U bood nuxurka
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Noor
Suuradda 24

An-Noor

Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.

Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22

Aayadda 11

إِنَّ ٱلَّذِينَ جَآءُو بِٱلْإِفْكِ عُصْبَةٌ مِّنكُمْ ۚ لَا تَحْسَبُوهُ شَرًّا لَّكُم ۖ بَلْ هُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۚ لِكُلِّ ٱمْرِئٍ مِّنْهُم مَّا ٱكْتَسَبَ مِنَ ٱلْإِثْمِ ۚ وَٱلَّذِى تَوَلَّىٰ كِبْرَهُۥ مِنْهُمْ لَهُۥ عَذَابٌ عَظِيمٌ 11

Pindi alipotaja katika yale yaliyotangulia hapo juu ukubwa wa shutuma za zinaa kwa ujumla; hili likawa kana kwamba ni utangulizi wa kisa hiki kilichotokea kwa mtukufu zaidi wa wanawake, Mama wa Waumini, Mungu amuwiye radhi. Aya hizi ziliteremka katika kisa mashuhuri cha uzushi, ambacho kimethibitishwa katika Sahih, Sunan na Musnad. Mwisho ni kwamba, Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, - alikuwa katika baadhi ya vita vyake pamoja na mkewe Aisha Al-Siddiqa -mkweli, binti wa Abubakar Al-Siddiq, na ukakatika mkufu wake, naye akazuilika katika kuutafuta mkufu huo. Wakamchukua ngamia wake na kikalio chake, wala hawakupeleleza kama yumo ndani ya kikalio hicho. Kisha jeshi likapanda vipando vyao likaondoka. Akafika Nana Aisha mahali hapo walipokuwa, na akajua kwamba wakimkosa watarejea hapo kwa ajili yake. Kisha wakaendelea na msafara wa mwendo wao. Safwan bin Al-Mu-a’tal Al-Sulami alikuwa miongoni mwa maswahaba bora kabisa, Mungu amuwie radhi. Na alikuwa kaingia usiku kwa watu wengine wa watu akalala, akamuona Aisha Mwenyezi Mungu amuwie radhi na akamtambua. Akamuinamisha ngamia wake, na Aisha akampanda bila ya hao wawili kuzungumziana. Kisha akaja akiwa anamuendesha baada ya jeshi kushuka alasiri. Na walipowaona baadhi ya wanafiki waliokuwa pamoja na Mtume, – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie – katika safari hiyo, kuja kwa Safwan na Aisha katika hali hii; ikavuma na kuenea yaliyoenea, na kisa kikaongezwa maelezo ya uongo na ndimi zikakiharibu na kukichafua kisa hiki mpaka wakadanganyika baadhi ya Waumini kwa hilo. Na wakawa wanasambaziana maneno hayo, na wahyi ukazuiliwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu – rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kwa muda mrefu. Na habari hiyo ilimfikia Aisha muda mfupi baadaye, na alihuzinika huzuni kubwa. Basi Mwenyezi Mungu akateremsha umbali wake na uzushi huo katika Aya hizi, na Mwenyezi Mungu akawaaidhia na kuwapa mawaidha Waumini na akalifanya kubwa jambo hilo, na akawausia wao wasia yenye manufaa.

{11} Na kauli yake Mwenyezi Mungu aliyetukuka, "Hakika wale walioleta uongo;" yaani, uongo mbaya." Yaani ni kumkashifu Mama wa Waumini, "Ni kundi miongoni mwenu." Yaani, kundi lililonasibiana na nyinyi, enyi kongamano la wa Waumini. Miongoni mwao kuna Muumini wa kweli katika Imani yake, lakini alidanganyika na propaganda za wanafiki. Na miongoni mwao mnafiki. "Msifikiri ni shari kwenu, bali hiyo ni kheri kwenu;" kwa lile lililofungamana nalo kwa kuepushwa na kuwekwa mbali kwa Mama wa Waumini na kutakaswa kwake na kusifu utajo, hadi ikawafikia sifa ya jumla wake zake wote Mtume – rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, – na kwa sababu ilifungamana katika kubainisha aya walizolazimishwa waja kuzifanya, ambazo bado zinaendelea kutekelezwa na kutendewa kazi hadi siku ya Kiyama. Yote haya ni kheri kubwa. Lau si maneno ya watu wa uzushi, hili lisingetokea. Na akitaka Mwenyezi Mungu jambo; hutoa na kujalia sababu. Na kwa hivyo, akaifanya hotuba kuwa ya jumla kwa waumini wote. Na akaeleza kuwa kusingizia na kusema vibaya baadhi yao wengine ni kama kujisema vibaya na kujisingizia wenyewe. Ndani yake ni kuwa waumini katika kupendana kwao, na kuhurumiana kwao, na umoja wao katika maslahi yao ni kama mwili mmoja, na Muumini kwa Muumini ni kama jengo linalotegemezana. Kama vile anavyochukia mtu yeyote kusemwa vibaya heshima yake; na basi achukie kwa kila mtu kumsema vibaya na kumkashifu Muumini mwenzake, ambaye yuko katika nafasi sawa na yeye mwenyewe. Na isipokuwa ikimfikia mja hali hii; basi hiyo ni kutokana na upungufu wa imani yake na kukosa ushauri. "Kila mtu katika wao atapata aliyoyachuma katika madhambi." Na hili ni onyo kwa wale waliokuja na uzushi, na kwamba wataadhibiwa kwa yale waliyoyasema katika hayo. Na alilizuia Mtume - rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kundi miongoni mwao; "Na yule aliyejitwika sehemu yake kubwa." Yaani, uzushi mkubwa, naye ni mnafiki mwovu kabisa, Abdullah bin Ubayy bin Salul, Mwenyezi Mungu amlaani. "Atapata adhabu kubwa." Ambayo ni kudumu milele katika tabaka la chini kabisa ya Moto.