At-Tawba
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
وَعَلَى ٱلثَّلَـٰثَةِ ٱلَّذِينَ خُلِّفُوا۟ حَتَّىٰٓ إِذَا ضَاقَتْ عَلَيْهِمُ ٱلْأَرْضُ بِمَا رَحُبَتْ وَضَاقَتْ عَلَيْهِمْ أَنفُسُهُمْ وَظَنُّوٓا۟ أَن لَّا مَلْجَأَ مِنَ ٱللَّهِ إِلَّآ إِلَيْهِ ثُمَّ تَابَ عَلَيْهِمْ لِيَتُوبُوٓا۟ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ 118
{118} "Na" vile vile [Mwenyezi Mungu] alikubali toba ya "wale watatu walioachwa nyuma" wakakosa kutoka pamoja na Waislamu katika vita hivyo. Na ni Ka'ab bin Malik na sahibu zake wawili. Na kisa chao ni mashuhuri na kinajulikana katika vitabu vya hadithi Sahih na Sunan. “Hata” walipohuzunika huuzuni mkubwa, “na ardhi wakaiona kuwa ni finyu juu yao pamoja na ukunjufu wake.” Yaani, pamoja na upana wake na wasaa wake, "na nafsi zao zikawabana," ambazo ndizo pendwa zaidi kwao kuliko kila kitu. Kwa hivyo, anga ya nje iliyo pana inayopendwa, ambayo haijawahi kuwa desturi kwamba mtu anaiona kuwa ni finyu. Na hilo haliwi isipokuwa kwa sababu ya jambo la kusumbua lililofikia kiwango cha ugumu na mashaka kisichowezakana kuelezwa. Na hilo ni kwa sababu walitanguliza ridha ya Mwenyezi Mungu na ridha ya Mtume Wake mbele ya kila kitu. "Na wakayakinika kuwa hakuna kimbilio kutoka kwa Mwenyezi Mungu isipokuwa kwake Yeye.” Yaani wakawa na yakini na wakajua hali yao ya kuwa hakuna awezaye kuokoa kutokana na ugumu, na kumkimbilia isipokuwa Mwenyezi Mungu peke Yake, asiyekuwa na mshirika yeyote, basi kufungamana kwao na viumbe, kukakatika, na wakafungamana na Mwenyezi Mungu, Mola wao Mlezi, na wakakimbia kutoka kwake kwenda kwake. Basi wakakaa katika ugumu huo kwa muda wa usiku hamsini. "Kisha akawakubalia toba;” yaani, akawaruhusu kutubia na akawawezesha kufanya hivyo, "ili watubu" kihalisi ili Mwenyezi Mungu awakubalie toba. "Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kukubali toba sana;” yaani, mwingi wa toba, na msamaha, na maghufira juu ya kuteleza kwao na mapungufu yao; "Mwenye kurehemu.” Sifa yake ni rehema kubwa ambayo haijaacha kuendelea kuwashukia waja wake katika kila wakati na kila zama, na katika kila muda ambayo kwayo yanasimama vyema mambo yao ya kidini na ya kidunia. Na katika aya hizi kuna ushahidi kwamba kukubali toba kwa Mwenyezi Mungu kutoka kwa mja ndilo lengo kubwa zaidi mwisho wa juu kabisa. Kwani Mwenyezi Mungu alifanya hilo kuwa mwisho wa waja wake maalumu. Na aliwaneemesha huo walipofanya matendo ambayo anayapenda na kuyaridhia. Na miongoni mwake ni upole wa Mwenyezi Mungu kwao, na kuwaimarisha kwake imani yao wakati wa shida na misiba ya kuudhi. Na miongoni mwake ni Ibada ambayo ni ngumu juu ya nafsi ina fadhila na ubora ambao haupo kwa nyinginezo. Na kila shida inapokuwa kubwa, malipo pia yanakuwa makubwa. Na miongoni mwake ni kwamba, toba ya Mwenyezi Mungu kwa mja Wake ni kulingana na majuto yake na huzuni wake mkubwa. Na kwamba yule ambaye hajali dhambi wala haoni ubaya anapoifanya, basi toba yake haikubaliwi, hata kama atadai kuwa inakubalika. Na miongoni mwake ni kwamba, alama ya heri na kuondoka kwa shida ni wakati moyo wake utafungamana kikamilifu na Mwenyezi Mungu Mtukufu na ukaacha kufungamana na viumbe. Na miongoni mwake ni kwamba, katika upole wa Mwenyezi Mungu kwa hao watatu ni kwamba aliwaeleza kwa alama isiyokuwa ya kuwaaibisha. Akasema, “walioachwa nyuma” ishara ya kuwa Waumini waliwaacha nyuma au waliachwa nyuma ya wale waliokwisha kubaliwa udhuru wao, au waliokataliwa udhuru wao, na kwamba kubaki kwao nyuma hakukuwa kwa sababu ya kukataa heri, na ndiyo maana hakusema: waliobaki nyuma. Na miongoni mwake ni kwamba, Mwenyezi Mungu Mtukufu aliwaneemesha ukweli, na ndiyo maana akaamrisha waigwe, akasema: