Ibrahim
Kani waa tarjumaad tafsiirka as-Saʿdī sida IslamHouse.com ugu daabacdo saadi.islamenc.com, oo laga akhriyay bogagga goobtaas. Goobtu ma sheegayso cidda tarjuntay ama daabacaadda la daabacay ee ay raacayso, mana sheegayso shuruudo qaadashada qoraalkeeda ah, sidaas darteed xaqa muujinteeda lama xaqiijin. Qofna ma barbardhigin buug la daabacay, aqoonyahanna ma dib u eegin. Qayb kasta waxay ag taagan tahay aayadaha ay ka hadlayso, kuwaas oo ah qoraalka Quraanka ee Tanzil, sida uu ugu yaal halkaas; aayad goobtu aanay faallo u gaar ah ka bixin waxay la taagan tahay qaybta ka horraysa, tusmaduna waxay magacaabaysaa aayad kasta oo caynkaas ah. Sabīl wax ka mid ah ma qorin, mana tarjumin.
Qoraalka waxaa laga helaysaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)la qaaday 2026-10-22
الٓر ۚ كِتَـٰبٌ أَنزَلْنَـٰهُ إِلَيْكَ لِتُخْرِجَ ٱلنَّاسَ مِنَ ٱلظُّلُمَـٰتِ إِلَى ٱلنُّورِ بِإِذْنِ رَبِّهِمْ إِلَىٰ صِرَٰطِ ٱلْعَزِيزِ ٱلْحَمِيدِ 1 ٱللَّهِ ٱلَّذِى لَهُۥ مَا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ ۗ وَوَيْلٌ لِّلْكَـٰفِرِينَ مِنْ عَذَابٍ شَدِيدٍ 2
{1 - 2} Yeye Mtukufu anajulisha kwamba aliteremsha Kitabu Chake kwa Mtume Wake Muhammad -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake - kwa manufaa ya viumbe, nayo ni kuwatoa watu katika giza la ujinga, ukafiri, tabia mbaya, na aina mbalimbali za maasia hadi kwenye nuru ya elimu, imani na tabia nzuri. Na kauli yake, "kwa idhini ya Mola wao Mlezi;" yaani, hawawezi kufanya kunachohitajika, kinachopendwa na Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa idhini na msaada wa Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo ndani yake kuna himizo kwa waja juu kuomba msaada kwa Mola wao Mlezi. Kisha akaibainisha nuru ambayo kitabu hiki kinawaongoza kuiendea, akasema: "Kwenye Njia ya Mwenye Nguvu, Msifika." Yaani, kuifikia na kufikia nyumba ya utukufu wake, ambacho kinajumuisha kuijua haki na kuifanyia kazi. Na katika kumtaja Mwenye nguvu, Msifika baada ya kutaja njia inayoelekea huko kuna ishara kwamba mwenye kuifuata, basi yeye ni mtukufu kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu, mwenye nguvu hata kama hana wasaidizi isipokuwa Mwenyezi Mungu, mwenye kusifiwa katika mambo yake, mwenye mwisho mwema, na hii inaashiria kuwa njia ya Mwenyezi Mungu ni moja ya ushahidi mkubwa zaidi juu ya kile alicho nacho Mwenyezi Mungu cha sifa kamilifu na utukufu. Na kwamba yule aliyewawekea waja wake ni mwenye mamlaka ya utukufu, Msifika katika kauli zake, vitendo vyake, na hukumu zake. Na kwamba Yeye ndiye afanyiwaye uungu, muabudiwa kwa ibada ambazo ndizo vituo vya njia hiyo iliyonyooka, na kwamba namna alivyo ina ufalme wa mbingu na ardhi kwa kuviumba, kuruzuku, na kuviendesha, basi anayo haki ya kuwahukumu waja Wake kwa mujibu wa hukumu zake za kidini. Kwa sababu hao ni milki yake, na haimfailii kuwaacha bure hivyo. Kwa hivyo, alipobainisha ushahidi na hoja, akawaahidi adhabu wale ambao hawakuyafuata hayo. Basi akasema, "Na ole wao makafiri kutokana na adhabu kali!" ambayo haiwezekani kupima kiasi chake, wala haiwezi kuelezwa jambo lake.