Dunia ni starehe, na starehe yake bora ni mke mwema
عن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «الدُّنْيَا مَتَاعٌ، وَخَيْرُ مَتَاعِ الدُّنْيَا الْمَرْأَةُ الصَّالِحَةُ».
Imepokewa kutoka kwa Abdallah Ibn Amri -Radhi za Allah ziwe juu yao wawili- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Dunia ni starehe, na starehe yake bora ni mke mwema".
Imepokelewa Imamu MuslimDarajaSahihi
Maelezo
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Dunia na vyote vilivyomo si kingine isipokuwa ni kitu cha kustarehe nacho kwa muda mchache kisha kinaondoka, nakuwa starehe yake bora ni mke mwema, ambaye akimtazama anamfurahisha, na akimuamrisha anamtii, na akiwa mbali naye humuhifadhi ndani ya nafsi yake na mali yake.
Mafunzo
Inafaa kustarehe na vizuri vya Dunia alivyovihalalisha Mwenyezi Mungu kwa waja wake bila kupita kiasi au kujikweza.
Himizo la kuchagua mke mwema; kwa sababu ni msaada kwa mume katika kumtii Mola wake Mlezi.
Starehe bora ya Dunia ni ile itakayokuwa katika kumtii Allah au ikasaidia katika hilo.
Marejeo
صحيح مسلم (2/ 1090) (1467).
بهجة الناظرين شرح رياض الصالحين، لسليم الهلالي (1/ 365).
كشف المشكل من حديث الصحيحين، لابن الجوزي (4/ 129).
نزهة المتقين شرح رياض الصالحين، لمصطفى الخن وغيره (1/ 286).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com