Al-Baqara
Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.
Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22
ٱلَّذِينَ ءَاتَيْنَـٰهُمُ ٱلْكِتَـٰبَ يَتْلُونَهُۥ حَقَّ تِلَاوَتِهِۦٓ أُو۟لَـٰٓئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِۦ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِهِۦ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْخَـٰسِرُونَ 121
Kisha akasema:
(121) Mwenyezi Mungu anafahamisha ya kwamba, wale waliojiwa na Kitabu na akawaneemesha kwacho neema isiyo na kifani, kwamba "wanakisoma kama ipasavyo kusomwa." Yani wanakifuata kwa haki ya kukifuata. Na kisomo ni kufuata. Kwa hivyo, wanahalalisha halali yake, na wanaharamisha haramu yake, na wanatenda kwa muhkam yake (Aya zenye maana wazi); na wanaamini katika Mutashabih yake (aya zisizo na maana wazi). Na hawa ndio wenye furaha miongoni mwa Watu wa Kitabu ambao walizijua neema za Mwenyezi Mungu na wakazishukuru, na wakamwamini kila Mtume, na wala hawakutofautisha baina ya yeyote miongoni mwao. Na hawa ndio Waumini wa kweli. Sio yule aliyesema miongoni mwao: Tunaamini tuliyoteremshiwa sisi, na wanayakataa yasiyokuwa hayo. Na kwa sababu ya hili, akawatishia kwa kusema: "Na wanao kikataa, basi hao ndio wenye kukhasiri."