عَنْ قَتَادَةَ قَالَ: سُئِلَ أَنَسٌ كَيْفَ كَانَتْ قِرَاءَةُ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؟ فَقَالَ: «كَانَتْ مَدًّا»، ثُمَّ قَرَأَ: {بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ} [الفاتحة: 1] يَمُدُّ بِبِسْمِ اللَّهِ، وَيَمُدُّ بِالرَّحْمَنِ، وَيَمُدُّ بِالرَّحِيمِ.
Kutoka kwa Katada amesema: Aliulizwa Anasi kilikuwa vipi kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake? Akasema: "Kilikuwa ni kuvuta", kisha akasoma: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu" [Al-Faatiha:1] Alikuwa akivuta neno: Bismillaahi, na anavuta Al-Rahmaani, na anavuta neno: Al-Rahiim.
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Aliulizwa Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake kilikuwa vipi kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika Qur'ani? Akasema: Alikuwa akivuta sauti yake kwa kisomo; akivuta herufi Lamu ilioko kabla ya "Haa" katika neno: "Allah", na anavuta herufi "Mim" ilioko kabla ya "Nuun" katika neno "Al-Rahmaan", na anavuta herufi "Haa" katika neno "Al-Rahiim".
Mafunzo
- Kuvuta ni kuzishibisha herufi za mada nazo ni (Alif, Wau, Yaa) zinapokuwa na sakina na kabla yake kukawa haraka (silabi) inayoendana nayo.
- Kumebainishwa muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kuisoma Qur'ani.
- Kutekeleza kwa vitendo kwa ajili ya kubainisha kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
- Amesema Assindi: Kauli yake: "Akivuta sauti yake", yaani anarefusha herufi zinazofaa kurefushwa kwa kuzitumia kuzingatia na kutafakari na kumkumbusha mwenye kukumbuka.
- Umuhimu wa kujua kanuni za kusoma Qur'ani (Tajwidi) na elimu za Qur'ani.
- Kuzielewa dalili kunarejeshwa kwa wanachuoni, kama alivyoulizwa Anasi radhi za Allah ziwe juu yake akambainishi muulizaji.
Marejeo
صحيح البخاري (6/ 195) (5046). عمدة القاري (20/55).