka, nenda kaimwage, nikatoka nikaimwaga, ikatiririka pombe mitaro ya Madina, baadhi ya watu wakasema: Wameuliwa baadhi ya watu na pombe ikiwa tumboni mwao, Mwenyezi Mungu akateremsha: "Hapana ubaya kwa wale walioamini na akafanya matendo mema katika vile walivyokula" [Al-Maaida: 93] Mpaka mwisho wa aya.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Anas bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba alikuwa akitoa huduma ya vinywaji (pombe) kwa wale waliokuwa katika nyumba ya mume wa mama yake Abuu Twalha radhi za Allah za ziwe juu yake, na pombe yao wakati huo ilikuwa ni mchanganyiko, kati ya tende mbivu na tende mbichi, ghafla mnadiji wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akanadi: Tambueni kuwa pombe imekwisha haramishwa, akasema: Anasema: Abuu Twalha akasema kuniambia, toka nenda kaimwage na uimimine, nikatoka nikaimwaga na nikaimimina, pombe ikatiririka katika mitaro ya Madina, wakasema baadhi ya watu: Wameuliwa baadhi ya Maswahaba na pombe ikiwa tumboni mwao ikiwa bado haijaharamishwa, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hapana ubaya kwa wale walioamini na wakafanya matendo mema katika yale waliyokula". [Al-Maaida: 93] Mpaka mwisho wa aya. Yaani: Hawana dhambi wale walioamini katika vile walivyokula na kunywa katika pombe kabla ya kuharamishwa kwake.

Mafunzo
  1. Ubora wa Abuu Twalha na Maswahaba wengine radhi za Allah ziwe juu yao, pale walipoitikia amri ya Mwenyezi Mungu kwa haraka bila kuuliza, na hivi ndivyo inavyotakiwa kwa muislamu wa kweli.
  2. Pombe: Ni jina linalokusanya kila chenye kulewesha.
  3. Fadhii: Ni kinywaji kinachotokana na tende mbichi na tende mbivu pasina kupikwa, na Busri: Ni matunda ya tende kabla hajaanza kuiva.
  4. Amesema bin Hajari: Amesema Mulhib: Bila shaka pombe ilimwagwa barabarani ili kutangaza kuikataa kwake na kutangaza kuiacha kwake, na hili linakuwa na masilahi makubwa kuliko kukereka kwa kuimwaga kwake barabarani.
  5. Kumebainishwa rehema ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na kwamba hawahesabu watu katika kitendo kabla ya kuteremsha hukumu.
  6. Mwenyezi Mungu Mtukufu ameharamisha pombe; kwakuwa ndani yake kuna uharibifu ambao madhara yake yanarudi katika akili na mali, na kwa sababu yake mtu hutenda madhambi mengi; kwa kutoweka akili yake.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 132) (2464). صحيح مسلم (3/ 1570) (1980). النهاية في غريب الحديث والأثر (709) (1006). فتح الباري لابن حجر (1/ 133). إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (4/ 267).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kinacholewesha kikiwa kingi, basi hata kidogo ni haramu

عَنْ جَابِرِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ رَضيَ اللهُ عنهُما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَا أَسْكَرَ كَثِيرُهُ فَقَلِيلُهُ حَرَامٌ».
Kutoka kwa Jaabir bin Abdillah radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake, amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: "Kinacholewesha kikiwa kingi, basi hata kidogo ni haramu".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy, Ibn Majah na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakuwa kila kinywaji au chakula kinachoondosha akili wakati wa kukitumia kingi chake, basi kukitumia kidogo chake ni haramu, hata kisipoondosha akili.

Mafunzo
  1. Sheria imehifadhi akili za watu.
  2. Kufaa kuzingatia mlango wa kuzuia sababu zinazopelekea katika maovu, na hiyo ni kwa kufunga kila njia inayopelekea katika machafu hayo.
  3. Kumeharamishwa kichache katika kilevi; kwa sababu ndio njia ya kulewa.
  4. Kisipolewesha si kidogo wala kingi, basi hicho si haramu.
Marejeo

سنن أبي داود (5/ 523) (3681). سنن الترمذي (3/ 442) (1865). سنن ابن ماجه (4/ 475) (3393). مسند أحمد (23/ 51) (14703). فتح ذي الجلال والإكرام بشرح بلوغ المرام (5/ 418). شرح سنن أبي داود للعباد (417/ 9). النهاية في غريب الحديث والأثر (437).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila kilevi ni haramu.

عَنْ أَبِي بُرْدَةَ، عَنْ أَبِيهِ أَبِي مُوسَى الأَشْعَريِّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ: أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَعَثَهُ إِلَى اليَمَنِ، فَسَأَلَهُ عَنْ أَشْرِبَةٍ تُصْنَعُ بِهَا، فَقَالَ: وَمَا هِيَ؟، قَالَ: «البِتْعُ وَالمِزْرُ»، فَقِيلَ لِأَبِي بُرْدَةَ: مَا البِتْعُ؟ قَالَ: نَبِيذُ العَسَلِ، وَالمِزْرُ: نَبِيذُ الشَّعِيرِ، فَقَالَ: «كُلُّ مُسْكِرٍ حَرَامٌ» خرجه البخاري. وَخَرَّجَهُ مُسْلِمٌ وَلَفْظُهُ: قَالَ: بَعَثَنِي رَسُولُ اَلله أَنَا وَمُعَاذٌ إِلَى اَليَمَنِ، فَقُلْتُ: يَا رَسُولُ اَللَّهِ! إِنَّ شَرَابًا يُصْنَعُ بِأَرْضِنَا يُقَال لَهُ: المِزَرُ مِنَ الشَّعِيرِ، وَشَرَابٌ يُقَالُ لَهُ: البِتْعُ مِنَ العَسَلِ، فَقَالَ: «كُلُّ مُسْكِرٍ حَرَامٌ». وَفِي رِوَايَةٍ لِمُسْلِمٍ: «فَقَالَ: كُلُّ مَا أَسْكَرَ عَنِ الصَّلَاةِ فَهُوَ حَرَامٌ». وَفِي رِوَايَةٍ لَهُ: «وَكَانَ رَسُولُ الله قَدْ أُعْطِيَ جَوَامِعَ الكَلِمِ بِخَوَاتِمِهِ، فَقَالَ: أَنْهَى عَنْ كُلِّ مُسْكِرٍ أَسْكَرَ عَنْ الصَّلَاةِ».
Kutoka kwa Abuu Buraida, kutoka kwa baba yake kutoka kwa Abuu Musa A-Ash'ari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimtuma kwenda Yemen, akamuuliza kuhusu vinywaji fulani vinavyotengenezwa huko, akasema: Ni vipi hivyo?, akasema: "Ni Bit'u na Mizru" akaulizwa Abuu Buraida: Bit'u ni nini? Akasema: Ni mvinyo wa Asali, na Mizru: Ni mvinyo wa ngano, akasema: "Kila kilevi ni haramu" Ameitoa Bukhari. Na ameitoa Muslim na tamko lake ni: Alisema: Alinituma Mtume rehema na amani ziwe juu yake mimi pamoja na Muadh kwenda Yemen, nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Kuna vinywaji hutengenezwa huko katika nchi yetu vinaitwa: Mvinyo wa Mizru hutengenezwa kwa ngano, na kinywaji kingine huitwa: Bit'u hutengenezwa kwa Asali, akasema: "Kila chenye kulewesha ni haramu". Na katika riwaya nyingine ya Muslim: "Akasema: "Kila chenye kulewesha dhidi ya swala ni haramu". Na katika riwaya yake nyingine: "Na alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kapewa maneno machache yenye kukusanya maana nyingi mwisho wake, akasema: Ninakataza kila kilevi chenye kulewesha dhidi ya swala".
Imepokelewa na Bukhari na MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Abuu Musa Al-Ash'ari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimtuma kwenda Yemen, akamuuliza kuhusu vinywaji vinavyo tengenezwa huko je ni haramu, akamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu hilo. Akasema Abuu Musa radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Ni Bit'u: Yaani mvinyo wa Asali, na Muruuz: Ni mvinyo wa ngano. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake na alikuwa amepewa maneno machache yenye maana pana: "Kile chenye lewesha ni haramu".

Mafunzo
  1. Mvinyo: Ni maji yanayotiwa tende ndani yake au Asali au Ngano na mfano wake; yakafyonza ladha na utamu, na wakati mwingine huenda yakapata kilevi baada ya hapo yakawa ni kilevi.
  2. Hadithi hii ni kanuni katika kuharamisha aina zote za vilevi kama pombe na bangi na nyinginezo.
  3. Umuhimu wa kuuliza yale anayoyahitajia Muislamu.
  4. Ilikuwa mwanzo ilipoharamishwa pombe ni wakati swala inapoingia, pindi waliposwali baadhi ya watu waliohamia Madina na wakasoma wakachanganya ndani ya kisomo chao; ikateremka kauli yake: "Enyi mlio amini! Msiikaribia swala hali nyinyi mmelewa mpaka mjue mnachokisema" [An Nisaa: 43]. Na alikuwa muadhini wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akinadi: Msiikaribie swala hali yakuwa mmelewa. Kisha Mwenyezi Mungu akaiharamisha moja kwa moja kwa kauli yake: "Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa (90) Hakika Shetani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kupitia ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je, mmeacha?" [Al-Maidah: 90,91].
  5. Nikuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu aliiharamisha pombe kulingana na madhara na maovu makubwa yaliyomo.
  6. Kinachozingatiwa katika uharamu ni uwepo wa sifa ya kilevi; mvinyo ukisifika kwa sifa ya kilevi basi ni haramu, na usipokuwa na kilevi basi ni halali.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 104) (5575). صحيح مسلم (3/ 1587) (2003). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (8/ 519). فتح ذي الجلال والاكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (5/ 418). توضِيحُ الأحكَامِ مِن بُلوُغ المَرَام، للبسام (6/ 307). معالم السنن، وهو شرح سنن أبي داود، للخطابي (4/ 264). الفتح الرباني لترتيب مسند الإمام أحمد بن حنبل الشيباني، للساعاتي (16/ 116). فيض القدير شرح الجامع الصغير، للمناوي (5/ 30). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (6/ 2382).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com