التوبة
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَمَا مَنَعَهُمْ أَن تُقْبَلَ مِنْهُمْ نَفَقَـٰتُهُمْ إِلَّآ أَنَّهُمْ كَفَرُوا۟ بِٱللَّهِ وَبِرَسُولِهِۦ وَلَا يَأْتُونَ ٱلصَّلَوٰةَ إِلَّا وَهُمْ كُسَالَىٰ وَلَا يُنفِقُونَ إِلَّا وَهُمْ كَـٰرِهُونَ ٥٤
{54} Kisha akabainisha sifa ya kuvuka kwao mipaka, na matendo yao [kwa hivyo akasema], "Na hawakuzuiliwa kukubaliwa kutoa kwao isipokuwa kwa kuwa walimkufuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake." Na sharti ya kukubaliwa matendo yote ni imani. Basi hawa hawana imani wala matendo mema, kiasi kwamba wakifanya swala, ambayo ndilo tendo bora zaidi ya mwili, wanapoifanya, wanaifanya kwa uvivu. Akasema: "wala hawaji kwenye Sala isipokuwa huku ni wavivu;" yaani, huku wanaona uzito na wanakaribia kutoifanya kwa sababu ya uzito wake juu yao. "Wala hawatoi isipokuwa nao wamechukia" bila ya kuwa na moyo mkunjufu na uthabiti wa nafsi. Basi katika hili kuna shutuma kubwa zaidi kwa mwenye kufanya mfano wa walivyofanya, na kwamba mja anapaswa asije kwenye Swala isipokuwa huku ni mkakamavu wa mwili na moyo juu yake, na wala asitoe isipokuwa huku ni mchangamfu wa kifua, thabiti wa moyo, akitaraji kuwa ni akiba yake na malipo yake kutoka kwa Mwenyezi Mungu peke yake, wala asijifananishe na wanafiki.