Al-An'aam
This is a translation of Tafsīr as-Saʿdī as IslamHouse.com publishes it at saadi.islamenc.com, read from that site’s pages. The site does not say who translated it or which printed edition it follows, and states no terms for taking its text, so the right to show it is not verified. Nobody has compared it with a printed book, and no scholar has reviewed it. Each passage stands beside the verses it comments on, which are the Qur’ān text of Tanzil, shown as it is there; a verse the site gives no commentary of its own stands with the passage before it, and the index names each such verse. Sabīl did not write or translate any of it.
Text fromsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)taken 2026-10-22
وَلَوْ نَزَّلْنَا عَلَيْكَ كِتَـٰبًا فِى قِرْطَاسٍ فَلَمَسُوهُ بِأَيْدِيهِمْ لَقَالَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوٓا۟ إِنْ هَـٰذَآ إِلَّا سِحْرٌ مُّبِينٌ 7
{7} Huku ni kumjulisha Mtume kunatoka kwa Mwenyezi Mungu kuhusu ukali wa ukaidi wa makafiri. Na kwamba, kukadhibisha kwao si kwa sababu ya upungufu ulio katika yale uliyowajia nayo, wala kutojua kwao hayo. Bali hilo ni dhuluma na kupita mipaka ambayo hamna hila yoyote katika hayo.” Kwa hivyo Akasema, "Na lau tungelikuteremshia kitabu cha karatasi, wakakigusa kwa mikono yao" na wakawa na yakini nacho, "basi wangelisema wale waliokufuru" kwa dhuluma na kiburi. "Haya si chochote isipokuwa ni uchawi ulio wazi" basi ni ushahidi gani ulio mkubwa zaidi kuliko ushahidi huu. Na hii ndiyo kauli yao mbaya juu yake, ambapo walilifanyia kiburi linalohisiwa ambalo hawezi mwenye akili hata kidogo kulikataa?