Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Hukumu za wanawake.

Hadithi 10

Hakika dunia ni tamu, ni ya kijani, na hakika Mwenyezi Mungu anakumilikisheni ndani yake aone ni namna gani mtafanya, iogopeni dunia na waogopeni wanawake

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِنَّ الدُّنْيَا حُلْوَةٌ خَضِرَةٌ، وَإِنَّ اللهَ مُسْتَخْلِفُكُمْ فِيهَا، فَيَنْظُرُ كَيْفَ تَعْمَلُونَ، فَاتَّقُوا الدُّنْيَا وَاتَّقُوا النِّسَاءَ، فَإِنَّ أَوَّلَ فِتْنَةِ بَنِي إِسْرَائِيلَ كَانَتْ فِي النِّسَاءِ».
imepokewaKutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Hakika dunia ni tamu, ni ya kijani, na hakika Mwenyezi Mungu anakumilikisheni ndani yake aone ni namna gani mtafanya, iogopeni dunia na waogopeni wanawake, kwani hakika fitina ya kwanza ya wana wa Israeli ilikuwa kwa wanawake"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Dunia ina ladha tamu, na ni kijani katika mandhari, hivyo mwanadamu hudanganyika nayo na kuikimbilia na kuifanya kuwa ndio hamu yake kubwa. Nakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amewafanya baadhi yetu kuwa warithi wa wengine katika dunia hii, ili aone ni namna gani tutafanya, je tutasimama katika utiifu wake, au maasi yake? Kisha akasema: Tahadharini sana na zisikudanganyeni starehe za Dunia na mapambo yake, zikakupelekeeni kuacha aliyokuamrisheni Mwenyezi Mungu, na kuingia katika yale aliyokukatazeni. Na miongoni mwa mambo makubwa ya wajibu kutahadhari nayo katika fitina za Dunia ni fitina ya wanawake, nakuwa ndio iliyokuwa fitina ya kwanza waliotumbukia ndani yake wana wa Israeli.

Mafunzo
  1. Himizo la kushikamana na uchamungu, na kutojishughulisha na mambo ya kidunia na pambo lake.
  2. Tahadhari ya kufitinika na wanawake, kwa kuwatazama au kujiachia kwa kuchanganyika na wanaume wa kando, au mengineyo.
  3. Fitina ya wanawake ni katika fitina kubwa katika Dunia.
  4. Kuzingatia na kuchukua mafunzo kutoka katika umma zilizotangulia, kilichotokea kwa wana wa Israeli kinaweza kutokea kwa wengine pia.
  5. Fitina ya wanawake, akiwa ni mke anaweza kumbebesha mwanaume mzigo mkubwa wa matumizi asiouweza, na akamshughulisha na kutafuta mambo ya kidunia, na akampelekea kumaliza umri wake katika kuitafuta Dunia, na akiwa ni mwanamke wa kando, anaweza kumfitini kwa kumlaghai mwanaume na kumtoa katika haki pale wanawake wakitoka na kuchanganyika pamoja na wanaume, hasa hasa wakiwa hawajisitiri kisheria, na hili linaweza kupelekea kuingia katika zinaa kwa ngazi zake, hivyo ni lazima kwa muumini kujikinga kwa Mwenyezi Mungu, na kuelekea kwake ili kusalimika na fitina za zao.
Marejeo

صحيح مسلم (4/ 2098) (2742). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 146). كنوز رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (2/ 173). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 103).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Hachukii muumini wa kiume tabia za muumini wa kike, akichukia tabia fulani basi ataridhishwa na tabia nyingine

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي لله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا يَفْرَكْ مُؤْمِنٌ مُؤْمِنَةً، إِنْ كَرِهَ مِنْهَا خُلُقًا رَضِيَ مِنْهَا آخَرَ» أَوْ قَالَ: «غَيْرَهُ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Hachukii muumini wa kiume tabia za muumini wa kike, akichukia tabia fulani basi ataridhishwa na tabia nyingine" Au alisema: "Tabia tofauti na hiyo"
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake mume kumchukia sana mke wake hadi kupelekea dhulma, na kumuacha na kumtelekeza; Mwanadamu ana asili ya kutokamilika, na ikiwa atachukia kwake tabia moja mbaya, basi atapata tabia nyingine nzuri; ataridhia kwa tabia hiyo nzuri anayoikubali, na avumilie kwa tabia asizozipenda miongoni mwa tabia mbaya, ambazo humfanya awe mvumilivu na asimchukie kiasi cha kutaka kumuacha.

Mafunzo
  1. Huu ni wito kwa muumini wa kuja katika haki na uadilifu, na kuhukumu mambo kwa akili katika mgogoro wowote unaotokea baina yake na mke wake, na sio kutoa maamuzi kwa hisia na mihemuko ya muda mfupi.
  2. Kazi ya muumini si kumchukia mwanamke muumini kabisa mpaka afikie kuachana naye, bali apuuze kile anachochukia kwa kile anachopenda.
  3. Himizo la kuishi vizuri na kutengeneza urafiki kati ya wanandoa.
  4. Imani ni msukumo wa maadili mema, hivyo hakuna muumini wa kiume au wa kike asiye na tabia njema; Imani inachochea uwepo wa sifa njema ndani yao.
Marejeo

صحيح مسلم (2/ 1091) (1469). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 359). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 122). فتح رب البرية بتلخيص الحموية، لابن عثيمين (ص117). مجموع فتاوى ابن باز (25/ 246). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 282).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Ukipenda unaweza kuvumulia na utapata malipo ya Pepo, na ukitaka nitakuombea kwa Mwenyezi Mungu akuponye

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رضيَ اللهُ عنهما: أنَّهُ قَالَ لعَطَاءِ بْنِ أَبِي رَبَاحٍ: أَلَا أُرِيكَ امْرَأَةً مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ؟ قُلْتُ: بَلَى، قَالَ: هَذِهِ الْمَرْأَةُ السَّوْدَاءُ، أَتَتِ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، قَالَتْ: إِنِّي أُصْرَعُ وَإِنِّي أَتَكَشَّفُ، فَادْعُ اللهَ لِي، قَالَ: «إِنْ شِئْتِ صَبَرْتِ وَلَكِ الْجَنَّةُ، وَإِنْ شِئْتِ دَعَوْتُ اللهَ أَنْ يُعَافِيَكِ» قَالَتْ: أَصْبِرُ، قَالَتْ: فَإِنِّي أَتَكَشَّفُ فَادْعُ اللهَ أَنْ لَا أَتَكَشَّفَ، فَدَعَا لَهَا.
Kutoka kwa bin Abbasi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, yeye na baba yake: Ya kwamba pindi aliposema kumwambia Atwaa bin Abii Rabaahi: Hivi je, nikuonyeshe mwanamke miongoni mwa wanawake wa Peponi? Nikasema: Ndio, akasema: Huyu mwanamke mweusi, alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Hakika mimi huanguka, na nguo zangu hufunuka ninapoanguka, nakuomba uniombee kwa Mwenyezi Mungu, akasema: "Ukipenda unaweza kuvumulia na utapata malipo ya Pepo, na ukitaka nitakuombea kwa Mwenyezi Mungu akuponye" Akasema: Bali nitavumilia, akasema: Lakini mimi huwa nafunuka nguo, basi niombee kwa Mwenyezi Mungu nisifunuke, basi akamuombea.
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alisema bin Abbasi Mwenyezi Mungu amuwie radhi kumwambia Atwaa bin Abii Rabaahi: Je, nikuonyeshe mwanamke miongoni mwa watu wa Peponi? Atwaa akasema: Ndio, akasema: Huyu mwanamke muethiopia mweusi, alikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake: akasema: Hakika mimi nina maradhi, huanguka na kufunuka nguo zangu, na kuonekana sehemu ya mwili wangu pasina mimi kujielewa, basi muombe Mwenyezi Mungu aniponye, akasema: Ukipenda unaweza kuvumilia na utakuwa na malipo ya Pepo, na ukipenda nitamuomba Mwenyezi Mungu akuponye, akasema: Basi nitavumilia, kisha akasema: Basi niombee kwa Mwenyezi Mungu nisifunuke nikianguka, basi akamuombea kwa Mwenyezi Mungu.

Mafunzo
  1. Subira juu ya mabalaa katika dunia hupelekea kupata Pepo.
  2. Amesema Nawawi: Na hapa kuna ushahidi kuwa ugonjwa wa kuanguka kwa mtu hulipwa malipo yaliyokamilika
  3. Tazama heshima na haya kwa wanawake wa kiswahaba, na pupa yao juu ya kujisitiri, radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, mwanamke huyu, kubwa zaidi alilokuwa akilihofia ni kufunuka sehemu ya mwili wake.
  4. Amesema bin Hajari: Kuchukua jambo gumu ni bora kuliko kuchukua ruhusa, kwa mtu atakayejua kuwa anauwezo wa kulibeba, na hatodhoofika kwa kulibeba gumu hilo.
  5. Amesema bin Hajari: Na hapa nikuwa; tiba ya maradhi yote ni kwa dua na kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, hufaa zaidi na kunufaisha zaidi kuliko tiba ya miti shamba (madawa), na kwamba athari ya hilo na muitikio wa mwili ni mkubwa zaidi kuliko athari ya dawa za mwili, lakini huleta ahueni kwa mambo mawili: La kwanza: Upande wa mgonjwa, kuwa na imani ya kweli na Mwenyezi Mungu, na la pili: Upande wa tabibu, kuwa na nguvu kubwa ya kuelekea kwa Mwenyezi Mungu, na kuwa na nguvu kubwa ya uchamungu, na kumtegemea Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu Ndiye Mjuzi zaidi.
  6. Amesema bin Hajari: Hapa kuna ushahidi juu ya kuacha kutumia dawa.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 116) (5652). صحيح مسلم (4/ 1994) (2576). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 95). شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (1/ 235).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Dunia ni starehe, na starehe yake bora ni mke mwema

عن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «الدُّنْيَا مَتَاعٌ، وَخَيْرُ مَتَاعِ الدُّنْيَا الْمَرْأَةُ الصَّالِحَةُ».
Imepokewa kutoka kwa Abdallah Ibn Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Dunia ni starehe, na starehe yake bora ni mke mwema".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Dunia na vyote vilivyomo si kingine isipokuwa ni kitu cha kustarehe nacho kwa muda mchache kisha kinaondoka, nakuwa starehe yake bora ni mke mwema, ambaye akimtazama anamfurahisha, na akimuamrisha anamtii, na akiwa mbali naye humuhifadhi ndani ya nafsi yake na mali yake.

Mafunzo
  1. Inafaa kustarehe na vizuri vya Dunia alivyovihalalisha Mwenyezi Mungu kwa waja wake bila kupita kiasi au kujikweza.
  2. Himizo la kuchagua mke mwema; kwa sababu ni msaada kwa mume katika kumtii Mola wake Mlezi.
  3. Starehe bora ya Dunia ni ile itakayokuwa katika kumtii Allah au ikasaidia katika hilo.
Marejeo

صحيح مسلم (2/ 1090) (1467). بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 365). كشف المشكل من حديث الصحيحين، لابن الجوزي (4/ 129). نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخن وغيره (1/ 286).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Tahadharini sana na kuingia/kukaa kwa wanawake" Mtu mmoja katika Maanswari akasema: Ewe Mtume wa Allah vipi kuhusu shemeji? Akasema: "Shemeji ni kifo

عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «إِيَّاكُمْ وَالدُّخُولَ عَلَى النِّسَاءِ» فَقَالَ رَجُلٌ مِنَ الأَنْصَارِ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَفَرَأَيْتَ الحَمْوَ؟ قَالَ: «الحَمْوُ المَوْتُ».
Imepokelewa kutoka kwa Uqbah bin Aamir -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake: "Tahadharini sana na kuingia/kukaa kwa wanawake" Mtu mmoja katika Maanswari akasema: Ewe Mtume wa Allah vipi kuhusu shemeji? Akasema: "Shemeji ni kifo".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala la kuchanganyikana na wanawake wa kando, na akasema: Jiepusheni sana kuingia kwa wanawake, na wanawake watahadhari kuingia kwa wanaume. Akasema mtu mmoja miongoni mwa Manswari (watu wa Madina): Wasemaje kuhusu ndugu wa karibu wa mume; kama kaka wa mume na mtoto wa kaka yake, na ami yake na mtoto wa ami yake, na kijana wa dada yake, na mfano wa hao katika wale wa halali kwao kumuoa akiwa hajaolewa? Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Mtahadharini kama mnavyokitahadhari kifo! Kwa sababu kukaa faragha na mashemeji kunapelekea fitina na maangamivu katika dini, ndugu wa mume wasiokuwa baba zake na wanawe, hawa wanatakiwa zaidi kuzuiliwa kuliko hata mtu wa kando; kwa sababu kukaa faragha na ndugu wa mume ni zaidi ya kukaa faragha na mtu mwingine, na shari iko karibu zaidi kwake kutokea kuliko hata kwa asiyekuwa yeye, na kuna uwezekano mkubwa wa kutokea; kwa sababu anauwezekano mkubwa wa kumfikia mwanamke na kukaa naye faragha pasina mtu wa kuwakemea, na ni kwa sababu hana budi lazima aonane naye kwakuwa ni ndugu wa mume, na ni vigumu kumzuia, kwa sababu tamaduni za watu zimezoeleka kulipuuza hilo, mtu akakaa faragha na mke wa kaka yake; hivyo anafanana na kifo katika ubaya na madhara, tofauti na mwanaume wa kando kwani huyo watu humtahadhari.

Mafunzo
  1. Katazo la kuingia kwa wanawake wa kando na kukaanao faragha, kwa ajili ya kuziba njia zinazopelekea kuingia katika uchafu.
  2. Katazo hilo ni kwa watu wa kando wote kwanzia kaka wa mume na ndugu zake wa karibu, ambao si haramu kwao kumuoa mwanamke, hivyo ni lazima kuchunguza ili kujua kama kuingia kwake kunapelekea kuwa faragha.
  3. Kujiweka mbali na maeneo yote ya kuteleza, kwa kuhofia kuingia katika shari.
  4. Amesema Imam Nawawi: Wamekubaliana wasomi wote wa Lugha ya kiarabu kuwa maana ya mashemeji ni ndugu wa karibu wa mume, kama baba yake na ami yake, na kaka yake, na mtoto wa kaka yake, na mtoto wa ami yake na mfano wao, nakuwa wakwe ni ndugu wa karibu wa mume, nakuwa wakwe wanakuwa kwa aina zote mbili.
  5. Ameufananisha ushemeji na kifo, amesema bin Hajari: Na waarabu hukifananisha kitu chenye kuchukiza na kifo, na namna ya kufanana kwake nikuwa ni kifo cha dini yakitokea maasi, na ni kifo cha mambo yote endapo yatatokea maasi kwani itakuwa wajibu kupigwa mawe, na ni kifo cha mwanamke kwa kuachana na mumewe endapo wivu utampelekea kumpa talaka.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 37) (5232). صحيح مسلم (4/ 1711) (2172). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (2/ 69). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، لعبد الله البسام (ص589).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Enyi hadhara ya wanawake, toeni sadaka, kwani hakika mimi nilionyeshwa kuwa nyinyi ndio wengi katika watu wa motoni" Wanawake wakasema: Na ni kwa nini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Mnazidisha sana kulaani (kutukana) na mnawapinga waume, na mimi sijapata kuona wapungufu wa akili na dini wenye kuweza kuteka moyo ya mwanaume makini kuliko nyinyi

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيِّ رضي الله عنه قَالَ: خَرَجَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي أَضْحَى أَوْ فِطْرٍ إِلَى المُصَلَّى، فَمَرَّ عَلَى النِّسَاءِ، فَقَالَ: «يَا مَعْشَرَ النِّسَاءِ، تَصَدَّقْنَ، فَإِنِّي أُرِيتُكُنَّ أَكْثَرَ أَهْلِ النَّارِ» فَقُلْنَ: وَبِمَ يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: «تُكْثِرْنَ اللَّعْنَ، وَتَكْفُرْنَ العَشِيرَ، مَا رَأَيْتُ مِنْ نَاقِصَاتِ عَقْلٍ وَدِينٍ أَذْهَبَ لِلُبِّ الرَّجُلِ الحَازِمِ مِنْ إِحْدَاكُنَّ»، قُلْنَ: وَمَا نُقْصَانُ دِينِنَا وَعَقْلِنَا يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: «أَلَيْسَ شَهَادَةُ المَرْأَةِ مِثْلَ نِصْفِ شَهَادَةِ الرَّجُلِ» قُلْنَ: بَلَى، قَالَ: «فَذَلِكِ مِنْ نُقْصَانِ عَقْلِهَا، أَلَيْسَ إِذَا حَاضَتْ لَمْ تُصَلِّ وَلَمْ تَصُمْ» قُلْنَ: بَلَى، قَالَ: «فَذَلِكِ مِنْ نُقْصَانِ دِينِهَا».
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alitoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika swala ya Idil Adhaa au Fitri kwenda katika uwanja wa kuswali, akapita kwa wanawake, akasema: "Enyi hadhara ya wanawake, toeni sadaka, kwani hakika mimi nilionyeshwa kuwa nyinyi ndio wengi katika watu wa motoni" Wanawake wakasema: Na ni kwa nini ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Mnazidisha sana kulaani (kutukana) na mnawapinga waume, na mimi sijapata kuona wapungufu wa akili na dini wenye kuweza kuteka moyo ya mwanaume makini kuliko nyinyi", Wakasema: Na ni upi upungufu wa dini yetu na akili zetu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Hivi kwani si ushahidi wa mwanamke mmoja ni sawa na ushahidi nusu wa mwanaume?" Wakasema: Ndivyo, akasema: "Hilo ni katika upungufu wa akili yake, na je hivi akiingia katika hedhi si haswali wala hafungi" Wakasema: Ndivyo, akasema: "Basi hilo ni katika upungufu wa dini yake".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Alitoka Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika siku ya Iddi kwenda katika uwanja wa swala, na alikuwa kawaahidi wanawake kuwa atawatengea nafasi ya kuwapa mawaidha, akaitimiza siku hizo, na akasema: Enyi kundi la wanawake toeni sadaka, na zidishe kuomba msamaha; kwani mambo mawili hayo ni katika sababu kubwa za kufutiwa madhambi, kwani mimi nilikuoneni usiku niliopandishwa mbinguni mkiwa wengi motoni. Mwanamke mmoja miongoni mwao mwenye akili na mawazo mazuri na heshima, akasema: Kwani tuna nini sisi ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu mpaka tuwe wengi motoni? Akasema: Kwa sababu ya mambo kadhaa: Mnazidisha sana kulaani na matusi, na mnakanusha haki za waume. Kisha akawasifu kwa kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: Sijapata kuona wenye mapungufu ya akili na dini wanaoweza kuwashinda wenye mioyo salama na akili na maamuzi na uwezo wa kutunza kumbukumbu zao kuliko nyinyi. Akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na ni upi upungufu wa akili na dini? Akasema: Ama upungufu wa akili ni kuwa ushahidi wa wanawake wawili unalingana na ushahidi wa mwanaume mmoja; huu ndio upungufu wa akili, na upungufu wa dini, ni upungufu wa kufanya amali njema, kiasi ambacho mwanamke anakaa siku kadhaa haswali kwa sababu ya hedhi, na anafungua siku kadhaa za Ramadhani kwa sababu ya hedhi, na huu ndio upungufu wa dini, isipokuwa wao hawalaumiwi wala hawaandikiwi dhambi juu ya hilo; kwa sababu ni katika asili ya maumbile, kama ambavyo mwanadamu ameumbwa na asili ya kuipenda mali, na haraka katika mambo yake na ni mjinga.... na mengineyo, lakini alilitanabahisha hilo ikiwa ni tahadhari kwa wanaume wasifitinike nao.

Mafunzo
  1. Sunna kwa wanawake kutoka kwenda katika swala ya Iddi, na watengewe muda wa mawaidha.
  2. Kuwapinga waume na kukithirisha laana ni katika madhambi makubwa; kwa sababu kuahidiwa moto ni katika alama za dhambi kuwa katika madhambi makubwa.
  3. Hapa kumebainishwa kuzidi kwa imani na kupungua kwake, yatakayekithiri matendo yake, basi imani yake na dini yake vitazidi, na zitakayepungua ibada zake dini yake itapungua.
  4. Amesema Imam Nawawi: Akili inakubali kuzidi na kupungua, na vile vile imani, na si makusudio ya kutajwa mapungufu kwa wanawake ni kuwalaumu kwa hilo; kwa sababu hilo ni katika asili ya maumbile, lakini tanbihi katika hilo ni kutahadharisha kutofitinika nao, na ndio maana amepanga adhabu kwa yale yaliyotajwa ikiwemo kuwapinga waume na mengineyo na si katika mapungufu, na mapungufu ya dini hayaishii tu katika madhambi bali ni zaidi ya hayo.
  5. Hapa kuna swala la mwanafunzi kumrejea mwalimu, na mfuasi kumrejea anayemfuata katika yale ambayo kwake maana haijawa wazi.
  6. Ndani ya hadithi kumeelezwa kuwa ushahidi wa mwanamke mmoja ni nusu ya ushahidi wa mwanaume mmoja, na hii ni kwa sababu ya upungufu wa kumbukumbu zake.
  7. Amesema bin Hajari katika kauli yake: "Sijapata kuona wapungufu...mpaka mwisho" Kinachodhihiri kwangu nikuwa, hili ni miongoni mwa sababu za kuwa kwao wengi motoni; kwa sababu wao wakiwa sababu ya kuondoa akili ya mwanaume shupavu mpaka akafikia kufanya au kusema maneno yasiyofaa watakuwa wameshirikiana naye katika madhambi na tena wamemzidi.
  8. Uharamu wa swala na swaumu kwa mwanamke wakati wa hedhi yake, na mfano huo huo kwa mwenye nifasi, kisha watalipa swaumu pekee watakapokuwa twahara.
  9. Uzuri wa tabia ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kwani aliwajibu wanawake maswali yao pasina ukali wala kuwalaumu.
  10. Amesema bin Hajari: Nikuwa sadaka inazuia adhabu, nakuwa inafuta makosa yaliyoko baina ya viumbe.
  11. Amesema Nawawi: Upungufu wa dini kwa wanawake kwa sababu ya kuacha kwao swala na swaumu katika wakati wa hedhi; kwa sababu zitakayekithiri ibada zake basi itaongezeka imani yake na dini yake, na zitakayepungua ibada zake itapungua dini yake, kisha upungufu wa dini unaweza kuwa katika sura ambayo anapata dhambi, kama atakayeacha swala au swaumu au mengineyo katika ibada za wajibu juu yake pasina udhuru, na inaweza kuwa katika sura ambayo hapati madhambi, kama atakayeacha swala ya Ijumaa au kwenda vitani au mengineyo ambayo si wajibu juu yake pasina udhuru, na inaweza kuwa katika sura ambayo yeye ndiye kalazimishwa kwa hilo, kama mwenye hedhi kuacha swala na swaumu.
Marejeo

صحيح البخاري (1/ 68) (304). صحيح مسلم (2/ 605) (889). إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري، لأحمد القسطلاني (1/ 346). مرقاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعلي القاري (1/ 92). مرعاة المفاتيح شرح مشكاة المصابيح، لعبيد الله المباركفوري (1/ 80). فتح الباري شرح صحيح البخاري، لابن رجب (2/ 39). المنهاج شرح صحيح مسلم، للنووي (2/ 65). شرح صحيح البخاري، لابن بطال (1/ 418). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، لعبد الله البسام (3/ 405). منار القاري، لحمزة قاسم (1/ 329).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Asisafiri mwanamke mwendo wa siku mbili mpaka awe pamoja na mume wake, au maharimu yake

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيَّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ -وَكَانَ غَزَا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ ثِنْتَيْ عَشْرَةَ غَزْوَةً- قَالَ: سَمِعْتُ أَرْبَعًا مِنَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَأَعْجَبْنَنِي، قَالَ: «لاَ تُسَافِرِ المَرْأَةُ مَسِيرَةَ يَوْمَيْنِ إِلَّا وَمَعَهَا زَوْجُهَا أَوْ ذُو مَحْرَمٍ، وَلاَ صَوْمَ فِي يَوْمَيْنِ: الفِطْرِ وَالأَضْحَى، وَلاَ صَلاَةَ بَعْدَ الصُّبْحِ حَتَّى تَطْلُعَ الشَّمْسُ، وَلاَ بَعْدَ العَصْرِ حَتَّى تَغْرُبَ، وَلاَ تُشَدُّ الرِّحَالُ إِلَّا إِلَى ثَلاَثَةِ مَسَاجِدَ: مَسْجِدِ الحَرَامِ، وَمَسْجِدِ الأَقْصَى، وَمَسْجِدِي هَذَا».
Kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudri radhi za Allah ziwe juu yake na alikuwa kapigana vita pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- takriban vita kumi na mbili (12) anasema: Nilisikia mambo manne kutoka Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, yakanifurahisha sana, anasema: "Asisafiri mwanamke mwendo wa siku mbili mpaka awe pamoja na mume wake, au maharimu yake (Ndugu asiyeweza kumuoa), hakuna kufunga ndani ya siku mbili: Idil Fitri na Idil Adh-ha, na hakuna swala baada swala ya Asubuhi mpaka lichomoze jua, na wala baada ya Lasiri mpaka lizame, na wala haifungwi safari isipokuwa katika misikiti mitatu: Msikiti mtukufu (wa Makka), na Msikiti wa Aqswa (Palestina), na msikiti wangu huu (Madina)".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Amekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mambo manne: La kwanza: Kamkataza mwanamke kusafiri mwendo wa siku mbili bila kuwa na mume wake au mmoja kati ya maharimu wake, naye ni mtu aliyeharamu kwake kumuoa uharamu wa moja kwa moja (usio wa moja kwa moja, kama mume wa dada yake) kama mwanaye, na baba, na mtoto wa kaka, na kijana wa dada, na baba mdogo au mkubwa, na mjomba, na mfano wake. La pili: Katazo la kufunga siku Idil Fitri na siku ya Idil Adh-ha, sawa sawa muislamu amezifunga kwa udhuru au kwa kujitolea, au kafara. La tatu: Amekataza kusali swala ya sunna baada ya swala ya Lasiri mpaka lizame Jua, na baada ya kuchomoza asubuhi mpaka lichomoze Jua. La nne: Katazo la kusafiri kwenda eneo katika maeneo kwa itikadi kuwa kuna ubora, na kuitakidi kuwa kuna kulipwa malipo mengi, isipokuwa misikiti hii mitatu, hivyo hakuna kufunga safari kwenda misikiti isiyokuwa hiyo kwa ajili kuswali ndani yake, kwani malipo hayalipwi kwa wingi isipokuwa katika misikiti hii mitatu, Msikiti mtukufu (wa Makka), na Msikiti wa Mtume (Madina), na Msikiti wa Aqswa (Palestina).

Mafunzo
  1. Haifai kwa mwanamke kusafiri bila maharim.
  2. Mwanamke hawezi kuwa maharim wa mwanamke mwenzie katika safari; kwa kauli yake: "Mume wake, au aliyeharamu kwake kumuoa (Maharim)"
  3. Kila inayoitwa safari basi mwanamke anakatazwa kusafiri bila mume wake au maharim yake, na hadithi ilikuwa kulinga na hali ya muulizaji na mji wake.
  4. Maharim wa mwanamke ni mume wake au aliyeharamu kwake kumuoa kwa uharamu wa moja kwa moja, kwa sababu ya udugu wa damu, kama baba na mtoto na baba mdogo au mkubwa na mjomba, au kwa kunyonya, kama baba wa kunyonya au baba mdogo wa kunyonya, au ukwe kama baba mkwe, na anatakiwa awe muislamu aliyebaleghe, mwaminifu, kwani lengo la maharim ni kumlinda mwanamke na kumchunga na kumjali katika mambo yake.
  5. Sheria imempa kipaumbele mwanamke, na imemhami na kumlinda.
  6. Haikubaliki swala ya sunna isiyokuwa na sababu, baada ya swala ya Alfajiri na Lasiri, na haingii hapa kulipa swala ya faradhi iliyopita, na zenye sababu, kama salamu ya msikiti na mfano wake.
  7. Uharamu wa kusali mara tu baada ya kuchomoza Jua, bali ni lazima linyanyuke kiasi cha mkuki, kwa takribani kama dakika kumi (10) mpaka robo saa hivi.
  8. Wakati wa Lasiri unakwenda mpaka kuzama Jua.
  9. Ndani ya hadithi kuna kufaa kufunga safari kwenda katika misikiti mitatu.
  10. Fadhila na ubora wa misikiti mitatu, na tofauti yake kwa misikiti mingine.
  11. Hairuhusiwi kusafiri kwenda kufanya ziara ya makaburi, hata kama ni kaburi la Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, ila inafaa kulitembelea kwa anayeishi Madina, au akalifikia kwa lengo la kisheria au lengo linalofaa.
Marejeo

صحيح البخاري (3/ 43) (1995). صحيح مسلم (2/ 975) (827). فتح الباري شرح صحيح البخاري، لابن حجر العسقلاني (4/ 75). توضيح الأحكام مِن بلوغ المرام، للبسام (3/ 544). فتح ذي الجلال والإكرام شرح بلوغ المرام، لابن عثيمين (3/ 311). سبل السلام، لمحمد الصنعاني (1/ 598). مجموع فتاوى ومقالات، لابن باز(6/ 321). الشرح الممتع على زاد المستقنع، لابن عثيمين (6/ 516). شرح سنن أبي داود، عبد المحسن العباد (65/ 8 بترقيم الشاملة آليا).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com