Anaeleza Abuu Musa Al-Ash'ari radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimtuma kwenda Yemen, akamuuliza kuhusu vinywaji vinavyo tengenezwa huko je ni haramu, akamuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu hilo. Akasema Abuu Musa radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake: Ni Bit'u: Yaani mvinyo wa Asali, na Muruuz: Ni mvinyo wa ngano. Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake na alikuwa amepewa maneno machache yenye maana pana: "Kile chenye lewesha ni haramu".
- Mvinyo: Ni maji yanayotiwa tende ndani yake au Asali au Ngano na mfano wake; yakafyonza ladha na utamu, na wakati mwingine huenda yakapata kilevi baada ya hapo yakawa ni kilevi.
- Hadithi hii ni kanuni katika kuharamisha aina zote za vilevi kama pombe na bangi na nyinginezo.
- Umuhimu wa kuuliza yale anayoyahitajia Muislamu.
- Ilikuwa mwanzo ilipoharamishwa pombe ni wakati swala inapoingia, pindi waliposwali baadhi ya watu waliohamia Madina na wakasoma wakachanganya ndani ya kisomo chao; ikateremka kauli yake: "Enyi mlio amini! Msiikaribia swala hali nyinyi mmelewa mpaka mjue mnachokisema" [An Nisaa: 43]. Na alikuwa muadhini wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akinadi: Msiikaribie swala hali yakuwa mmelewa. Kisha Mwenyezi Mungu akaiharamisha moja kwa moja kwa kauli yake: "Enyi mlio amini! Bila ya shaka ulevi na kamari, na kuabudu masanamu, na kupiga ramli ni uchafu katika kazi ya Shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa (90) Hakika Shetani anataka kutia kati yenu uadui na chuki kupitia ulevi na kamari, na akuzuieni kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kusali. Basi je, mmeacha?" [Al-Maidah: 90,91].
- Nikuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu aliiharamisha pombe kulingana na madhara na maovu makubwa yaliyomo.
- Kinachozingatiwa katika uharamu ni uwepo wa sifa ya kilevi; mvinyo ukisifika kwa sifa ya kilevi basi ni haramu, na usipokuwa na kilevi basi ni halali.
صحيح البخاري (7/ 104) (5575). صحيح مسلم (3/ 1587) (2003). منحة العلام في شرح بلوغ المرام، لعبد الله الفوزان (8/ 519). فتح ذي الجلال والاكرام بشرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (5/ 418). توضِيحُ الأحكَامِ مِن بُلوُغ المَرَام، للبسام (6/ 307). معالم السنن، وهو شرح سنن أبي داود، للخطابي (4/ 264). الفتح الرباني لترتيب مسند الإمام أحمد بن حنبل الشيباني، للساعاتي (16/ 116). فيض القدير شرح الجامع الصغير، للمناوي (5/ 30). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (6/ 2382).