عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضيَ اللهُ عنهما: أنَّهُ قَالَ لعَطَاءِ بْنِ أَبِي رَبَاحٍ: أَلَا أُرِيكَ امْرَأَةً مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ؟ قُلْتُ: بَلَى، قَالَ: هَذِهِ الْمَرْأَةُ السَّوْدَاءُ، أَتَتِ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَتْ: إِنِّي أُصْرَعُ وَإِنِّي أَتَكَشَّفُ، فَادْعُ اللهَ لِي، قَالَ: «إِنْ شِئْتِ صَبَرْتِ وَلَكِ الْجَنَّةُ، وَإِنْ شِئْتِ دَعَوْتُ اللهَ أَنْ يُعَافِيَكِ» قَالَتْ: أَصْبِرُ، قَالَتْ: فَإِنِّي أَتَكَشَّفُ فَادْعُ اللهَ أَنْ لَا أَتَكَشَّفَ، فَدَعَا لَهَا.
Kutoka kwa bin Abbasi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, yeye na baba yake: Ya kwamba pindi aliposema kumwambia Atwaa bin Abii Rabaahi: Hivi je, nikuonyeshe mwanamke miongoni mwa wanawake wa Peponi? Nikasema: Ndio, akasema: Huyu mwanamke mweusi, alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Hakika mimi huanguka, na nguo zangu hufunuka ninapoanguka, nakuomba uniombee kwa Mwenyezi Mungu, akasema: "Ukipenda unaweza kuvumulia na utapata malipo ya Pepo, na ukitaka nitakuombea kwa Mwenyezi Mungu akuponye" Akasema: Bali nitavumilia, akasema: Lakini mimi huwa nafunuka nguo, basi niombee kwa Mwenyezi Mungu nisifunuke, basi akamuombea.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Alisema bin Abbasi Mwenyezi Mungu amuwie radhi kumwambia Atwaa bin Abii Rabaahi: Je, nikuonyeshe mwanamke miongoni mwa watu wa Peponi? Atwaa akasema: Ndio, akasema: Huyu mwanamke muethiopia mweusi, alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: akasema: Hakika mimi nina maradhi, huanguka na kufunuka nguo zangu, na kuonekana sehemu ya mwili wangu pasina mimi kujielewa, basi muombe Mwenyezi Mungu aniponye, akasema: Ukipenda unaweza kuvumilia na utakuwa na malipo ya Pepo, na ukipenda nitamuomba Mwenyezi Mungu akuponye, akasema: Basi nitavumilia, kisha akasema: Basi niombee kwa Mwenyezi Mungu nisifunuke nikianguka, basi akamuombea kwa Mwenyezi Mungu.
Mafunzo
- Subira juu ya mabalaa katika dunia hupelekea kupata Pepo.
- Amesema Nawawi: Na hapa kuna ushahidi kuwa ugonjwa wa kuanguka kwa mtu hulipwa malipo yaliyokamilika
- Tazama heshima na haya kwa wanawake wa kiswahaba, na pupa yao juu ya kujisitiri, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, mwanamke huyu, kubwa zaidi alilokuwa akilihofia ni kufunuka sehemu ya mwili wake.
- Amesema bin Hajari: Kuchukua jambo gumu ni bora kuliko kuchukua ruhusa, kwa mtu atakayejua kuwa anauwezo wa kulibeba, na hatodhoofika kwa kulibeba gumu hilo.
- Amesema bin Hajari: Na hapa nikuwa; tiba ya maradhi yote ni kwa dua na kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, hufaa zaidi na kunufaisha zaidi kuliko tiba ya miti shamba (madawa), na kwamba athari ya hilo na muitikio wa mwili ni mkubwa zaidi kuliko athari ya dawa za mwili, lakini huleta ahueni kwa mambo mawili: La kwanza: Upande wa mgonjwa, kuwa na imani ya kweli na Mwenyezi Mungu, na la pili: Upande wa tabibu, kuwa na nguvu kubwa ya kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, na kuwa na nguvu kubwa ya uchamungu, na kumtegemea Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu Ndiye Mjuzi zaidi.
- Amesema bin Hajari: Hapa kuna ushahidi juu ya kuacha kutumia dawa.
Marejeo
صحيح البخاري (7/ 116) (5652).
صحيح مسلم (4/ 1994) (2576).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 95).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (1/ 235).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ سَهْلُ بْنُ سَعْدٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ يَوْمَ خَيْبَرَ: «لَأُعْطِيَنَّ هَذِهِ الرَّايَةَ غَدًا رَجُلًا يَفْتَحُ اللَّهُ عَلَى يَدَيْهِ، يُحِبُّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَيُحِبُّهُ اللَّهُ وَرَسُولُهُ»، قَالَ: فَبَاتَ النَّاسُ يَدُوكُونَ لَيْلَتَهُمْ أَيُّهُمْ يُعْطَاهَا، فَلَمَّا أَصْبَحَ النَّاسُ غَدَوْا عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كُلُّهُمْ يَرْجُو أَنْ يُعْطَاهَا، فَقَالَ: «أَيْنَ عَلِيُّ بْنُ أَبِي طَالِبٍ؟» فَقِيلَ: هُوَ يَا رَسُولَ اللَّهِ يَشْتَكِي عَيْنَيْهِ، قَالَ: «فَأَرْسِلُوا إِلَيْهِ»، فَأُتِيَ بِهِ فَبَصَقَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي عَيْنَيْهِ وَدَعَا لَهُ، فَبَرَأَ حَتَّى كَأَنْ لَمْ يَكُنْ بِهِ وَجَعٌ، فَأَعْطَاهُ الرَّايَةَ، فَقَالَ عَلِيٌّ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أُقَاتِلُهُمْ حَتَّى يَكُونُوا مِثْلَنَا؟ فَقَالَ: «انْفُذْ عَلَى رِسْلِكَ حَتَّى تَنْزِلَ بِسَاحَتِهِمْ، ثُمَّ ادْعُهُمْ إِلَى الإِسْلاَمِ، وَأَخْبِرْهُمْ بِمَا يَجِبُ عَلَيْهِمْ مِنْ حَقِّ اللَّهِ فِيهِ، فَوَاللَّهِ لَأَنْ يَهْدِيَ اللَّهُ بِكَ رَجُلًا وَاحِدًا، خَيْرٌ لَكَ مِنْ أَنْ يَكُونَ لَكَ حُمْرُ النَّعَمِ».
Kutoka kwa Sahli bin Sa'ad Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume Rehema na Amani za Allah ziwe juu yake alisema siku ya vita vya Khaibari: "Kesho nitampa bendera hii mtu ambaye Mwenyezi Mungu ataleta ushindi kupitia mikononi mwake, ambaye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda." Akasema: Watu wakalala usiku kucha wakijadili hilo, ni nani kati yao atakayepewa! Palipopambazuka watu walikwenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake wote wakitaraji kuwa atapewa, akasema: “Yuko wapi Ally bin Abi Twalib?" pakasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, anaumwa macho, akasema: “Basi mtumieni mtu akamuite.” Akaletwa, Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akamtemea mate machoni mwake na akamuombea, akapona kana kwamba hakuwa na maradhi, hivyo akampa bendera, na Ally akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nipigane nao mpaka wawe kama sisi? Akasema: “Songa mbele, mpaka utue kwenye uwanja wao, kisha uwaite kuja katika Uislamu, na uwafahamishe yale yaliyo wajibu juu yao katika haki za Mwenyezi Mungu kwake, Ninamuapa Mwenyezi Mungu, ikiwa Mwenyezi Mungu atamuongoza mtu mmoja kupitia kwako, hilo ni bora zaidi kwako kuliko ngamia wekundu."
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo
Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliwaeleza Maswahaba kuhusu ushindi wa Waislamu dhidi ya Mayahudi wa Khaibar siku ya kesho, na hilo litakuwa mikononi mwa mtu atakayempa bendera, nayo ni bendera ambayo hutumiwa na jeshi kama nembo yake. Na mtu huyu miongoni mwa sifa zake ni pamoja na kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanampenda. Kwa hiyo Maswahaba walipitisha usiku kucha wakijadiliana na kuzungumza juu ya nani atapewa bendera? Kwa kutamani kuipata heshima hii kubwa, Ilipofika asubuhi walikwenda kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake wote wakiwa na matumaini ya kupata heshima hii.
Basi Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamuulizia Ally bin Abi Twalib Allah amuwie radhi?
Pakasemwa: Ni mgonjwa na analalamika kuhusu macho yake.
Basi rehema na amani zimshukie, akamtumia watu wakamlete, akamtemea Ally machoni katika mate yake matukufu na akamuombea, akapona ugonjwa wake kana kwamba hakuwa na maradhi, akampa bendera na akamwamuru aende kwa upole mpaka aikaribie ngome ya maadui na awaite katika Uislamu, ikiwa watamjibu; Awaambie ni wajibu gani wanapaswa kufanya.
Kisha rehema na amani ziwe juu yake, akamueleza Ally ubora wa kumuita mtu kwa Mwenyezi Mungu, na kwamba ikiwa mlinganiaji atakuwa ni sababu ya kuongoka kwa mtu mmoja, hiyo ni bora zaidi kwake kuliko kuwa na ngamia wekundu ambao ndio utajiri wa thamani zaidi kwa Waarabu, azimiliki au azitoe sadaka.
Mafunzo
- Ubora wa Ally bin Abi Twalib – Mwenyezi Mungu amuwie radhi – na ushahidi wa Mtume – Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani – juu yake, wa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake juu yake, na mapenzi yake kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.
- Maswahaba walikuwa na shauku ya kufanya kheri na kulikimbilia kwao hilo.
- Sheria ya adabu wakati wa vita na kuacha kutojali na kelele zenye kuudhi yasiyokuwa ya lazima.
- Miongoni mwa dalili za utume wake, rehema na amani ziwe juu yake, ni kutoa habari ya ushindi dhidi ya Mayahudi, na kumponya kwake macho Ally bin Abi Twalib mikononi mwake, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.
- Madhumuni makubwa ya Jihadi ni watu kuingia katika Uislamu.
- Nikuwa wito wa kuwaita watu katika Uislamu hutolewa taratibu taratibu, kwanza kafiri ataombwa kusilimu kwa kutamka Shahada mbili, kisha ataamrishwa kutekeleza faradhi za Uislamu baada ya hapo.
- Fadhila za kuwaita watu katika Uislamu na kheri zilizomo kwa mlinganiwaji na mlinganiaji, mlinganiwaji anaweza kuongoka, na mlinganiaji kwa hilo atalipwa malipo makubwa.
Marejeo
صحيح البخاري (5/ 134) (4210).
صحيح مسلم (4/ 1872) (2406).
فتح المجيد شرح كتاب التوحيد، (ص88).
القول المفيد على كتاب التوحيد، (1/ 134).
الملخص في شرح كتاب التوحيد، (ص57).
الجديد في شرح كتاب التوحيد، (ص67).
التمهيد لشرح كتاب التوحيد، (ص59).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com