Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 2 · Aya ya 121

Al-Baqara 2:121

البقرة

ٱلَّذِينَ ءَاتَيْنَـٰهُمُ ٱلْكِتَـٰبَ يَتْلُونَهُۥ حَقَّ تِلَاوَتِهِۦٓ أُو۟لَـٰٓئِكَ يُؤْمِنُونَ بِهِۦ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِهِۦ فَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْخَـٰسِرُونَ

Maana

Wale tuliowapa Kitabu, wanakisoma kama ipasavyo kukisoma. Hao ndio kweli wanakiamini. Na wanaokikataa, basi hao ndio wenye kuhasiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wale tulio wapa Kitabu, wakakisoma kama ipasavyo kusomwa, hao ndio kweli wanakiamini. Na wanao kikataa basi hao ndio wenye kukhasiri. [121]

[121] Tena kipo kikundi katika Mayahudi na Wakristo walio wataalamu katika vitabu vyao vya asli, na wakavisoma vilivyo, na wakafahamu mageuzo yaliomo ndani yake, hao wanauamini ukweli wa mambo, na kwa hivyo wanaiamini hii Qur'ani. Na wenye kukikataa Kitabu kilicho teremka kutoka kwa Mwenyezi Mungu hao ndio wenye kukhasiri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wale Mayahudi na Wanaswara tuliowapa Kitabu, wanakisoma kisomo cha sawasawa, wanakifuata kipasavyo kufuatwa na wanayaamini yaliyomo ndani yake ya kuwaamini Mitume wa Allah Mtukufu, ambao miongoni mwao ni wa mwisho wao, Nabii wetu na Mtume wetu Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie,. Na hawayapotoi wala hawayabadilishi yaliyokuja ndani yake. Hawa ndio waliomuamini Nabii, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na aliyoteremshiwa. Ama wale waliogeuza sehemu ya Kitabu na wakaficha baadhi yake, hao ndio waliomkanusha Nabii wa Allah Mtukufu Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, na yale aliyoteremshiwa. Na wenye kumkanusha, hao watakuwa ni wetu wenye hasara kubwa mbele ya Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Baqara

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net