Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · Al-Baqara
Sura ya 2

Al-Baqara

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 253

تِلْكَ ٱلرُّسُلُ فَضَّلْنَا بَعْضَهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۘ مِّنْهُم مَّن كَلَّمَ ٱللَّهُ ۖ وَرَفَعَ بَعْضَهُمْ دَرَجَـٰتٍ ۚ وَءَاتَيْنَا عِيسَى ٱبْنَ مَرْيَمَ ٱلْبَيِّنَـٰتِ وَأَيَّدْنَـٰهُ بِرُوحِ ٱلْقُدُسِ ۗ وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ مَا ٱقْتَتَلَ ٱلَّذِينَ مِنۢ بَعْدِهِم مِّنۢ بَعْدِ مَا جَآءَتْهُمُ ٱلْبَيِّنَـٰتُ وَلَـٰكِنِ ٱخْتَلَفُوا۟ فَمِنْهُم مَّنْ ءَامَنَ وَمِنْهُم مَّن كَفَرَ ۚ وَلَوْ شَآءَ ٱللَّهُ مَا ٱقْتَتَلُوا۟ وَلَـٰكِنَّ ٱللَّهَ يَفْعَلُ مَا يُرِيدُ 253

{253} Al-Bari (Muumba mwanzilishi) anajulisha kwamba Yeye alitofautisha kati ya Mitume katika fadhila kubwa na mateuzi mazuri. Kulingana na kile ambacho Mwenyezi Mungu aliwapa na walichofanya wao kama vile imani kamili, yakini madhubuti, tabia na maadili ya juu, kulingania, kuelimisha na manufaa ya jumla. Miongoni mwao kuna yule aliyemfanya kuwa rafiki mwandani. Na miongoni mwao kuna yule aliyezungumza naye kwa maneno. Na miongoni mwao kuna yule aliyemnyanyua daraja juu ya viumbe. Na wote, hakuna njia kwa yeyote kati ya watu ya kufikia fadhila zao za juu mno. Na akamteua Isa bin Maryam kwa kumpa hoja zilizo wazi zenye kuoyesha kwamba yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa haki, na mja wake kwa ukweli. Na kwamba yale aliyokuja nayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni haki. Basi akamfanya kuwaponya vipofu wa tangu kuzaliwa na wakoma. Na akawafufuwa maiti kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na aliwaongelesha watu katika malezi hali ya kuwa ni mtoto. Na akamtia nguvu kwa Roho mtakatifu. Yani kwa roho wa imani. Kwa hivyo, akaifanya hali yake ya kiroho kuwa bora zaidi ya hali za kiroho za wengine. Na akapata nguvu na kuungwa mkono kwa hilo. Hata ingawa asili ya kuungwa mkono na roho hii ni ya jumla kwa kila Muumini kulingana na imani yake, kama alivyosema. "Na akawaunga mkono kwa roho itokayo kwake". Lakini alicho nacho Isa ni kikubwa zaidi kuliko kile walicho nacho wengine. Na ndio maana Mwenyezi Mungu akamtaja hususan. Na ikasemwa: Roho Mtakatifu hapa ni Jibril, Mwenyezi Mungu alimuunga mkono kwa msaada na kumtia nguvu, lakini maana sawa ni ile ya kwanza. Na alipojulisha kuhusu ukamilifu wa Mitume na alichowapa katika fadhila na sifa maalumu. Na kwamba Dini yao ni moja, na wito wao kwa heri ni mmoja. Na ilikuwa inalazimu kwa sababu ya hilo kwamba umma zote zikusanyike juu ya kuwasadiki. Na kuwafuata kwa sababu ya yale aliyowapa miongoni mwa hoja zilizo wazi ambazo mfano wake watu waliamini. Lakini wengi wao walipotoka njia iliyonyooka, na hitilafu ikatokea kati ya umma. Basi miongoni mwao kuna wale walioamini na miongoni mwao kuna wale waliokufuru, kwa hivyo kwa sababu ya hilo vikatokea vita ambavyo ni matokeo ya hitilafu hiyo na uadui huo. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angependa, angeliwakusanya juu ya uwongofu, na wasingelihitalifiana. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angependa pia baada ya kutokea hitilafu hiyo iliyolazimu kupigana, hawangepigana. Lakini hekima yake ililazimu mambo yaende kulingana na mfumo huu kulingana na sababu. Basi katika aya hii kuna ushahidi mkubwa kabisa kwamba, Mwenyezi Mungu Mtukufu anaziendesha sababu zote zinazolazimu matokeo yake, na kwamba akipenda, anazibakisha. Na akipenda, anazizuia. Na hayo yote yanafuata hekima yake peke yake. Kwani, yeye ndiye afanyaye atakalo. Kwa hivyo, mapenzi yake na kutaka kwake hakuna kizuizi chochote, wala mpinzani, wala msaidizi.