انتقل إلى المحتوى
Tafsir As-Saadi - Swahili · التوبة
السورة ٩

التوبة

هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.

النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22

الآية ٥٥

فَلَا تُعْجِبْكَ أَمْوَٰلُهُمْ وَلَآ أَوْلَـٰدُهُمْ ۚ إِنَّمَا يُرِيدُ ٱللَّهُ لِيُعَذِّبَهُم بِهَا فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَتَزْهَقَ أَنفُسُهُمْ وَهُمْ كَـٰفِرُونَ ٥٥

{55} Yeye Mtukufu anasema: basi zisikufurahishe mali za wanafiki hawa, wala watoto wao. Kwani, hakuna kuwafurahia na kutamani mfano wake katika hilo, na baraka yake ya kwanza kwao ni kwamba walizitanguliza mbele ya ridha za Mola wao Mlezi na wakamuasi Mwenyezi Mungu kwa sababu yake. "Hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwaadhibu kwazo katika maisha ya dunia hii" na maana ya adhabu hapa ni dhiki inayowapata katika kuitafuta, na juhudi kubwa katika hilo, na wasiwasi mkubwa ya moyo juu yake, na uchovu wa mwili. Lau kuwa utalinganisha raha zao ndani yake na dhiki zake, basi raha hizo hazingelilingana na chochote katika dhiki hizo. na zilipowaghafilisha na Mwenyezi Mungu na utajo wake, zikawa ni balaa kwao hata katika dunia hii. Na katika balaa zake kubwa na hatari zaidi ni kwamba nyoyo zao zimefungamana nazo, na utashi wao hayaendi zaidi ya hayo, kwa hivyo yanakuwa ndiyo mwisho wa yale wanayotafuta, na mwisho wa matamanio yao, wala halibaki fungu lolote kwa ajili ya Akhera katika nyoyo zao. Kwa hivyo hayo yanalazimu kwamba waondoke katika dunia, "na zitoke roho zao na hali wao ni makafiri." Basi je, ni adhabu gani kubwa zaidi kuliko adhabu hii inayosababisha masaibu ya kudumu, na kujuta kukubwa kusikoisha?