Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Yakuwa aliulizwa kuhusu kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake

عَنِ ابْنِ أَبِي مُلَيْكَةَ: عَنْ بَعْضِ أَزْوَاجِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ -قَالَ: أَبُو عَامِرٍ، قَالَ نَافِعٌ: أُرَاهَا حَفْصَةَ- أَنَّهَا سُئِلَتْ عَنْ قِرَاءَةِ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَتْ: إِنَّكُمْ لَا تَسْتَطِيعُونَهَا قَالَ: فَقِيلَ لَهَا أَخْبِرِينَا بِهَا. قَالَ: فَقَرَأَتْ قِرَاءَةً تَرَسَّلَتْ فِيهَا قَالَ أَبُو عَامِرٍ: قَالَ نَافِعٌ: فَحَكَى لَنَا ابْنُ أَبِي مُلَيْكَةَ {الحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ} [الفاتحة: 2] ثُمَّ قَطَّعَ {الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ} [الفاتحة: 1] ثُمَّ قَطَّعَ {مَالِكِ يَوْمِ الدِّينِ}.
Kutoka kwa Abuu Mulaika: Kutoka kwa baadhi ya wake za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amesema: Abuu Aamir, amesema Naafii: Nafikiri ni Hafswa -Yakuwa aliulizwa kuhusu kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Hakika nyinyi hamkiwezi, akasema: Akaambiwa hebu tueleze. Akasema: Akasoma kisomo cha taratibu, akasema Abuu Aamiri: Akasema Naafii: Akatusimulia Abuu Mulaika: "Alhamdulillaah Rabbil-Aalamiin" [Al-Faatiha: 1] Kisha akakata "Al Rahmaanir Rahiim" [Faatiha:3] kisha akakata "Maaliki yaumid diin".
Imepokelewa na AhmadDarajaSahihi
Maelezo

Aliulizwa Hafswa mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Kilikuwa vipi kisomo cha Qur'ani cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake? Akasema: Hakika nyinyi hamkiwezi mfano wake, akaambiwa: Tueleze. Amesema Naafii: Akatusomea Abuu Mulaika kisomo alichotulizana ndani yake; ili kielezee na kikaribiane na kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasoma: "Alhamdulillaahi Rabbil Aalamiin" kisha akakata kisomo, "Al Rahmaanir Rahiim", kisha akakata kisomo, "Maaliki yaumid diin".

Mafunzo
  1. Kumebainishwa muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kusoma Qur'ani.
  2. Kufanya kwa vitendo ili kubainisha namna ya kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  3. Sheria ya kwenda taratibu katika kuisoma Qur'ani, hilo huleta msukumo wa kuizingatia.
  4. Kuitilia maanani Qur'ani wema waliotangulia, na matendo ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  5. Umuhimu wa kujua kanuni za kuisoma Qur'ani (Tajwidi) na elimu za Qur'ani.
Marejeo

مسند أحمد (44/ 70) (26470). الفتح الرباني لترتيب مسند أحمد الشيباني (3/237).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Elimu ya Tajwiid.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com