Ameeleza Abdallah bin Masudi radhi za Allah ziwe juu yake katika kauli yake Aliyetakasika na kutukuka: "Na yeyote anayetaka, ndani ya Msikiti Mtukufu, kwenda kombo na haki kwa njia ya udhalimu na akamuasi Mwenyezi Mungu humo ndani, basi tutamuonjesha adhabu kali yenye kuumiza" [Al-Hajji: 25], akasema: Lau mtu yeyote atawaza ndani ya nafsi yake na akaazimia kufanya jambo baya ndani ya sehemu tukufu ya Makka, likahalalishwa ndani yake aliloliharamisha Mwenyezi Mungu, kama makosa ya ulimi au kuuwa kwa makusudi, basi hiyo ni dhulma, hata kama maazimio atayaweka akiwa katika mji wa Eden huko Yemen, basi huyu atastahiki Mwenyezi Mungu amuonjeshe adhabu chungu kwa sababu ya hilo, hata kama hajalifanya, maazimio yake katika hilo yanatosha.
- Kumebainishwa umahususi wa Haramu na kuitukuza kwake.
- Amesema Assa'diy: Na katika aya hii tukufu, kuna uwajibu wa kuiheshimu Haramu na kuitukuza sana, na tahadhari ya kudhamiria maasi ndani yake na kuyatenda.
- Amesema Adh-dhahaku: Hakika mtu anapodhamiria ovu Makka huku akiwa katika ardhi nyingine linaandikwa juu yake kuwa ni dhambi hata kama hajalitenda.
مسند أحمد (7/ 155) (4071). المستدرك على الصحيحين للحاكم (2/ 420) (3461). إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (10/ 52). جامع العلوم والحكم (2/ 327). النهاية في غريب الحديث والأثر ( ص 829،1012، 597).