عن حُصين بن عبد الرحمن قال: كنتُ عند سعيد بن جُبير فقال: أيكم رأى الكوكب الذي انقَضَّ البارحة؟ فقلتُ: أنا، ثم قلتُ: أما إني لم أكن في صلاة، ولكني لُدغْتُ، قال: فما صنعتَ؟ قلت: ارتقيتُ، قال: فما حَمَلك على ذلك؟ قلت: حديث حدَّثَناه الشعبي، قال: وما حدَّثَكم؟ قلتُ حدثنا عن بريدة بن الحُصيب أنه قال: "لا رُقْية إلا مِن عَيْن أو حُمَة"، قال: قد أحسَن مَن انتهى إلى ما سمع، ولكن حدثنا ابن عباس عن النبي صلى الله عليه وسلم أنه قال:
"عُرضت عليّ الأُمم، فرأيتُ النبي ومعه الرَّهط والنبي ومعه الرجل والرجلان، والنبي وليس معه أحد، إذ رُفع لي سواد عظيم فظننتُ أنهم أمَّتي، فقيل لي: هذا موسى وقومه، فنظرتُ فإذا سواد عظيم، فقيل لي: هذه أمَّتك، ومعهم سبعون ألفا يدخلون الجنة بغير حساب ولا عذاب، ثم نهض فدخل منْزله، فخاض الناس في أولئك؛ فقال بعضهم: فلعلهم الذين صحِبوا رسول الله صلى الله عليه وسلم وقال بعضهم: فلعلهم الذين وُلِدُوا في الإسلام فلم يشركوا بالله شيئا، وذكروا أشياء، فخرج عليهم رسول الله صلى الله عليه وسلم فأخبروه، فقال: هم الذين لا يَسْتَرقون، ولا يَكْتَوُون، ولا يَتَطَيَّرون، وعلى ربهم يتوكلون، فقام عُكاشة بن مِحصَن فقال: ادع الله أن يجعلني منهم، قال: أنت منهم، ثم قام جل آخر فقال: ادع الله أن يجعلني منهم، فقال: سَبَقَك بها عكاشة".
Kutoka kwa Huswain bin Abdirrahman amesema: Nilikuwa kwa Saidi bin Jubair akasema: Ni nani kati yenu aliyeiona nyota iliyodondoka jana usiku? Nikasema: Mimi, kisha nikasema: Ama mimi sikuwa katika swala, lakini niling'atwa na Nge, akasema: nini ulifanya? nikasema: nilijisomea Ruqya, akasema: Ni nini kilikupelekea kufanya hivyo? Nikasema: Ni hadithi aliyotuhadithia Sha'abiy, akasema: Aliwahadithia nini? Nikasema: Alituhadithia kutoka kwa Buraida bin Huswaib yakwamba yeye amesema:"Hakuna kisomo cha ruqya isipokuwa kwa kijicho au homa", Akasema: Amefanya vizuri aliyeishia pale aliposikia, lakini alituhadithia sisi bin Abbasi kutoka kwa Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Nilikusanyiwa mimi Ummati, nikamuona Nabii akiwa pamoja na kundi na Nabii akiwa pamoja na mtu mmoja na watu wawili, Na Nabii akiwa hana hata mtu mmoja, Ghafla ukanyanyuliwa kwangu weusi mkubwa, nikadhania kuwa hao ni umma wangu, nikaambiwa: Huyu ni Musa na watu wake, nikatazama tena, Ghafla nikaona weusi mkubwa, nikaambiwa: Huu ni umma wako, Ukiwa pamoja na watu elfu sabini wanaingia peponi bila hesabu wala adhabu, kisha akanyanyuka akaingia nyumbani kwake, watu wakazungumza mengi kuhusu watu hao (wanaoingia peponi bila hesabu wala adhabu); Wakasema baadhi yao: Huenda hao ni wale waliosuhubiana (walioambatana) na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Na wakasema baadhi yao: Huenda hao ni wale waliozaliwa katika uislamu na wakawa hawakumshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote, Na wakataja mambo mengi! Basi akatoka kwao Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- wakamueleza, Akasema: Hao ni wale ambao hawaombi watu kuwasomea ruqya, na wala hawajitibu kwa moto, na wala hawaamini mikosi ya ndege, na kwa Mola wao ndiko wanakotegemea, hapo akasimama (bwana mmoja akiitwa) Ukasha bin Mihswani akasema: Muombe Mwenyezi Mungu anifanye kuwa miongoni mwao, akasema: Wewe ni miongoni mwao, kisha akasimama mtu mwingine akasema: Muombe Mwenyezi Mungu anifanye kuwa miongoni mwao, Akasema: kakutangulia kwa hilo Ukasha".
Wamekubaliana Bukhaariy na MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anatueleza Huswain bin Abdirrahman -Mwenyezi Mungu amrehemu- kuhusu mazungumzo yaliyojiri kati yake na Saidi bin Jubair -Mwenyezi Mungu amrehemu- kuhusu swala la kisomo cha Ruqya,Na hiyo ni kwasababu Huswain aling'atwa na nge na akajisomea kwaajili ya hilo ruqya ya kisheria, na alipomuuliza Saidi kuhusu ushahidi wake akamueleza kwa hadithi ya Sha'biy ambayo ina halalisha ruqya kwasababu ya kijicho au sumu,Saidi akamsifia kwa hilo,lakini yeye akampokelea hadithi ambayo inayopendekeza kuacha kufanya ruqya, nayo ni hadithi ya bin Abbasi ambayo inaambatana na sifa Nne ambazo atakayesifika nazo atastahiki kuingia peponi bila hesabu wala adhabu, nazo ni kutotafuta kisomo cha ruqya, na kutojitibu kwa moto,na kutoamini mikosi, na ukweli wa kutegemea kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu,na alipoomba Ukasha toka kwa Nabii-Rehema na Amani ziwe juu yake- kuwa amuombee ili awe miongoni mwao akamueleza kuwa yeye ni miongoni mwao,na aliposimama mtu mwingine kwa lengo hilo hilo akamjibu kwa upole Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa kumzuilia hilo na kwa kufunga mlango na kukata muendelezo wa watu wengine.
Marejeo
-صحيح البخاري، المحقق: محمد زهير بن ناصر الناصر، الناشر: دار طوق النجاة (مصورة عن السلطانية بإضافة ترقيم محمد فؤاد عبد الباقي)، الطبعة: الأولى، 1422ه.
-صحيح مسلم، المحقق: محمد فؤاد عبد الباقي - الناشر: دار إحياء التراث العربي - بيروت.
-الملخص في شرح كتاب التوحيد، دار العاصمة، الرياض، الطبعة: الأولى، 1422ه - 2001م.
-الجديد في شرح كتاب التوحيد، مكتبة السوادي، جدة، المملكة العربية السعودية، الطبعة: الخامسة، 1424هـ - 2003م.
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعن عبد الله بن مسعود رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: «إنَّ الرُّقَى والتَمائِمَ والتِّوَلَةَ شِرْكٌ».
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "Hakika makombe, na hirizi, na limbwata, ni ushirikina".
Imepokelewa na Abu Daud, Ibn Majah na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- vitu ambavyo kuvifanya kwake ni katika ushirikina; na miongoni mwavyo ni:
Cha kwanza: Makombe: Ni maneno ambayo watu wajinga huyatumia kama tiba yanayoambatana na ushirikina.
Cha pili: Vyenye kutundikwa ni kama hirizi na mfano wake: zinazotundikwa kwa watoto wadogo na wanyama na wengineo kwa ajili ya kuzuia kijicho.
Cha tatu: Limbwata: Ambalo hutengenezwa ili mmoja kati ya wanandoa amvute mwenzake kimapenzi.
Mambo haya yote ni katika ushirikina: Kwa sababu hii ni katika kukifanya kitu kuwa sababu, hali yakuwa si sababu ya kisheria iliyothibiti kwa ushahidi, wala si sababu inayoonekana wazi iliyothibiti kwa majaribio. Ama sababu za kisheria kama kusoma Qur'ani, au zenye kuonekana kama dawa zilizothibiti kwa majaribio, hizi zinafaa pamoja na kuamini kuwa hizi ni sababu tu, nakuwa manufaa na madhara yako mkononi mwa Mwenyezi Mungu.
Mafunzo
- Kuilinda tauhidi na itikadi dhidi ya yale yenye kuzibomoa.
- Uharamu wa kutumia makombe ya kishirikina na hirizi na limbwata.
- Mtu kuamini katika mambo matatu haya kuwa yenyewe ndiyo sababu: Hii ni shirki ndogo; Kwa sababu hii ni kuyafanya yasiyokuwa sababu kuwa ni sababu, ama akiitakidi kuwa yananufaisha na kudhuru yenyewe hii ni shirki kubwa.
- Tahadhari ya kufanya sababu za kishirikina na zilizoharamishwa.
- Kumeharamishwa makombe na kuwa ni katika shirki isipokuwa yale yatakayokuwa kisheria.
- Ni lazima moyo ufungamane na Mwenyezi Mungu peke yake, kwake ndio hutoka madhara na manufaa peke yake asiyekuwa na mshirika, hakuna aletaye kheri isipokuwa Allah na hakuna azuiaye shari isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Ruqiya inayofaa ni ile iliyoambatana na sharti tatu: 1- Aitakidi kuwa ni sababu na wala haiwezi kunufaisha isipokuwa kwa idhini ya Allah. 2- Iwe kwa Qur'ani na majina ya Mwenyezi Mungu na sifa zake na dua za Mtume za kisheria. 3- Iwe kwa lugha inayofahamika, na wala isiambatane na matalasimu na mazingaombwe.
Marejeo
سنن أبي داود (6/ 31) (3883).
سنن ابن ماجه (4/ 554) (3530).
مسند أحمد (6/ 110) (3615).
الجديد في شرح كتاب التوحيد، لمحمد القرعاوي (ص91).
الملخص في شرح كتاب التوحيد، لصالح الفوزان (ص79).
القول المفيد على كتاب التوحيد، لابن عثيمين (1/ 180).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المؤْمنينَ رَضيَ اللهُ عنها قَالَت: كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا أَتَى الْمَرِيضَ يَدْعُو لَهُ قَالَ: «أَذْهِبِ الْبَاسَ، رَبَّ النَّاسِ، وَاشْفِ أَنْتَ الشَّافِي، لَا شِفَاءَ إِلَّا شِفَاؤُكَ، شِفَاءً لَا يُغَادِرُ سَقَمًا».
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapomuendea mgonjwa basi anamuombea dua, anasema "Ondosha tatizo, ewe Mola wa watu, na ponya kwani wewe ndiye mponyaji, hakuna ponyo ila ponyo lako, ponyo lisiloacha ugonjwa".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapomtembelea mgonjwa anamuombea dua kwa kusema: Ewe Mwenyezi Mungu "Ondoa" ondosha "ugumu" na ukali wa maradhi, "Ewe Mola wa watu" na Muumba wao na Mlezi wao, "na ponya" maradhi haya "wewe" Mtukufu "Ndiye mponyaji" na ninaomba kupitia jina lako Mponyaji, "hakuna ponyo" linaloweza kupatikana kwa mgonjwa "isipokuwa ponyo lako" na afya yako, "ponyo" la moja kwa moja "lisiloacha" na kubakisha na kuacha "ugonjwa" na maradhi mengine.
Mafunzo
- Mponyaji ni Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka, na daktari na dawa hivyo vyote ni sababu, havinufaishi wala havidhuru isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
- Kumtembelea mgonjwa ni katika haki zilizoko baina ya waislamu, nayo kwa familia inakuwa ni haki zaidi.
- Himizo kwa mwenye kumtembelea mgonjwa amuombee dua hii yenye baraka na iliyonukuliwa kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
- Miongoni mwa muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kujitibu kwa kisomo (cha Ruqya) ya kisheria kwa Qur'ani na dua nzuri, alikuwa rehema na amani ziwe juu yake akijisomea mwenyewe anapougua, na vile vile alikuwa akimsomea yeyote mwenye kuhisi maumivu katika familia yake na watu wengine pia.
- Amesema bin Hajari: Na imewatatiza baadhi ya watu dua ya kumuombea mgonjwa kupona hali yakuwa katika maradhi kuna kufutiwa madhambi na kupata thawabu kama zilivyokuja hadithi kwa wingi kuhusu hilo, na jawabu la hilo: Nikuwa dua ni ibada, na wala haiondoi thawabu na kufutiwa makosa; kwa sababu hayo hupatikana mwanzoni mwa ugonjwa na pale mtu anaposubiri juu ya maradhi, na muombaji anakuwa kati ya neema mbili: Ima apate lengo lake, au apewe badala kwa kuletewa manufaa au kuzuiliwa madhara, na yote hayo ni kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Marejeo
صحيح البخاري (7/ 134) (5750).
صحيح مسلم (4/ 1721) (2191).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 162).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 477).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (11/ 539).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 687).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أَبِي سَعِيدٍ رَضيَ اللهُ عنه: أَنَّ جِبْرِيلَ أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: يَا مُحَمَّدُ اشْتَكَيْتَ؟ فَقَالَ: «نَعَمْ» قَالَ: «بِاسْمِ اللهِ أَرْقِيكَ، مِنْ كُلِّ شَيْءٍ يُؤْذِيكَ، مِنْ شَرِّ كُلِّ نَفْسٍ أَوْ عَيْنِ حَاسِدٍ، اللهُ يَشْفِيكَ بِاسْمِ اللهِ أَرْقِيكَ».
Kutoka kwa Abuu Saidi Al Khudri -radhi za Allah ziwe juu yake-: Ya kwamba Jibril alimjia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Ewe Muhammad umetekesa kwa maumivu? Akasema: "Ndiyo" Akasema: "Bismillaahi Arqiika, Min kulli shai-in Yu-udhiika, min sharri kulli nafsin Au Aini Haasidin, Allaahu yash-fiika, bismillaahi Arqiika" Yaani: Kwa jina la Mwenyezi Mungu ninakuombea, kutokana na kila kitu kinachokuudhi, na kutokana na shari ya kila nafsi au jicho la hasidi, Mwenyezi Mungu atakuponya, kwa jina la Mwenyezi Mungu ninakusomea.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Alikuja Malaika Jibril amani iwe juu yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akamuuliza: Ewe Muhammad, unalalamika kwa maradhi? Akasema: Ndiyo. Jibril akamsomea Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kwa kusema: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu" Kwa kutaka msaada kwa jina hilo "Ninakusomea" na ninakukinga, "kutokana na kila kitu kinachokuudhi" Kiwe kikubwa au kidogo, "kutokana na shari ya kila nafsi" chafu, "au jicho la hasidi" lisije kukufika, basi Mwenyezi Mungu "atakuponya" na akukinge na akuhifahdi dhidi ya kila maradhi, "kwa jina la Mwenyezi Mungu ninakuombea" amelikariri neno hili kwa ajili ya ziada, na ameanza nalo na amemaliza nalo akiashiria kuwa hakuna awezaye kunufaisha isipokuwa Yeye Mtukufu.
Mafunzo
- Kufaa kuelezea maradhi ikiwa kama ni kuelezea uhalisia wa hali, na si sehemu ya kunung'unika na kulalamika.
- Inafaa kusoma Ruqya kwa sharti zifuatazo: 1- Iwe kwa Qur'ani au kwa kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu na dua za kisheria. 2- Iwe kwa lugha ya kiarabu, au kwa maneno yanayoeleweka maana yake katika lugha zingine. 3- Aamini kuwa Ruqya haiathiri yenyewe; bali ni sababu miongoni mwa sababu, haina athari yoyote isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka. 4- Iiepukane na ushirikina, au haramu, au uzushi, au yenye kupelekea katika hayo.
- Kumethibitishwa madhara ya kijicho, na kwamba ni kweli, inatakiwa kujisomea kutokana na kijicho.
- Ni sunna kujifanyia kisomo kupitia yale yaliyokuja katika hadithi.
- Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kama watu wengine, humtokea yale yanayowatokea watu wengine, kama maradhi.
- Ulinzi wa Mwenyezi Mungu kwa Nabii wake na kumuhifadhi kwake, na kumuwekea kwake Malaika kwa ajili ya hilo.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 1718) (2186).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 164).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص538).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 485).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (11/ 568).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 690).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ عُثْمَانَ بْنِ أَبِي الْعَاصِ الثَّقَفِيِّ رضي الله عنه أَنَّهُ شَكَا إِلَى رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَجَعًا يَجِدُهُ فِي جَسَدِهِ مُنْذُ أَسْلَمَ، فَقَالَ لَهُ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «ضَعْ يَدَكَ عَلَى الَّذِي تَأَلَّمَ مِنْ جَسَدِكَ، وَقُلْ بِاسْمِ اللهِ ثَلَاثًا، وَقُلْ سَبْعَ مَرَّاتٍ أَعُوذُ بِاللهِ وَقُدْرَتِهِ مِنْ شَرِّ مَا أَجِدُ وَأُحَاذِرُ».
Kutoka kwa Othman bin Abil Aswi Ath-thaqafi radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba yeye alilalamika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu maumivu anayoyapata katika mwili wake tangu aliposilimu, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: "Weka mkono wako juu ya mahala panapoumia katika mwili wako, na usema: Bismillaah, (kwa jina la Mwenyezi Mungu) mara tatu, na useme mara saba: Audhubillaahi wa quduratihi min sharri maa ajidu wa uhaadhiru (Ninajikinga kwa Mwenyezi Mungu na uwezo wake kutokana na shari ya kile ninachokipata na kile ninachokihofia)"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Othman bin Abil Aswi alipata maumivu makali ambayo yalikaribia kumuua, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaenda kumtembelea, na akamfundisha dua ambayo Mwenyezi Mungu atamuondolea maradhi yaliyomfika; nayo ni aweke mkono wake juu ya mahala panapoumia, na aseme: "Bismillaah" mara tatu, kisha aseme mara saba: "Ninataka kinga" na ninajikinga na kujiweka na kujilinda (kwa Mwenyezi Mungu na kudura zake kutokana na shari za yale ninayoyapata) katika maumivu ya wakati huu (na kuyahofia) na ninahofia kutokea maumivu mengine baadaye miongoni mwa huzuni na hofu, au kuendelea kwa maradhi na yakasambaa maumivu yake katika mwili.
Mafunzo
- Sunna ya mtu kujifanyia kisomo cha ruqya yeye mwenyewe kama ilivyokuja katika hadithi.
- Malalamiko -pasina kuchukizwa na hali wala kupingana na Kadari- hakupingani na kutawakali na subira.
- Dua ni miongoni mwa kuchukua sababu, na ndio maana ni lazima kushikamana na matamshi yake na idadi yake.
- Dua hii inasomwa kwa maumivu ya kila kiungo.
- Kuweka mkono juu ya mahala palipo na maumivu wakati wa kusoma dua hii.
Marejeo
صحيح مسلم (4/ 1728) (2202).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 163).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 481).
فيض القدير شرح الجامع الصغير، لعبدالرؤوف المناوي (1/ 284).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 689).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضي الله عنهما عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ عَادَ مَرِيضًا، لَمْ يَحْضُرْ أَجَلُهُ فَقَالَ عِنْدَهُ سَبْعَ مِرَارٍ: أَسْأَلُ اللَّهَ الْعَظِيمَ رَبَّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ أَنْ يَشْفِيَكَ، إِلَّا عَافَاهُ اللَّهُ مِنْ ذَلِكَ الْمَرَضِ».
Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao -kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - amesema: "Atakayemtembelea mgonjwa ambaye hajafikiwa na mauti, akasema akiwa kwake mara saba: Namuomba Allah Mtukufu, Mola wa Arshi Tukufu, akuponye, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamponya kwa maradhi hayo".
Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yakuwa hakuna muislamu atakayemtembelea muislamu katika maradhi yake, ambaye muda wa mauti yake haujafika, kisha aliyekwenda kumtembelea akamuombea mgonjwa kwa kusema: "Namuomba Allah Mtukufu" katika dhati yake na sifa zake na vitendo vyake, "Mola wa Arshi Tukufu akuponye", na akarudia mbele yake mara saba, isipokuwa Mwenyezi Mungu atamponya kutokana na maradhi hayo.
Mafunzo
- Inapendeza kumuombea mgonjwa kwa dua hii, na kuirudiarudia mara saba.
- Kupatikana kwa ponyo kwa atakayeombewa mbele yake dua hii kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ikisomwa kwa dhati na kwa mtu mwema.
- Ataisoma dua hii kwa siri na kwa wazi, yote hiyo inafaa, lakini akimsikilizisha mgonjwa ndiyo bora zaidi; kwa sababu katika hilo kuna kuingiza furaha kwake.
Marejeo
سنن أبي داود (5/ 22) (3106).
سنن الترمذي (3/ 593) (2083).
السنن الكبرى للنسائي (9/ 385) (10820).
مسند أحمد (4/ 40) (2137).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 163).
تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص537).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 483).
كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (11/ 559).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 689).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comKila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com