Ruka hadi kwenye maudhui
Hadithi zenye maelezo

Kisasi.

Hadithi 1

La kwanza litakalohukumiwa kati ya watu siku ya kiyama ni katika damu

عَنْ عَبْدِ اللهِ بنِ مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «أَوَّلُ مَا يُقْضَى بَيْنَ النَّاسِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِي الدِّمَاءِ».
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema: "La kwanza litakalohukumiwa kati ya watu siku ya kiyama ni katika damu".
Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wakeDarajaSahihi
Maelezo

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa jambo la kwanza litakalohukumiwa baina ya watu katika dhulma zao wao kwa wao siku ya Kiyama: Itakuwa katika damu, kama kuua na kujeruhi.

Mafunzo
  1. Ukubwa wa swala la damu, kwani siku zote jambo muhimu zaidi ndio hutangulizwa.
  2. Dhambi huwa kubwa kulingana na madhara yanayojitokeza, na kuua nafsi isiyo na hatia ni katika madhara makubwa na hakuna kubwa zaidi yake isipokuwa ukafiri na kumshirikisha Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Marejeo

صحيح البخاري (9/ 2) (6864). صحيح مسلم (3/ 1304) (1678). خلاصة الكلام شرح عمدة الأحكام، لفيصل آل مبارك (ص319). تيسير العلام شرح عمدة الأحكام، للبسام (ص640). الإلمام بشرح عمدة الأحكام، لإسماعيل الأنصاري (2/ 103).

Hadithi hii kwenye HadeethEnc.com

Kila hadithi, daraja, maelezo na funzo hapa vinaonyeshwa kama HadeethEnc.com inavyovichapisha, kwa masharti yake ya kuchapisha upya. Daraja halimtaji aliyelitoa. Tafsiri na maelezo ni ya waandishi wake wenyewe, na baadhi hutaja hukumu; wahakiki wa Sabīl hawajavichunguza. Hadithi ya Kiarabu ndiyo matini. Chanzo: HadeethEnc.com