الأنعام
هذه ترجمة لتفسير السعدي كما ينشرها IslamHouse.com في saadi.islamenc.com، مقروءةً من صفحات ذلك الموقع. لا يذكر الموقع من ترجمها ولا أي طبعة مطبوعة تتبعها، ولا يذكر شروطًا لأخذ نصّها، ولذلك لم يُتحقق من حق عرضها. لم يقارنها أحد بكتاب مطبوع، ولم يراجعها أحد من العلماء. يقف كل مقطع بجانب الآيات التي يعلّق عليها، وهي نص القرآن من Tanzil كما هو عنده؛ والآية التي لا يعطيها الموقع شرحًا خاصًّا بها تقف مع المقطع الذي قبلها، ويسمّي الفهرس كل آية من هذا النوع. لم يكتب سبيل شيئًا منها ولم يترجمه.
النص منsaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)أُخذ في 2026-10-22
وَمَا ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَآ إِلَّا لَعِبٌ وَلَهْوٌ ۖ وَلَلدَّارُ ٱلْـَٔاخِرَةُ خَيْرٌ لِّلَّذِينَ يَتَّقُونَ ۗ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ٣٢
{32} Huu ndio uhakika wa dunia na uhakika wa akhera. Ama uhakika wa dunia, hiyo ni mchezo na pumbao. Ni mchezo katika miili, na pumbao katika nyoyo. Mioyo inauchezea, nafsi inaupenda sana, wasiwasi zimeshikamana nao, na kujishughulisha nao ni kama mchezo wa mtoto. Na ama akhera; hiyo ni "bora zaidi kwa wanaomcha Mwenyezi Mungu, ni bora hiyo yenyewe na katika sifa zake, na kubaki kwake, na kudumu kwake. Na ndani yake kuna yale yanayotamaniwa na nafsi na macho yanayafurahia; katika neema za nyoyo na roho, na wingi wa furaha, lakini si kwa kila mtu, bali ni kwa wachamungu, wanaotekeleza amri za Mwenyezi Mungu, na wanaacha makatazo yake na makemeo Yake. "Basi je! Hamtumii akili?" Yaani; je, hamna akili ambayo kwayo mnaweza kutambua ni gani kati ya hizi nyumba mbili ndiyo inayostahiki zaidi kupendelewa?