Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Muumini hatoacha kuendelea kuwa katika wigo mpana katika dini yake, madam hajagusa damu ya haramu

عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَنْ يَزَالَ المُؤْمِنُ فِي فُسْحَةٍ مِنْ دِينِهِ، مَا لَمْ يُصِبْ دَمًا حَرَامًا».
Kutoka kwa bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-: "Muumini hatoacha kuendelea kuwa katika wigo mpana katika dini yake, madam hajagusa damu ya haramu".
Imepokelewa na Al-BukhaariyDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba muumini huendelea kuwa katika nafasi pana ya matendo mema, na kutaraji rehema ya Mwenyezi Mungu na msamaha na maghufira yake, mpaka atakapouwa mtu aliyeharamishwa kuuawa basi amali zake zitakuwa nyembamba kwake; kwa sababu hazitoshelezi kulipa mauaji na dhambi lake kubwa.

Mafunzo
  1. Uzito wa kuuwa pasina haki na kuuwa kwa makusudi, kwani hilo linamtoa muumini katika nafasi ndani ya dini na kuwa katika dhiki.
  2. Damu zilizoharamishwa ni aina nne: 1. Damu ya Muislamu, na hii ni ya thamani kubwa zaidi. 2. Damu ya Dhimmi, hawa ni Wayahudi na Wakristo ambao wanaishi katika nchi za Kiislamu wakiwa na dini yao, kwa masharti ya kulipa jizia (kodi maalum) na kukubali kutii sheria za Kiislamu. 3. Damu ya Muahid - Hawa ni makafiri wanaoishi katika nchi zao ambao kati yetu na wao kuna mkataba wa amani, hatuwapigi vita wala wao hawatupigi vita. 4. Damu ya Musta'min - Huyu ni kafiri wa kivita ambaye kati yetu na yeye hakuna mkataba wala ahadi, lakini amepewa ulinzi kwa muda maalum ili kuingia katika ardhi za Waislamu kwa idhini ya mtawala wa Kiislamu au mmoja wa wawakilishi wake wenye mamlaka ya kutoa ulinzi huo.
Marejeo

صحيح البخاري (9/ 2) (6862). إرشاد الساري لشرح صحيح البخاري (10/ 41). تطريز رياض الصالحين (ص: 171).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com
Makosa ya jinai.

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com