Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Makosa ya jinai.

Hadithi 4

Muumini hatoacha kuendelea kuwa katika wigo mpana katika dini yake, madam hajagusa damu ya haramu

عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَنْ يَزَالَ المُؤْمِنُ فِي فُسْحَةٍ مِنْ دِينِهِ، مَا لَمْ يُصِبْ دَمًا حَرَامًا».
Kutoka kwa bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Muumini hatoacha kuendelea kuwa katika wigo mpana katika dini yake, madam hajagusa damu ya haramu".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba muumini huendelea kuwa katika nafasi pana ya matendo mema, na kutaraji rehema ya Mwenyezi Mungu na msamaha na maghufira yake, mpaka atakapouwa mtu aliyeharamishwa kuuawa basi amali zake zitakuwa nyembamba kwake; kwa sababu hazitoshelezi kulipa mauaji na dhambi lake kubwa.

Mafunzo
  1. Uzito wa kuuwa pasina haki na kuuwa kwa makusudi, kwani hilo linamtoa muumini katika nafasi ndani ya dini na kuwa katika dhiki.
  2. Damu zilizoharamishwa ni aina nne: 1. Damu ya Muislamu, na hii ni ya thamani kubwa zaidi. 2. Damu ya Dhimmi, hawa ni Wayahudi na Wakristo ambao wanaishi katika nchi za Kiislamu wakiwa na dini yao, kwa masharti ya kulipa jizia (kodi maalum) na kukubali kutii sheria za Kiislamu. 3. Damu ya Muahid - Hawa ni makafiri wanaoishi katika nchi zao ambao kati yetu na wao kuna mkataba wa amani, hatuwapigi vita wala wao hawatupigi vita. 4. Damu ya Musta'min - Huyu ni kafiri wa kivita ambaye kati yetu na yeye hakuna mkataba wala ahadi, lakini amepewa ulinzi kwa muda maalum ili kuingia katika ardhi za Waislamu kwa idhini ya mtawala wa Kiislamu au mmoja wa wawakilishi wake wenye mamlaka ya kutoa ulinzi huo.
Marejeo

صحيح البخاري (9/ 2) (6862). إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (10/ 41). تطريز رياض الصالحين (ص: 171).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Atakayejirusha kutoka juu ya mlima akajiua basi huyo atakuwa motoni akijirusha humo milele na milele

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «مَنْ تَرَدَّى مِنْ جَبَلٍ فَقَتَلَ نَفْسَهُ فَهُوَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ يَتَرَدَّى فِيهِ خَالِدًا مُخَلَّدًا فِيهَا أَبَدًا، وَمَنْ تَحَسَّى سُمًّا فَقَتَلَ نَفْسَهُ فَسُمُّهُ فِي يَدِهِ يَتَحَسَّاهُ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدًا مُخَلَّدًا فِيهَا أَبَدًا، وَمَنْ قَتَلَ نَفْسَهُ بِحَدِيدَةٍ فَحَدِيدَتُهُ فِي يَدِهِ يَجَأُ بِهَا فِي بَطْنِهِ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدًا مُخَلَّدًا فِيهَا أَبَدًا».
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Atakayejirusha kutoka juu ya mlima akajiua basi huyo atakuwa motoni akijirusha humo milele na milele, na atakayemeza sumu akajiua basi sumu yake itakuwa mkononi mwake akiimeza ndani ya Moto wa Jahannamu milele na milele humo, na atakayeiua nafsi yake kwa chuma basi chuma chake kitakuwa mkono mwake akilichomo tumbo lake ndani ya Moto Jahannamu milele na milele humo".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa yeyote atakayekusudia kujiua katika dunia, basi ataadhibiwa siku ya Kiyama ndani ya Moto wa Jahannamu kwa njia hiyo hiyo aliyoifanya yeye mwenyewe katika dunia, hayo yakiwa ni malipo kulingana na alichokifanya, atakayejirusha mwenyewe kutoka juu ya mlima akajiua, basi atakuwa ndani ya Moto wa Jahannam akidondoka humo katika milima ya Jahannamu na katika mabonde yake milele na mile humo, na atakayejipiga mwenyewe kwa chuma tumboni mwake akajiua, basi chuma chake kitakuwa mkononi kwake akichoma kwa chuma hicho tumbo lake ndani ya Moto wa Jahannam milele na milele humo.

Mafunzo
  1. Uharamu wa mtu kujiua mwenyewe, na kwamba hilo ni katika madhambi makubwa ambayo mtu anastahiki adhabu kali kwa hilo.
  2. Yaliyotajwa katika hadithi ni baadhi ya aina za kujitoa uhai, na vinginevyo, kwa njia yoyote atakayojiua mtu ataadhibiwa kwa mfano wa kile alichokifanya, na imekuja katika Sahihi Bukhari kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: "Anayejinyonga mwenyewe basi anainyonga nafsi yake katika Moto, na anayejichoma kwa kitu chenye ncha kali basi anaichoma nafsi yake katika Moto".
  3. Amesema Nawawi: Na ama kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: "Basi atakuwa katika Moto wa Jahannam milele na milele humo"; Kumesemwa ndani yake kauli nyingi: Ya kwanza: Nikuwa hili linachukuliwa hivyo kwa atakayefanya hivyo kwa kuhalalisha kitendo hicho huku akijua uharamu wake, basi huyu ni kafiri, na hii ndiyo adhabu yake. Ya pili: Nikuwa makusudio ya milelel ni kukaa muda mrefu na maisha marefu na si uhalisia wa kuishi milele, kama inavyoweza kusemwa: Mwenyezi Mungu aubakishe milele ufalme wa mfalme. Na ya tatu: Ni kuwa haya ni malipo yake, lakini kwa takrima ya Aliyetakasika na kutukuka alieleza kuwa hatombakisha milele yeyote atakayekufa akiwa ni muislamu.
  4. Hii ni katika sehemu ya adhabu za Akhera kuendana na aina ya makosa ya duniani, na inachukuliwa katika hili kuwa kosa la jinai la mtu kwa nafsi yake ni kama kumtendea jinai mtu mwingine kulingana na madhambi yake; kwa sababu nafsi yake si milki yake moja kwa moja, bali ni milki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, hivyo, hawezi kuwa na maamuzi yoyote isipokuwa yale yaliyoidhinishwa kwake.
Marejeo

صحيح البخاري (7/ 139) (5778). صحيح مسلم (1/ 103) (109). البحر المحيط الثجاج في شرح صحيح الإمام مسلم بن الحجاج (3/ 306). إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (8/ 414). المفهم لما أشكل من تلخيص كتاب مسلم (1/ 310). عمدة القاري شرح صحيح البخاري (21/ 291).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Asiashirie mmoja wenu silaha kwa ndugu yake, kwani hajui, huenda Shetani akaipokonya kutoka mkononi mwake, akatumbukia katika shimo la moto

عَن أَبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لاَ يُشِيرُ أَحَدُكُمْ عَلَى أَخِيهِ بِالسِّلاَحِ، فَإِنَّهُ لاَ يَدْرِي، لَعَلَّ الشَّيْطَانَ يَنْزِعُ فِي يَدِهِ، فَيَقَعُ فِي حُفْرَةٍ مِنَ النَّارِ».
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Asiashirie mmoja wenu silaha kwa ndugu yake, kwani hajui, huenda Shetani akaipokonya kutoka mkononi mwake, akatumbukia katika shimo la moto".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake muislamu kuashiria juu ya ndugu yake muislamu kwa silaha, kwa aina yoyote ile miongoni mwa aina za silaha, kwa sababu yeye hajui huenda Shetani akamsukuma kuitikisa silaha mkononi mwake, akamuuwa ndugu yake au akamuudhi, akatumbukia katika maasi yanayoweza kumpelekea kuingia katika shimo la moto.

Mafunzo
  1. Kumebainishwa uharamu wa damu muislamu.
  2. Ulazima wa kumheshimu muislamu na tahadhari ya kumfikishia shari kwake kwa kitendo au kauli, ikiwemo kumuashiria kwa chuma au silaha, hata kama ni kwa mzaha; kwa sababu Shetani anaweza kuutelezesha mkono wake na akampendezeshea kumpiga ndugu yake, au akaipokonya silaha kutoka mkononi mwake ikatua pasina maamuzi yake ikamdhuru ndugu yake.
  3. Kuziba njia zinazopelekea katika jambo kwa kukataza yanayopelekea katika haramu.
  4. Pupa ya kuhakikisha usalama wa jamii na kuhifadhi mahusiano baina ya watu, na kutowatisha na kuwaogopesha hata kama ni kwa ishara na kutishia.
Marejeo

صحيح البخاري (9/ 49) (7072). صحيح مسلم (4/ 2020) (2617). عمدة القاري شرح صحيح البخاري (24/ 187).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com