Ameeleza Anas bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba alikuwa akitoa huduma ya vinywaji (pombe) kwa wale waliokuwa katika nyumba ya mume wa mama yake Abuu Twalha radhi za Allah za ziwe juu yake, na pombe yao wakati huo ilikuwa ni mchanganyiko, kati ya tende mbivu na tende mbichi, ghafla mnadiji wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akanadi: Tambueni kuwa pombe imekwisha haramishwa, akasema: Anasema: Abuu Twalha akasema kuniambia, toka nenda kaimwage na uimimine, nikatoka nikaimwaga na nikaimimina, pombe ikatiririka katika mitaro ya Madina, wakasema baadhi ya watu: Wameuliwa baadhi ya Maswahaba na pombe ikiwa tumboni mwao ikiwa bado haijaharamishwa, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hapana ubaya kwa wale walioamini na wakafanya matendo mema katika yale waliyokula". [Al-Maaida: 93] Mpaka mwisho wa aya. Yaani: Hawana dhambi wale walioamini katika vile walivyokula na kunywa katika pombe kabla ya kuharamishwa kwake.
- Ubora wa Abuu Twalha na Maswahaba wengine radhi za Allah ziwe juu yao, pale walipoitikia amri ya Mwenyezi Mungu kwa haraka bila kuuliza, na hivi ndivyo inavyotakiwa kwa muislamu wa kweli.
- Pombe: Ni jina linalokusanya kila chenye kulewesha.
- Fadhii: Ni kinywaji kinachotokana na tende mbichi na tende mbivu pasina kupikwa, na Busri: Ni matunda ya tende kabla hajaanza kuiva.
- Amesema bin Hajari: Amesema Mulhib: Bila shaka pombe ilimwagwa barabarani ili kutangaza kuikataa kwake na kutangaza kuiacha kwake, na hili linakuwa na masilahi makubwa kuliko kukereka kwa kuimwaga kwake barabarani.
- Kumebainishwa rehema ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na kwamba hawahesabu watu katika kitendo kabla ya kuteremsha hukumu.
- Mwenyezi Mungu Mtukufu ameharamisha pombe; kwakuwa ndani yake kuna uharibifu ambao madhara yake yanarudi katika akili na mali, na kwa sababu yake mtu hutenda madhambi mengi; kwa kutoweka akili yake.
صحيح البخاري (3/ 132) (2464). صحيح مسلم (3/ 1570) (1980). النهاية في غريب الحديث والأثر (709) (1006). فتح الباري لابن حجر (1/ 133). إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (4/ 267).