Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Bismillaahi Arqiika, Min kulli shai-in Yu-udhiika, min sharri kulli nafsin Au Aini Haasidin, Allaahu yash-fiika, bismillaahi Arqiika" Yaani: Kwa jina la Mwenyezi Mungu ninakuombea, kutokana na kila kitu kinachokuudhi, na kutokana na shari ya kila nafsi au jicho la hasidi, Mwenyezi Mungu atakuponya, kwa jina la Mwenyezi Mungu ninakusomea

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ رَضيَ اللهُ عنه: أَنَّ جِبْرِيلَ أَتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ: يَا مُحَمَّدُ اشْتَكَيْتَ؟ فَقَالَ: «نَعَمْ» قَالَ: «بِاسْمِ اللهِ أَرْقِيكَ، مِنْ كُلِّ شَيْءٍ يُؤْذِيكَ، مِنْ شَرِّ كُلِّ نَفْسٍ أَوْ عَيْنِ حَاسِدٍ، اللهُ يَشْفِيكَ بِاسْمِ اللهِ أَرْقِيكَ».
Kutoka kwa Abuu Saidi Al Khudri -radhi za Allah ziwe juu yake-: Ya kwamba Jibril alimjia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Ewe Muhammad umetekesa kwa maumivu? Akasema: "Ndiyo" Akasema: "Bismillaahi Arqiika, Min kulli shai-in Yu-udhiika, min sharri kulli nafsin Au Aini Haasidin, Allaahu yash-fiika, bismillaahi Arqiika" Yaani: Kwa jina la Mwenyezi Mungu ninakuombea, kutokana na kila kitu kinachokuudhi, na kutokana na shari ya kila nafsi au jicho la hasidi, Mwenyezi Mungu atakuponya, kwa jina la Mwenyezi Mungu ninakusomea.
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Alikuja Malaika Jibril amani iwe juu yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akamuuliza: Ewe Muhammad, unalalamika kwa maradhi? Akasema: Ndiyo. Jibril akamsomea Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kwa kusema: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu" Kwa kutaka msaada kwa jina hilo "Ninakusomea" na ninakukinga, "kutokana na kila kitu kinachokuudhi" Kiwe kikubwa au kidogo, "kutokana na shari ya kila nafsi" chafu, "au jicho la hasidi" lisije kukufika, basi Mwenyezi Mungu "atakuponya" na akukinge na akuhifahdi dhidi ya kila maradhi, "kwa jina la Mwenyezi Mungu ninakuombea" amelikariri neno hili kwa ajili ya ziada, na ameanza nalo na amemaliza nalo akiashiria kuwa hakuna awezaye kunufaisha isipokuwa Yeye Mtukufu.

Mafunzo
  1. Kufaa kuelezea maradhi ikiwa kama ni kuelezea uhalisia wa hali, na si sehemu ya kunung'unika na kulalamika.
  2. Inafaa kusoma Ruqya kwa sharti zifuatazo: 1- Iwe kwa Qur'ani au kwa kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu na dua za kisheria. 2- Iwe kwa lugha ya kiarabu, au kwa maneno yanayoeleweka maana yake katika lugha zingine. 3- Aamini kuwa Ruqya haiathiri yenyewe; bali ni sababu miongoni mwa sababu, haina athari yoyote isipokuwa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka. 4- Iiepukane na ushirikina, au haramu, au uzushi, au yenye kupelekea katika hayo.
  3. Kumethibitishwa madhara ya kijicho, na kwamba ni kweli, inatakiwa kujisomea kutokana na kijicho.
  4. Ni sunna kujifanyia kisomo kupitia yale yaliyokuja katika hadithi.
  5. Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kama watu wengine, humtokea yale yanayowatokea watu wengine, kama maradhi.
  6. Ulinzi wa Mwenyezi Mungu kwa Nabii wake na kumuhifadhi kwake, na kumuwekea kwake Malaika kwa ajili ya hilo.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 1718) (2186). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (2/ 164). تطريز رياض الصالحين، لفيصل آل مبارك (ص538). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (4/ 485). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (11/ 568). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 690).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Ruq'ya ya Kisheria.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com