عَنِ الأَسْوَدِ بنِ يَزِيدَ قَالَ: سَأَلْتُ عَائِشَةَ مَا كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَصْنَعُ فِي بَيْتِهِ؟ قَالَتْ: كَانَ يَكُونُ فِي مِهْنَةِ أَهْلِهِ -تَعْنِي خِدْمَةَ أَهْلِهِ-، فَإِذَا حَضَرَتِ الصَّلاَةُ خَرَجَ إِلَى الصَّلاَةِ.
Kutoka kwa Aswadi bin Yadizi amesema: Nilimuuliza Aisha, nini alikuwa akifanya Mtume rehema na amani ziwe juu yake nyumbani kwake? Akasema: Alikuwa akishiriki katika kazi za familia yake (anakusudia kuhudumia familia yake), unapofika wakati wa swala anatoka kwenda katika swala.
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Aliulizwa mama wa Waumini Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake kuhusu hali ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake nyumbani kwake, na alikuwa akifanya nini? Akasema: Alikuwa ni mtu kama watu wengine, na anafanya wanayofanya wanaume katika majumba yao, anashughulika na kujihudumia yeye na familia yake; anakamua mbuzi wake mwenyewe, na anashona nguo yake, na anashona kiatu chake, na anatengeneza ndoo yake, na ulikuwa unapofikia wakati wa kusimamishwa swala anatoka kwa ajili yakusali rehema na amani ziwe juu yake bila kuchelewa.
Mafunzo
- Ukamilifu wa unyenyekevu wake rehema na amani ziwe juu yake na wema wake kwa familia yake.
- Amali za kidunia hazitakiwi kumshughulisha mja akawacha swala.
- Kuhifadhi kwake Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala, mwanzo wa wakati wake.
- Amesema bin Hajari: Na hapa kunahimizo la kuwa mnyenyekevu na kuacha kiburi na mwanaume kuihudumia familia yake.
Marejeo
صحيح البخاري (1/ 136) (676).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 660).
شرح رياض الصالحين، لابن عثيمين (3/ 526).
شرح صحيح البخاري، لابن بطال (2/ 296).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمجموعة من الباحثين (1/ 516).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.comعَنْ أُمَيْمَةَ بِنْتِ رُقَيْقَةَ رضي الله عنها أَنَّهَا قَالَتْ: أَتَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي نِسْوَةٍ مِنَ الْأَنْصَارِ نُبَايِعُهُ، فَقُلْنَا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، نُبَايِعُكَ عَلَى أَلَّا نُشْرِكَ بِاللَّهِ شَيْئًا، وَلَا نَسْرِقَ، وَلَا نَزْنِيَ، وَلَا نَأْتِيَ بِبُهْتَانٍ نَفْتَرِيهِ بَيْنَ أَيْدِينَا وَأَرْجُلِنَا، وَلَا نَعْصِيَكَ فِي مَعْرُوفٍ، قَالَ: «فِيمَا اسْتَطَعْتُنَّ، وَأَطَقْتُنَّ» قَالَتْ: قُلْنَا اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَرْحَمُ بِنَا، هَلُمَّ نُبَايِعْكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «إِنِّي لَا أُصَافِحُ النِّسَاءَ، إِنَّمَا قَوْلِي لِمِائَةِ امْرَأَةٍ كَقَوْلِي لِامْرَأَةٍ وَاحِدَةٍ، أَوْ مِثْلُ قَوْلِي لِامْرَأَةٍ وَاحِدَةٍ».
Kutoka kwa Umaima binti Ruqaiqa radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba yeye alisema: Nilikuja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa katika kundi la wanawake ili wampe ahadi ya utiifu (Baiaa) wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tunakupa ahadi juu ya kutomshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na tusizini, na tusilete uzushi tutakaouzua mbele ya mikono yetu na miguu, na wala tusikuasi katika jema lolote, akasema: "Katika yale mnayoyaweza, na mkayahimili" Anasema: Tukasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wanahuruma zaidi kwetu, njoo tukupe ahadi ya utiifu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika mimi siwapi mkono wanawake, bali hakika kauli yangu kwa wanawake mia moja ni sawa na kauli yangu kwa mwanamke mmoja, au ni mfano wa kauli yangu kwa mwanamke mmoja".
Imepokelewa na Tirmidhiy, Nasai na Ibn MajahDarajaSahihi
Maelezo
Ameeleza Umaima binti Ruqaiqa radhi za Allah ziwe juu yake: Ya kwamba yeye alimuendea Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa pamoja na wanawake wa ki Answari (watu wa Madina) wampe ahadi ya utiifu juu ya kutomshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na wala wasiibe, na wala wasizini, na wala wasilete uzushi watakaouzua mbele ya mikono yao na miguu yao, na wala wasimuasi katika jema lolote, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Katika yale mnayoyaweza, na mkayamudu. Tukasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wanahuruma zaidi kweli, njoo tukupe ahadi ya utiifu ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwa kukupa mkono kama wanavyofanya wanaume, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hakika mimi siwapi mkono wanawake, bali kauli yangu na kukubali kwangu kuungwa mkono na wanawake mia moja ni sawa na kauli yangu kwa mwanamke mmoja.
Mafunzo
- Kumebainishwa namna ya kumpa ahadi ya utiifu Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa wanawake.
- Uharamu wa kuwapa mkono wanawake wasiokuwa ndugu walioharamishwa kuwaoa.
- Majukumu ya kisheria yamefungamanishwa na uwezo na kumudu.
Marejeo
سنن الترمذي (3/ 247) (1597).
سنن النسائي (7/ 149) (4181).
سنن ابن ماجه (4/ 128) (2874).
ذخيرة العقبى في شرح المجتبى (32/ 263).
Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com