Imepokelewa kutoka kwa Abuu Abdulrahman Al-Sulamiy- Mwenyezi Mungu amrehemu amesema: Ametusimulia mmoja miongoni mwa waliokuwa wakitusomea Qur'ani katika Maswahaba wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- walikuwa wakitusomea Aya kumi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, hivyo hawakuwa wakichukua Aya kumi zingine mpaka wawe wamekwishayafanyia kazi yaliyo ndani ya aya hizo kumi kwa kujifunza na kuyafanyia kazi, wakasema: Basi tukajifunza elimu na kuifanyia kazi.
Imepokelewa na AhmadDarajaNi nzuri (Hasan)
Maelezo
Walikuwa Maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- wakipokea Aya kumi kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na hawakuwa wakihama kwenda Aya zingine mpaka wawe wamekwishajifunza elimu liyopo kwenye hizo Aya kumi, na wanazifanyia kazi, hivyo wakajifunza elimu pamoja na kuifanyia kazi.
Mafunzo
Ubora wa Maswahaba -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, na pupa yao ya kujifunza Qur'ani.
Kujifunza Qur'ani kunakuwa kwa kujifunza na kufanyia kazi yaliyopo ndani yake na kuyafanyia kazi, na siyo kuisoma na kuihifadhi peke yake.
Kutoka kwa Katada amesema: Aliulizwa Anasi kilikuwa vipi kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake? Akasema: "Kilikuwa ni kuvuta", kisha akasoma: "Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu" [Al-Faatiha:1] Alikuwa akivuta neno: Bismillaahi, na anavuta Al-Rahmaani, na anavuta neno: Al-Rahiim.
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo
Aliulizwa Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake kilikuwa vipi kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika Qur'ani? Akasema: Alikuwa akivuta sauti yake kwa kisomo; akivuta herufi Lamu ilioko kabla ya "Haa" katika neno: "Allah", na anavuta herufi "Mim" ilioko kabla ya "Nuun" katika neno "Al-Rahmaan", na anavuta herufi "Haa" katika neno "Al-Rahiim".
Mafunzo
Kuvuta ni kuzishibisha herufi za mada nazo ni (Alif, Wau, Yaa) zinapokuwa na sakina na kabla yake kukawa haraka (silabi) inayoendana nayo.
Kumebainishwa muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kuisoma Qur'ani.
Kutekeleza kwa vitendo kwa ajili ya kubainisha kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Amesema Assindi: Kauli yake: "Akivuta sauti yake", yaani anarefusha herufi zinazofaa kurefushwa kwa kuzitumia kuzingatia na kutafakari na kumkumbusha mwenye kukumbuka.
Umuhimu wa kujua kanuni za kusoma Qur'ani (Tajwidi) na elimu za Qur'ani.
Kuzielewa dalili kunarejeshwa kwa wanachuoni, kama alivyoulizwa Anasi radhi za Allah ziwe juu yake akambainishi muulizaji.
Marejeo
صحيح البخاري (6/ 195) (5046).
عمدة القاري (20/55).
Kutoka kwa Abuu Mulaika: Kutoka kwa baadhi ya wake za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, amesema: Abuu Aamir, amesema Naafii: Nafikiri ni Hafswa -Yakuwa aliulizwa kuhusu kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Hakika nyinyi hamkiwezi, akasema: Akaambiwa hebu tueleze. Akasema: Akasoma kisomo cha taratibu, akasema Abuu Aamiri: Akasema Naafii: Akatusimulia Abuu Mulaika: "Alhamdulillaah Rabbil-Aalamiin" [Al-Faatiha: 1] Kisha akakata "Al Rahmaanir Rahiim" [Faatiha:3] kisha akakata "Maaliki yaumid diin".
Imepokelewa na AhmadDarajaSahihi
Maelezo
Aliulizwa Hafswa mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Kilikuwa vipi kisomo cha Qur'ani cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake? Akasema: Hakika nyinyi hamkiwezi mfano wake, akaambiwa: Tueleze. Amesema Naafii: Akatusomea Abuu Mulaika kisomo alichotulizana ndani yake; ili kielezee na kikaribiane na kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasoma: "Alhamdulillaahi Rabbil Aalamiin" kisha akakata kisomo, "Al Rahmaanir Rahiim", kisha akakata kisomo, "Maaliki yaumid diin".
Mafunzo
Kumebainishwa muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kusoma Qur'ani.
Kufanya kwa vitendo ili kubainisha namna ya kisomo cha Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Sheria ya kwenda taratibu katika kuisoma Qur'ani, hilo huleta msukumo wa kuizingatia.
Kuitilia maanani Qur'ani wema waliotangulia, na matendo ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
Umuhimu wa kujua kanuni za kuisoma Qur'ani (Tajwidi) na elimu za Qur'ani.
Marejeo
مسند أحمد (44/ 70) (26470).
الفتح الرباني لترتيب مسند أحمد الشيباني (3/237).
Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com