Al-An'aam
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
وَقَالُوا۟ لَوْلَآ أُنزِلَ عَلَيْهِ مَلَكٌ ۖ وَلَوْ أَنزَلْنَا مَلَكًا لَّقُضِىَ ٱلْأَمْرُ ثُمَّ لَا يُنظَرُونَ 8
{8} "Na walisema," pia kwa kuuegemea ujinga na kutokuwa na elimu mambo ya busara. "Mbona hakuteremshiwa Malaika?" Yaani, mbona hakuteremshwa Malaika pamoja na Muhammad ili amsaidie katika jambo lake? Kwa kudai kwao kwamba yeye ni mwanadamu na kwamba ujumbe wa Mwenyezi Mungu hauwi isipokuwa katika mikono ya malaika. Mwenyezi Mungu akasema katika kubainisha rehema yake na upole wake kwa waja wake kwa kuwa aliwatumia mwanadamu kutoka miongoni mwao, ili kuamini katika aliyoyaleta iwe juu ya elimu, na ufahamu na mambo ya ghaibu: "Na kama tungelimteremsha Malaika," kwa ujumbe wetu, basi Imani ingekuwa si kwa kutokana na kujua haki, lakini ingekuwa imani kwa ushahidi ambayo peke yake hainufaishi kitu. Hii ni ikiwa wataamini. Lakini uwezekano mkubwa zaidi ni kwamba hawataamini katika hali hii. Basi ikiwa hawaamini, "basi bila ya shaka ingeshahukumiwa amri;" kwa kuwaharakishia maangamizo juu yao na wala wasingengojewa. Kwa sababu hii ndiyo ada ya Mwenyezi Mungu katika wale wanaoomba aya wanazozipendekeza wao, kisha wasiziamini. Basi kuwatumia Mtume wa kibinadamu na Aya zilizo wazi ambazo Mwenyezi Mungu anajua kuwa, hizo ndizo bora zaidi kwa waja wake na nyepesi zaidi kwao, pamoja na Mwenyezi Mungu kuwapa muhula makafiri na wale wanaokadhibisha ni bora kwao na ni lenye manufaa zaidi. Basi maombi yao kwamba ateremshwe Malaika ni ubaya kwao, laiti wangelikuwa wanajua.