Al-Jaathiya
Voici une traduction du tafsîr d’as-Saʿdī, telle qu’IslamHouse.com la publie sur saadi.islamenc.com, lue dans les pages de ce site. Le site ne dit ni qui l’a traduite ni quelle édition imprimée elle suit, et n’indique aucune condition pour en reprendre le texte, si bien que le droit de la montrer n’est pas vérifié. Personne ne l’a comparée à un livre imprimé, et aucun savant ne l’a relue. Chaque passage se tient à côté des versets qu’il commente, qui sont le texte coranique de Tanzil, montré tel qu’il y est ; un verset auquel le site ne donne aucun commentaire propre se tient avec le passage qui le précède, et l’index nomme chacun de ces versets. Sabīl n’en a rien écrit ni traduit.
Texte desaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)pris le 2026-10-22
وَسَخَّرَ لَكُم مَّا فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ جَمِيعًا مِّنْهُ ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ لِّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ 13
{13} "Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake." Yaani, hayo yote ni kutokana na fadhila zake na wema wake. Hayo yanajumuisha vyombo vilivyo mbinguni na duniani, na vyote alivyoweka humo Mwenyezi Mungu kama vile jua, mwezi, sayari zisizosonga na zenye kusonga, na aina mbalimbali za wanyama, miti, mazao, aina mbalimbali za madini na mambo mengineyo ambayo yametayarishwa kwa ajili ya masilahi ya wanadamu ambayo wanayahitaji sana. Hayo yote yanawalazimu kufanya juhudi kubwa zaidi katika kushukuru neema zake, na kwamba fikira zao zizame katika kuzingatia ishara zake na hekima zake, na ndiyo maana akasema: "Hakika katika hayo zimo Ishara kwa watu wanaofikiri." Kwa ufupi, uumbaji wake, uendeshaji wake na kuvitiisha kwake vyote vinaonyesha kutekelezeka kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na ukamilifu wa uwezo wake. Na ustadi mkubwa ulio ndani yake, usawasawa wake, ufundi wake wa hali ya juu na maumbile yake mazuri zaidi, yote haya yanaashiria ukamilifu wa hekima yake na elimu yake. Na upana wake, ukubwa wake na wingi wake vinaashiria upana wa ufalme wake na mamlaka yake. Na mambo maalumu yaliyomo, na vitu vilivyo kinyume cha vingine ni ushahidi kwamba Yeye ndiye anafanya kabisa anachotaka. Na manufaa yaliyo ndani yake na masilahi ya kidini na kidunia ni ushahidi wa upana wa rehema yake, ujumla wa fadhila zake na wema wake, na upole wake mkubwa na wema wake, na hayo yote yanaashiria kwamba Yeye peke yake ndiye anayestahiki kufanyiwa uungu na kuabudiwa, ambaye haifai kufanywa ibada wala kujidhalilisha wala kumpenda isipokuwa Yeye, na kwamba Mitume wake ni wakweli katika yale waliyokuja nayo. Huu ni ushahidi wa kiakili ulio wazi, ambao haukubali shaka au kusitasita kokote.